Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Wadau- kama tunavyishuhudia siku hizi polisi wanashindana na raia wa kawaida katika kufanya vitendo vya ujambazi, wizi, mauaji nk nk ingawa wao ndiyo wanatakiwa kulinda raia.
Habari za juzi za IGP Mwema, bosi wao mkuu kabisa kuibiwa upanga wa dhahabu unadhihirisha jinsi jeshi letu kuanzia juu kabisa hadi chinilimeoza. Mtu aibe kitu kutoka ofisi ya IGP? Naye (IGP) hata haoni aibu kujiuzulu? (Anyway kwa huyu Mwema kutoona aibu ni kawaida, kwani si mnakumbuka 2002 pale mahabusi 35 walipokufa kwa kukosa hewa kule Mbarali baada ya kufungiwa katika chumba kidogo bila ya kuwepo madirisha ya kutosha?) Mwema alikuwa RPC Mbeya.
Lakini sasa hivi kidogo twaanza kuelewa kwa nini katika jeshi letu la polisi kumeongezeka wimbi la maovu na uharamia wa kila aina -- ni kwa sababu hakuna wa kuwawajibisha na hii inatokana na kwamba nao wanatarajiwa, au wameagizwa kufanya kazi moja tu, kudhalilisha wapinzani kila pale sababu inapojitokeza, hata kama sababu yenyewe ni ndogo au isiyokuwa na msingi.
Kwa utawala wa CCM ambao umefikia mahala ambapo wanazidiwa sana na hoja za wapinzani, basi silaha yao kubwa ni kutumia polisi ili eti kuonyesha raia kuwa hawa ni watu wa vurugu tu. Ajabu ni kwamba mbinu hii walianza kutumia tangu zamani -- kwa NCCR, CUF na sasa CDM. Kwa CCM vyama vyote ambavyo huwa tishio kwa uhai wao, basi ni lazima vionyeshwe kwa umma kwamba ni vyama vya vurugu kwa sababu kihoja CCM haiwezi kuzijibu zile za upinzani.
Maneno 'uvunjifu wa amani' ndiyo umekuwa mwongozo mkuu kwao -- utadhani amani katika nchi huwa inasimikwa na jeshi la polisi. Ingekuwa hivyo, basi kusingekwa na vita katika nchi mbali mbali duniani, kwani si yapo majeshi ya polisi pia?
Hivyo basi wimbi la wizi, ujambazi, uharamia unaofanywa na polisi ni kama asante yao kutoka kwa utawala wa CCM kwa matarajio kwamba waendelee 'kuwadhalilisha viongozi wa upinzani.
Nawasilisha.