Sababu ya kutoa Choo kigumu,chenye harufu ya kutisha na kutoa gesi ya ukaa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
nipo arusha kwa siku kadhaa sasa.leo asubuhi hapa ofisini kuna jambo lilitokea mbalo kwa kiasi flani lilihatarisha hali ya utulivu ,amani na utengamano ambayo ilikuwepo ofisini. ndugu yetu mmoja wa kitanzania alipata nafasi ya kwenda kujisitiri na katika kutimiza haki yake hiyo ya kimsingi kabisa.pasipo kujua maskini alisababisha uchafuzi wa hali ya hewa na uharibifu wa mazingira tulivu yaliyokuwa yamejengeka mle ofisini.

choo cha ofisi yetu kipo sehemu flani si mbali sana ila kuna mlango unaojitegemea kukupeleka kwenye korido iliyopo ofisi hiyo ya mtakuja( yaani maliwato) jamaa alienda kujisitiri huko kitendo hicho kilikuwa gumzo sana kutokana na harufu kali ambayo jamaa alisababisha kuenea ofisi nzima.kiasi kwamba hata yeye ilikuwa imemganda.jambo hili lilipelekea watu wa usafi waitwe kwa ajili ya kwenda kushughulikia hilo eneo kwa kumwagia dawa na manukato kuondoa harufu ile kali.

Watanzania hasa wa mikoani tumekuwa na tatizo sana kwenye suala la ulaji. tumejikuta mara nyingi tukishindilia mavyakula magumu sana hasa usiku na kutokutumia kabisa matunda na mboga mboga. jambo hili limekuwa likisababisha watu wengi wapate choo kwa shida sana na tena bada ya muda flani kupita. nimeshawahi kwenda maliwato nikamsikia mtu wa chumba cha pili akijisaidia kwa mateso makubwa sana.akinung'unika,akisikitika na kuomboleza kwa maumivu aliyokuwa akiyapata. binafsi nlienda kwa haja ndogo ila ilibidi nitoke maana hali ya hewa ilikuwa mbaya sana.

jamaa alikuja kutoka baada ya dk 40. akiwa amechoka,macho mekundu na hana nguvu kabisa.hata alikuwa akitembea kwa shida sana.ulaji mbovu wa vyakula. mtu unaenda kulala usiku unakula ugali wa dona sijui sembe mgumu.maharagwe na nyama. au unakula makande na mavyakula magumu sana. matokeo yake digestion hai take place au inakuwa kwa shida sana. na hapo ndo mwanzo wa kuota ndoto mbaya...unaota unakimbizwa,unaota unakabwa au unatwangwa kwenye kinu.

hayo yote ni sababu mwili unahitaji nishati ili uweze kusaga saga chakula kile tumboni na wakati huo huo mwili unahitaji mapumziko.kwa hiyo kunakuwa na hali ya kuchanganyikiwa flan hvi ambako kunasababisha mhusika awe katika hali ya mashaka na ugegezi.mwili unakuwa bado unafanya kazi ilhali ni wakati wake wa kupumzika.

kitaalamu usiku unapaswa ule chakula laini.kula chakula kingi asubuh na mchana kiasi.ila usiku kula chakula laini na matunda kwa wingi.pia usisahau vyakula vyenye nyuzi nyuzi ,mboga za majani na maji ya kutosha. mnakula mavyakula magumu mnashindwa kwenda choo week nzima.mkija kwenda mnatoa choo kigumu pamoja na gesi ya ukaa. na huu ni uchafuzi wa mazingira.nimeshawahi kulalamika dada mmoja mzuri ambaye aliwah kujisaidia mpaka nikakimbia room.sababu ya harufu.(mtu unaweza kufa kwa harufu mbaya inayotoka huko) tuleni kwa mpango mzuri ndugu zangu.
 
Hiyo sio Arusha pekee kaka GuDume hii hali ni kwa Watanzania tulio wengi huwa hatujui namna ya ulaji ulio bora na wa mpangilio.

Endapo utaeleweka kwa ulichoandika nadhani ndio itakuwa mwanzo wa hao wanaopupu kwa zaidi ya dk 40 kupungua sababu inakuwa hiyo kitu haina tofauti na adhabu sasa ambayo sababu yake ni ulaji usioeleweka.
 
ni kweli unachosema .. nimezungumzia arusha coz i was there lakini hata dar hili jambo lipo.. watu hawajui kula.. wana ulaji mbovu na wa hovyo sana. mtu akienda kujisaidia anachukua saa zima mpaka masaa mawili akija kutoka amechooooooooka na anatembea kwa maumivu makali sababu yakujisadia choo kigumu .

Hiyo sio Arusha pekee kaka GuDume hii hali ni kwa Watanzania tulio wengi huwa hatujui namna ya ulaji ulio bora na wa mpangilio.

Endapo utaeleweka kwa ulichoandika nadhani ndio itakuwa mwanzo wa hao wanaopupu kwa zaidi ya dk 40 kupungua sababu inakuwa hiyo kitu haina tofauti na adhabu sasa ambayo sababu yake ni ulaji mbovu.
 
ni kweli unachosema .. nimezungumzia arusha coz i was there lakini hata dar hili jambo lipo.. watu hawajui kula.. wana ulaji mbovu na wa hovyo sana. mtu akienda kujisaidia anachukua saa zima mpaka masaa mawili akija kutoka amechooooooooka na anatembea kwa maumivu makali sababu yakujisadia choo kigumu .
Nadhani elimu zaidi inahitajika juu ya ulaji ulio bora ila nje ya hapo haiwezi kwisha hiyo hali sababu wenye kutambua ulaji ulio bora mpaka sasa ni asilimia ndogo mno.
 
Hiyo sio Arusha pekee kaka GuDume hii hali ni kwa Watanzania tulio wengi huwa hatujui namna ya ulaji ulio bora na wa mpangilio.

Endapo utaeleweka kwa ulichoandika nadhani ndio itakuwa mwanzo wa hao wanaopupu kwa zaidi ya dk 40 kupungua sababu inakuwa hiyo kitu haina tofauti na adhabu sasa ambayo sababu yake ni ulaji usioeleweka.
Naona umewahi nafasi ya mtu
 
watu wamikoani wanakunyaga Ghalika (storm)

Na awawezi kuacha kula Dona kwasababu uchumi ndo uko ivyo....alafu Acha zalau wewe Gudume.
 
Mkuu ulaji hovyo na kutokunywa maji ya kutosha.

Janga lingine ni pombe. Zipo pombe ukinywa cho chake kina harufu mbaya na kali. Sasa imagine ndio unywaji wa kudumu. Chukua senator, eagle, n.k linganisha na ndovu au castle lite.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom