ForeverMore
JF-Expert Member
- Nov 12, 2014
- 813
- 1,928
Ki ukweli, kama wewe kwa akili zako zooote, umekaa na kuwaza, ukafanya utafiti na jibu ulilopata ni kuwa Lissu angechukua nchi uchaguzi huu, walahi wewe ni KILAZA.
Magufuli kawa zunguka sana. Kapiga pasi ndefu.
Embu soma hiki
1. Wakati upinzani wamefanikiwa kufanya kampeni miezi 2 tu. CCM wamefanya kampeni miaka yote mi5. Yaani kila siku, mara Magufuli yupo huku, Majaliwa kule, Samia pale, Jafo Ndiyo kabisaa, Ummy Mwalimu naye kila sehemu. Safari zote hizo za "kusimamia" miradi ni kampeni. Wamefika karibia kila kona ya nchi.
Miezi miwili ya kampeni haiwezi tosha kuzunguka maeneo yote na kumwaga sera kwa ufasaha.
2. Watanzania wengi siyo watu complicated. Tupo simple, wachache ndiyo wenye uwezo wa kuchambua mambo.
Magufuli katumia miaka 5 kutuaminisha kuwa mabeberu ni watu wabaya. Miaka mitano (five years) kuonyesha msisitizo, alafu unatarajia Tundu Lissu katika miezi miwili ya kampeni, aweze kuwashawishi watu kuwa ni sawa yeye kuwa na wakili mzungu (Amsterdam) tena shoga. Haiwezekani.
3. Magufuli katumia miaka 5 kutuaminisha watanzania kuwa tunaibiwa mali asili zetu madini na wazungu. Na kuwa ni vita kubwa ya kiuchumi.
Lissu amekuja na kutarajia ndani ya miezi 2 atawabadilisha watu, Kweli? Tena anasema ataweka rehani madini kwa hao wazungu ili apate hela ya maendeleo wakati Magufuli akaweka sherehe ya kupokea Bil 100 kutoka Barrick siku chache kabla ya uchaguzi.
Kwa hili, Magufuli akafanikiwa kuwaonyesha watu kuwa sera ya kuweka rehani madini ni mbaya maana mbona tumeanza kupokea gawio la Bil 100?
Jamaa mjanja sana.
4. Miaka mi 5 yote, Serikali ya Magufuli imepambana kutengeneza uhusiano mzuri na viongozi wa dini zote. Katika kila uzinduzi, kila mkutano, viongozi wa dini wamealikwa na kuhudhuria. Na amehakikisha Kija Jumapili amehudhuria kanisani.
Kama unavyojua, watanzania wengi hasa vijijini ni wapenda dini.
Alafu unatarajia kutumia viongozi wawili watatu kwenye kampeni ya miezi 2 utaweza kuwa shawishi watanzania wengi waachane na mtu wanaye muona anaunga mkono dini? ni miss calculations kubwa sana.
5. Ni lazima upinzani uache kuangalia na kutunga sera za watu wachache wa mjini na kuangalia Watanzania wengi kwa mapana.
Sera ya Huru, haki na demokrasia ni sera nzuri lakini, inawagusa watu wachache.
Binadamu wengi ni Tomaso. Kwa wale wasiyoelewa, Tomaso ni kuwa mpaka uone ndiyo uamini.
Katika hili, mpaka janga la kukosa uhuru au haki inayotokana na serikali (CCM) limkute, hataona wala kuelewa maana ya huru, haki na demokrasia.
Haswa ukilinganisha na idadi gani ya watanzania walioguswa na kuielewa sera ya Elimu Bure, vituo vya afya, ujenzi wa barabara, reli, vivuko na kadharika.
Uongozi wa Upinzani hapa imechukua kero na matatizo walionayo wao ya kushitakiwa na kupelekwa mahakamani kila siku kuwa ni tatizo la watanzania wote. Hivyo wakaja na sera ya Huru, Haki na Demokrasia. Kwa hili wame zingua sana.
Kiukweli, ukiweka ushabiki pembeni, nakuangalia kwa makini hizo Point, unaona kabisa kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa Lissu kuchukua nchi mwaka huu.
Kama bado unadhani hivyo, siyo ishu. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Wacha tupambane na hali zetu. Tukatane tena 2025.