Sababu ya nyumba kuungua kwa tatizo la Umeme na utatuzi wake

Mr Electric

Member
Apr 26, 2019
10
28
SABABU YA NYUMBA KUUNGUA KWA TATIZO LA
UMEME NA UTATUZI WAKE:
Napenda kuwakaribisha katika majadiliano ya tatizo hili
ambalo limekuwa likisababisha majanga makubwa sana
hapa kwetu Tanzania kutokana na hasa kuongezeka
kwa matumizi ya umeme..
Uchambuzi nitakao utoa hapa ni kwa majibu wa elimu
yangu ya umeme pamoja ufahamu wangu juu sheria ya
umeme ya kimataifa IEE regulation.
Pia uchambuzi huu utazingatia British Standard of the
IEE Wiring Regulations. Kwani mfumo yetu mingi ya
umeme ya Kiafrika hata ule wa Tanzania ume-copy
kutoka katika regulation hizi kubwa mbili duniani.
Na sababu ya kutumia IEE wiring regulation ambayo ni
ya British standard 7671 ni kwa sababu inazungumzia
sheria na kanuni za umeme wa kiwango cha 230V kwa
single phase.Ambao ndiyo shirika la umeme Tanzania
Tanesco linausambaza kwenye makazi ya watu.
1.MAKOSA YANAYO SABABISHWA NA MAFUNDI
KWENYE KUFANYA WIRING.
(a). Overload of power supply wire:
Hii husababishwa na line moja ya power supply kutoka
katika main switch kutumika kusambaza umeme katika
vyumba vingi.
Mfano nyumba nyingi mafundi hutumia 2.5 mm2 wire
kama supply ya kwenye vyumba,supply hii hutumika
kama junction supply ya vyumba vingine.
Wire ya 2.5 mm2 kitaalamu mwisho wake wa kupitisha
current kiusalama ni 20Ampere ikitokea current zaidi ya
ishirini ikalazimishwa kupita katika waya ya namna hii
husababisha waya kupata moto,kama hali hii itakua
kubwa sana waya uungua. Na huenda ukasababisha
moto.
(b). Current ya Miniature Circuit Breaker(MCB):
kuwa kubwa kuliko current ya wire.
Mfano wire wa 2.5 mm2 tumeona kuwa una uwezo wa
kupitisha 20Ampere kiusalama
Hivyo MCB yake inatakiwa iwe ya 20Ampere.
Lakini mafundi wengine kwa kujua au kuto kujua
hujikuta wanafunga MCB zenye current kubwa zaidi ya
wire husika hali hii huweza kusababisha wire husika
kuungua kwani MCB itashindwa kujizima hata pale wire
itakapo kuwa imefikia kiwango chake cha mwisho cha
kupitisha current.
Matokeo yake wire husika unaweza kuungua na
kusababisha moto.
Viwango sahihi vya MCB na size ya waya zake zinazo
shauliwa kimataifa ni hizi hapa:
1.5 mm2 cable - 15 amp miniture circuit breaker.
2.5 mm2 cable - 20 amp miniture circuit breaker.
4 mm2 cable - 25 amp miniture circuit breaker.
6 mm2 cable - 32 amp miniture circuit breaker.
10 mm2 cable - 40 amp miniture circuit breaker.
(c). Loose Connection:
katika maungio ya waya na kwenye vifaa vinavyo funga
waya kwa screw.
Kama fundi hato kaza waya vizuri wakati wa kuziunga
pamoja katika viungo vya screw au waya kwa waya ni
chanzo kikubwa cha kutokea kwa cheche ambazo
hatimaye huweza kuanzisha moto.
(d). Tabia ya mafundi umeme kukubali kuunga mfumo
wa wiring wa nyumba nyingine dhidi ya nyumba
nyingine:
Kwa kawaida Tanesco huingiza umeme katika nyumba
kutokana na plan pamoja na mahitaji ya kiwango cha
umeme cha nyumba husika(Kilowatt Hour).Hili
hujumuisha ukubwa wa size ya waya wa kuingiza
umeme katika nyumba yako n.k
Pia waya unao ingiza umeme kutoka katika meter
kwenda ndani ya nyumba (tail wire) mara nyingi size
yake hutegemea mahitaji ya nyumba husika.
Hivyo nyumba inapo pewa umeme hua imejitosheleza
kwa mahitaji yake binafsi kitaalamu.
Inapotokea nyumba nyingine ikaungwa katika mfumo
huo wakati plan yake haikuhusishwa wakati wa kufunga
umeme katika nyumba ya awali hali hii hupelekea
OVERLOAD katika tail wire hali ambayo inaweza
kupelekea wire hiyo kuungua na kusababisha moto.
2. MAKOSA YA SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME
(a). Kuto funga Vilinda circuit wakati wa kufunga meter
za umeme.
Shirika la usambazaji umeme ni lazima lihakikishe
linaweka vifaa vya kulinda nyumba husika dhidi ya
matatizo ya umeme.
Shirika la umeme ni lazima liweke vifaa kama vile CUT-
OUT au CRCUIT BREAKER kabla ya umeme haujaingia
katika METER ya umeme au ndani ya nyumba
Ufungaji wa vifaa hivi ulikua unazingatiwa sana zamani
(sababu licha ya kuwa kama fuse CUT-OUT zilitumika
kukata umeme katika nyumba pale mteja akishindwa
kulipa bill ya umeme).
Sasa baada ya kuingia kwa meter za LUKU imeonekana
kama CUT-OUT hazina maana tena hivyo suala lake la
kutumika kama kifaa cha kulinda mfumo wa umeme
kama fuse limepuuziwa.
Kuna baadhi ya nyumba zimefungwa CUT-OUT hadi
sasa licha ya kuwa zinatumia LUKU,pia kuna wenye
bahati ambao mita zao zina Circuit breaker.
Ufungaji wa umeme usio zingatia vifaa hivi,unaongeza
uwezekano mkubwa wa kutokea short ya umeme yenye
madhara.
Kama umeingiziwa umeme katika nyumba yako halafu
vifaa nilivyo vitaja hapo juu hujafungiwa hata kimoja
(yaani umeme umetoka katika bracket na kuingia katika
meter moja kwa moja bila kupitia katika CUT-OUT au
CIRCUIT BREAKER ) mfumo wako wa umeme si salama
ni haki yako kufungiwa vitu hivyo una haki ya kudai
kwa usalama wa nyumba yako.
(b). Miundo mbinu mibovu ya shirika la ugavi wa
umeme.
Hali hii hupelekea kukatika katika hovyo kwa
umeme,hali hii huweza kuzalisha Electrical Surges
ambazo huweza kuleta madhara kwa watumiaji wa
umeme.
3. KUCHAKAA KWA WIRING ,VIFAA BANDIA NA VIFAA
VIBOVU .
(a) Circuit breaker mbovu au feki. Kuna circuit breaker
nyingine mbovu au bandia ambazo zinashindwa
kujizima pale short ikitokea,hakikisha unaijaribu circuit
breaker yako mara kwa mara kwa kubonyeza “trip test”
kuona kama inafanya kazi au la.
(b) Switch za umeme na extension cables ambazo ni
mbovu au hazijakidhi vigezo(bandia)ni chanzo kikubwa
cha moto katika makazi yetu.
Vifaa kama vile switch ambazo zimesha haribika
vibadilishwe ili kuepuka kutokea kwa moto.
Pia epuka kutumia Extension cables ambazo ni bandia.
(c) Wiring iliyo chakaa huweza kusababisha kutokea
kwa moto kutokana na kulegea kwa viungo vyake
ambavyo husababisha chehe,pia wire zake huwa
zimeshambuliwa sana na wanyama na wadudu hivyo
zinaweza zikagusana na kusababisha short yenye
kupelekea moto kutokea.
4. KUFANYA MATENGENEZO YA VIFAA VYA UMEME
NA KUVITUMIA BILA KUWA NA UTAALAMU:
Watu wengi wamekuwa wakifanya matengenezo ya
vifaa vya umeme angali hawana utaalamu wa
umeme.Vifaa vyote vya umeme ni lazima
vikatengenezwa na mtu ambaye amesomea kazi hiyo.
Mfano watu wengi hubadilisha fuse katika mifumo
mbalimbali ya vifaa vya umeme pale zinapo
ungua.Ubadilishaji wa fuse hizi mara nyingi hufanyika
kiholela bila kuzingatia kiwango cha current cha fuse
husika.
Hali hii husababisha fuse husika kuto kukatika wakati
short ikitokea hivyo huweza kupelekea waya kuuungua
napengine kusababisha short ya umeme.
5. KUJAZA VIFAA VINAVYO TUMIA UMEME KATIKA
EXTENSION CABLE KUZIDI UWEZO WAKE:
Extension cable zimetengenezwa kwa uwezo tofauti
tofauti.Hakikisha hauzidishi vifaa vya umeme vinavyo
chukua umeme kupitia extension cable yako ili kuepuka
uwezekano wa extension cable hiyo kuungua.
SOLUTION 1. 1. Makosa haya makubwa matano
yanaweza yakaepukika kwa kila mmoja kufata utaratibu
na kanuni za ndani ya nchi na za kimataifa zinazo
simamia matumizi bora ya umeme.
2. 2. Walaji wa umeme wawe na utaratibu wa kukagua
mifumo yao ya umeme mara kwa mara Kupitia
wataalamu wa umeme ili kuthibitisha usalama wa
mfumo wake wa umeme katika nyumba yake.
Utaratibu huu wa ukaguzi ni muhimu ambapo mtaalamu
atakagua kama wiring system yako imekidhi vigezo;
ambapo mtaalamu wa umeme hutakiwa kuchukua
vipimo maalumu na kuangalia kama mfumo wako wa
umeme umekidhi kanuni na taratibu zinazo simamia
mifumo ya umeme..
Baada ya vipimo mtaalamu huyo hutakiwa kuandaa
ripoti yenye taarifa ya ukaguzi na kutoa matokeo ya
ukaguzi huo wa mfumo wa umeme katika nyumba
yako.
Mkaguzi atatoa majibu makuu matatu kulingana na
sheria na kanuni za mifumo ya umeme majumbani
kuwa mfumo wako wa umeme ni (Salama,Salama
kidogo unahitaji marekebisho au si salama).Report hiyo
ataisaini na kukukabidhi.
3. Ufungaji wa vifaa vinavyo tambua ishara ya kutokea
kwa moto(fire sensor)
1. 4. Kuepuka kufanya matendo ambayo yatapelekea
kutokea kwa tatizo la umeme ambalo linaweza
kusababisha moto.
5.Kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika majumba
yetu.
Not always electrical fault will give you a chance to
correct your mistake.BE CAREFULLY!
.
Kwa mawasiliano na na shunghuli zote zinazo husu umeme wasiliana nami kwa 0620320089 / whatsapp
FB_IMG_1557476263958.jpeg
 
Asante kwa maelezo mazuri! Naomba kujua tatizo ni nini,
nina changamoto ninapotumia umeme hapa kwangu yaani nikiwasha TV au nikiunganisha cable ya computer mainswitch inazima. Sijui tatizo ni nini na mwanzoni nilkuwa natumia bila tatizo lolote.
 
Kwa mawasiliano na na shunghuli zote zinazo husu umeme wasiliana nami kwa 0620320089 / whatsapp View attachment 1093178
Fire sensor gharama yake tafadhali!
 
Daaa mkuu umetubariki sana na ushauri uliotukuka na tena umeutoa kwa weledi wa hali ya juu sana.
Ubarikiwe sana kiongozi.
 
Back
Top Bottom