Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,265
- 105,432
Mkuu heshima yako.Mkuu sijui ni tatizo la Taifa au kizazi kilichopo. Kuna ombwe la kufikiri na kutafuta ufahamu.
Takwimu za medical si sawa na takwimu za miti au malimao.
Takwimu za medical zipo katika Bio statistic na hutafsiriwa katika epidemiology.
Maeneo hayo mawili yanafanya kazi kwa pamoja kila moja liki suppliment jingine.
Huwezi kujua uwepo wa tatizo kama huna takwimu. Huwezi kujua trend ya ugonjwa kama huna takwimu.
Huwezi kujua 'factor' za tatizo kama huna takwimu.Huwezi kulikabili tatizo kama huna takwimu.
Mimi sioni kwanini tatizo la dunia Tanzania ilikatae kwa aibu. Leo tunasema hatuna Corona, je, ni kweli hatuna?
At the end of the day waathirika ni sisi na watakaolia au kubaki na tatizo ni sisi.
Nimesoma hoja ya ''takwimu' zinasaidia nini kila siku hapa jamvini. Nilichobaini ni kuwa ima wanaosema hivyo hawajui wanasema nini, au wanajua lakini wanapotosha tu .
Tanzania ni masikini kwasababu ya kizazi kama hiki kisichojua takwimu na bado tunategemea kuingia uchumi wa kati na mentality ya watu hao ambao wengine ni 'senior' katika vyombo mbali mbali tunavyotegemea!
Mimi nafikiri hapa pia kuna mambo ya kisaikolojia na evolutionary biology.
Watu washaingizwa chaka la habari za "us against them", herd thinking ya "Covid ni njama za mabeberu na WHO kutuangusha kiuchumi" na ujinga mwingine kama huo.
Sasa ukishafika level hiyo, na mambo ya "my country, wrong or right", ndipo unakuta mtu anahoji umuhimu wa kukusanya data.
He is simply wishing the problem away, he is blaming others, usually mabeberu, for this issue.Mtu analeta figisu zozote na conspiracy theory yoyote, ilimradi asi address the core issue kwamba ugonjwa upo na tunahitaji data kupambana nao na serikali haikusanyi data.