Sababu ya kuendelea kuwa na rafiki huyu wa kike imepotea kabisa

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,454
12,767
Nisiseme jambo lolote nje ya mada yangu acha niende moja kwa moja kwenye tukio lenyewe.. nitaeleza sifa baadhi za msichana mwenyewe na mahusiano yetu yalivyo.

Huyu msichana ni jirani yangu wa miaka mingi tu, sikua na ukarbu nae sana hapo nyuma lakini pia nina share nae marafik baadhi wa kiume kwani tuliishi mtaa mmoja toka secondary.
Miaka mitano iliyopita alianza degree yake ya kwanza.
Mwaka huu pia tumekuja kukaa mtaa mwingine tukiwa wote tena, urafk ndo ukakolea sasa.

Naongea nae sana mala kwa mala na kuchat nae, hiyo yote mim nilikua nimeanza kumpenda..
i kiss her one time, lakini hakutaka mahusiano na mim na akadai anataka tuendelee kua marafik tu,
So mim nikaona isiwe tabu fresh tu,
Yeye husema hajawai kukaa kwenye mahusiano ya kimapenz (up to sex)
what she love more rather than sex?hatujui.
Tumeendelea kua marafik, nimemsimulia sana story zangu ya mahusino ya nyuma hadi mwanamke wangu wa kwanza, zote anapenda nae hizo story
Ni mshika dini mzuri kama mim pia, tupiga story za bible sana, na anatabia nzur tu kikawaida.

Sasa bhana, kuna siku alipata dili yani, niite dili la kufanya kazi fulani tu kwa muda fulani.
Kutoka kwa afisa elimu, tunakaa nae mtaa moja.
Basi siku hiyo naona alikua na furaha kidogo, kwa kupata extra money, na kudai anapenda awe busy hivo kila siku asiwe anakosa ubusy kama huo.
Kazi yenyewe ilikua ni kuandaa mitihani ya secondary (form 2).

Sasa aliponieleza akadai kazi yeye kaishia saa 3 usiku, lakin kazi hiyo inafanyika usiku kucha.
Nikamwambia kazi za usiku ndo fresh sasa si unaliunga tu.
Akasema daa alafu ningejua ningekuingiza ukafanye wew hiyo kazi.
Nikamuuliza kwanin hukufanya hivo.

Akadai nilikumbuka kwenu kuna kijana anasoma secondary, nikahofia shetani anaweza kukupitia..

Aliposema hivo nilibaki na maswali kama kumi..

Lakini kilicho nikeleketa na kunikwaza kupita yote, kua haniamini na anafikia hadi kunidhani jambo baya naweza fanya hata akinikataza, ananifananisha naweza kua mtu fulani bila kua na sababu yoyote.

Kilichonikwaza hata sio kukosa posho ya hiyo kazi, iko wapi Trust mim na yeye?
Alafu na kijana anae soma sasa hata akisikia habar za mtihani, awezi omba possible, darani ni kichwa balaa.

Uaminifu wangu kwake unamaana gani hadi hapo, nadhani ni wakati wa mimi kumtoa thamani niliyompa kwangu, na kumvika madhaifu kama yeye alivyo nivika.

Karibuni kwa mawazo yenu wakuu.
 
Kusema kweli,sijaelewa umekasirika nini.!
Huwezi kuelewa kama, rafiki na mtu wa karbu kwako ni mzazi na ndugu yako tu.
Wanao heshimu mahusiano au urafiki wa kukutana mbali na undugu tu ndio wataelewa uzi huu.
 
Mkuu nionavyo mimi,
Unamchukia tu, especially after rejection from her..
Acha mbinu za Nduli bana..
Unalilia kupendwa mpaka leo.
Kwanza huu uzi wako umekuvua nguo..hebu chutama kidogo.
What a loser.
(Sijawahi toa mchango kama huu, na wala msinisamehe)

sent from Samsung Galaxy A30
 
Nimesoma kidogo ikabidi nirudi kureview avatar ili kujiridhisha, hivi kumbe kuna @Suriya na Surya.?
 
Hapa wenye akili kubwa ndo wataelewa kuwa ujumbe wako haujabeba hisia moja tu,hata suala la bint kukataa muingie kwenye mahusiano imekuwa sababu kubwa zaidi ya kukufanya uwe na hasira nae na kutaka ushkaji ufike tamati,,,,na log off.
 
Back
Top Bottom