Sababu ya kufeli kwa waandishi wa Tanzania

Investaa

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
789
654
Habari wa JF!

Leo nitaongelea muendelezo wa biashara ya uandishi wa vitabu, makala nyingi nilielezea biashara ya ebook ambayo mwandishi hawezi kupata hasara kama wanayopata sasa kwa wale wanaouza whatsapp na facebook.

Leo kwenye kupitapita youtube nimeona tangazo la nguli wa ushauri wa biashara na motivational speaker Joel. Nilikuwa namfuatilia sana makala zako especially youtube, ni miongoni wa waandishi wanaofanya vizuri na mwenye ushawishi mkubwa sana kwenye upande wa biashara.

Nitamtumia kama mfano kwenye makala ya leo ambayo ina title "SABABU YA KUFELI WAANDISHI WA VITABU BONGO".

Ipo sababu moja kubwa ambayo inawatoa waandishi wengi kuelekea kwenye mafanikio, sababu hiyo ni kuuza softcopy whatsapp.

Inafika sehemu wasomaji hawanunui hardcopy inabidi maisha yaendelea na kumforce mwandishi kuuza softcopy ili aweze ku survive kwenye jua hili kali na kuingia mtego wa kuuza softcopy kitu ambacho anaji sell short na kuua demand ya vitabu vyake kwa kusambazwa mtandao na wanunuzi.

Kumbuka bado hardcopy zipo madukani, wasomaji hawanunui tena kwasababu wanayo softcopy tayari.

Waandishi wengi wanaoandika vitabu vya biashara, wengi wao wana struggle kwenye marketing; mfano mzuri ni Joel.

Nikiona mwandishi anauza softcopy kwenye social media huwaga najiskia vibaya sana maana najua ana kwenda kuuza soko la vitabu vyake kwa kujisell short (Short term gain longterm pain).

Waandishi ni watu wanakandamizwa especially kwenye hardcopy, wakienda kwa publisher. Madharani wanakubaliana wataprint vitabu 1000, 200 vya publisher na 800 vya mwandishi. Mwandishi akimpa kisogo publisher, publisher anafanya yake na kusambaza chapu mikoa mingine ukienda kwa publisher unakuta mzigo bado upo.

Kipindi nafanya research nilipata stori kama hizi nyingi sana za kusalitiwa na publisher.

Kama huna future na uandishi unaweza endelea kuuza softcopy social media ila kama unataka kufanikiwa zaidi fikiria kulinda kazi yako ikiwa kwenye softcopy.

Nimejitahidi kutafuta chama cha waandishi wa vitabu tanzania kwenye google sijafanikiwa. Kama kuna waandishi wapo kwenye hicho wanachama naomba nijoin nataka niongee na waandishi kuhusu kuuza vitabu softcopy kwq faida bila kuua demand and supply kwenye soko.

Kiu yangu nikuona AMAZON KINDLE YA BONGO IMEZALIWA NA WAANDISHI WANAFAIDA NA TECHNILOGIA YA SASA KUPITIA SMARTPHONE AU COMPUTER.

Final word:

Nikiona mwandishi anavyoangaika namna hii kama picha zinavyoonesha hapo chini najiskia vibaya sana.

Solution ninayo ya kuponya hili tatizo ndio maana mara nyingi napenda kuwakumbusha mjatibu kutumia njia hii ya kisasa ya kuuza ebook kwenye app.

Kama kuna chamba cha waandishi wa vitabu naomba nipe link yake kupitia whatsapp 0652247221.

Pamoja tunaweza kufika mbali na kutimiza malengo tuliyojiwekea.

Screenshot_20220221-182625_YouTube.jpg


Screenshot_20220221-182620_YouTube.jpg


Screenshot_20220221-182611_YouTube.jpg
 
"Kama huna future na uandishi unaweza endelea kuuza softcopy social media ila kama unataka kufanikiwa zaidi fikiria kulinda kazi yako ikiwa kwenye softcopy"

Unachanganya yaani mpaka basi. Unaunga mkono soft copy au unapinga?

Wabongo hawapendi kusoma vitabu mtawalaumu waandishi bure tu. Ni mwandishi gani Bongo hapa aliyetoka kimaisha kwa kuuza vitabu vyake? Labda wanaobahatisha vitabu vyao kuingizwa kwenye mitaala ya mashule kama huwa wanalipwa vizuri.
 
"Kama huna future na uandishi unaweza endelea kuuza softcopy social media ila kama unataka kufanikiwa zaidi fikiria kulinda kazi yako ikiwa kwenye softcopy"

Unachanganya yaani mpaka basi. Unaunga mkono soft copy au unapinga?

Wabongo hawapendi kusoma vitabu mtawalaumu waandishi bure tu. Ni mwandishi gani Bongo hapa aliyetoka kimaisha kwa kuuza vitabu vyake? Labda wanaobahatisha vitabu vyao kuingizwa kwenye mitaala ya mashule kama huwa wanalipwa vizuri.
Nyambari nyangwine😂😂
 
Nyambari nyangwine
Nyambari Nyangwine ni sawa tu na Shigongo kwenye magazeti ya udaku. Walifanya timing nzuri sana kwa walichofanya kwa wakati wao na mimi nawaona kama exceptions tu; ndiyo maana sidhani kama cases zao zinaweza kuwa replicated.
 
Back
Top Bottom