Sababu ya Marekani kupiga yowe kuwa nchi za Afrika zinaficha takwimu za Corona ni kuficha aibu kuwa wao taifa kubwa limeshindwa kupambana na Corona!

Mkuu sijui ni tatizo la Taifa au kizazi kilichopo. Kuna ombwe la kufikiri na kutafuta ufahamu.
Takwimu za medical si sawa na takwimu za miti au malimao.

Takwimu za medical zipo katika Bio statistic na hutafsiriwa katika epidemiology.
Maeneo hayo mawili yanafanya kazi kwa pamoja kila moja liki suppliment jingine.

Huwezi kujua uwepo wa tatizo kama huna takwimu. Huwezi kujua trend ya ugonjwa kama huna takwimu.
Huwezi kujua 'factor' za tatizo kama huna takwimu.Huwezi kulikabili tatizo kama huna takwimu.

Mimi sioni kwanini tatizo la dunia Tanzania ilikatae kwa aibu. Leo tunasema hatuna Corona, je, ni kweli hatuna?
At the end of the day waathirika ni sisi na watakaolia au kubaki na tatizo ni sisi.

Nimesoma hoja ya ''takwimu' zinasaidia nini kila siku hapa jamvini. Nilichobaini ni kuwa ima wanaosema hivyo hawajui wanasema nini, au wanajua lakini wanapotosha tu .

Tanzania ni masikini kwasababu ya kizazi kama hiki kisichojua takwimu na bado tunategemea kuingia uchumi wa kati na mentality ya watu hao ambao wengine ni 'senior' katika vyombo mbali mbali tunavyotegemea!
Mkuu heshima yako.

Mimi nafikiri hapa pia kuna mambo ya kisaikolojia na evolutionary biology.

Watu washaingizwa chaka la habari za "us against them", herd thinking ya "Covid ni njama za mabeberu na WHO kutuangusha kiuchumi" na ujinga mwingine kama huo.

Sasa ukishafika level hiyo, na mambo ya "my country, wrong or right", ndipo unakuta mtu anahoji umuhimu wa kukusanya data.

He is simply wishing the problem away, he is blaming others, usually mabeberu, for this issue.Mtu analeta figisu zozote na conspiracy theory yoyote, ilimradi asi address the core issue kwamba ugonjwa upo na tunahitaji data kupambana nao na serikali haikusanyi data.
 
Hao si ndio wanafurahigi mwafrika anavyoteseka,waache wafe tu kadri kirusi covid 19 kitakavyoona inafaa
 
"Kiranga, post: 35602920, member: 13377"]
Watu washaingizwa chaka la habari za "us against them", herd thinking ya "Covid ni njama za mabeberu na WHO kutuangusha kiuchumi" na ujinga mwingine kama huo.
Na hapa kunashangaza. US,Italy , UK na nchi nyingi za magharibi zimeathirika na zinatangaza. Hao ndio mabeberu lakini wanaeleza hali yao.
Hivi nchi kama Marekani inasababu gani ya kuwa na kinyongo na Tz? Ni uchumi upi Wamarekani anaonea wivu?
Uchumi wa Jiji la New York ni mkubwa kuliko bajeti ya TZ. Kipi hasa hapa ambacho tunadhani Marekani wanakitaka.
Kama hujafikia, husomi wala huangalii habari za nchi kama Marekani , unaweza kudhani ni kama Morogoro!
Kuhusu WHO wana taratibu zao si kukurupuka kama rais wa Madagascar anayetaka dawa yake iingie sokoni bila kutafitiwa.
Sasa ukishafika level hiyo, na mambo ya "my country, wrong or right", ndipo unakuta mtu anahoji umuhimu wa kukusanya data.
Data hazitakiwi kwasababu zitaonyesha ukubwa wa tatizo. Kinachotakiwa ni kuficha mambo twende mbele. Hakuna sababu za kuficha takwimu ikiwa dunia nzima ikiwemo Brazil wanafanya hivyo.
Tunajiuimiza wenyewe. Wenzetu wakitufungia mipaka tunalalamika wakati tumeamua kuficha matatizo
He is simply wishing the problem away, he is blaming others, usually mabeberu, for this issue.Mtu analeta figisu zozote na conspiracy theory yoyote, ilimradi asi address the core issue kwamba ugonjwa upo na tunahitaji data kupambana nao na serikali haikusanyi data.
Mabeberu ni kisingizo tu.
Halafu tunawalaumu huku wanatuletea ARV. Inashangaza sana. Mikopo ya pesa tunawaomba wao.
Mashine za kupumulia tunanua kwao. Chanjo wanatupa bure ! Hata mashine za kukusanyia kodi za TRA zinatoka kwao. ha ha ha ha
 
Mkuu wewe upo nchi gani. Watu wanaugulia tu uko majumbani kwao. Kila wiki kitaa tunazika watu wanaokufa kwa ugonjwa usiojulikana.
 
Ila watanzania mishipa ya upumbavu ndiyo mingi zaidi. Hivi kweli tz imepambana na janga la koona!
 
Kinachowauma ni kwamba "mbona hawa kima hawafi na kupukutika kama sisi "?walitabiri kuwa watu zaidi ya robo bilioni watakufa sasa hapo ndio patamu nimetoka kuangalia wameisha fariki kwao kama laki moja na elfu kumi hivi hapo lazima kichwa kiwaume. Wana tabia flan hivi pakiwa na vita nchi yoyote basi wanatuma midege yao sijui airforce nininini sijui hawks kuja kuchukua raia wao sasa leo raia wapo humo humo wanawaya waya acheni mungu aitwe mungu tena basi mataifa yote yenye nguvu na healthcare bora kabisa ndo wanaongoza kwa vifo na maambukizi mengi.
 
Kinachowauma ni kwamba "mbona hawa kima hawafi na kupukutika kama sisi "?walitabiri kuwa watu zaidi ya robo bilioni watakufa sasa hapo ndio patamu nimetoka kuangalia wameisha fariki kwao kama laki moja na elfu kumi hivi hapo lazima kichwa kiwaume. Wana tabia flan hivi pakiwa na vita nchi yoyote basi wanatuma midege yao sijui airforce nininini sijui hawks kuja kuchukua raia wao sasa leo raia wapo humo humo wanawaya waya achani mungu aitwe mungu tena basi mataifa yote yenye nguvu na healthcare bora kabisa ndo wanaongoza kwa vifo na maambukizi mengi.
Uko sawa mkuu!
 
Kama wamarekani wanapambana vizuri kwa kutumia njia ya lockdown baada ya siku 14 tokea waweke lock down takwimu zingefika peak na kuanza kushuka
 
Back
Top Bottom