Sababu ya JK Kuwapenda Wanaomuangusha - Tuwe Makini 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu ya JK Kuwapenda Wanaomuangusha - Tuwe Makini 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Goodrich, Mar 15, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Kanuni inaonyesha kuwa mtu anapotimiza malengo huwa na furaha, na anaposhindwa kutimiza malengo huwa na hasira (frustration).

  Kwa Kiongozi, furaha huonekana kwa kuwapenda wasaidizi wake waliomsaidia kufikia hapo, na hasira huonekana kwa kuwa mkali kwa wasaidizi waliomuangusha.

  Hali inaonyesha kuwa JK ana furaha ya kutimiza malengo yake na hivyo anawalinda waliomsaidia kufikia hapo.

  Kukokotoa zaidi
  hesabu yetu, inaonyesha malengo yake ya kuutaka Urais yalikuwa ni ule Ujiko, Ulaji, Matanuzi na Ukuu.

  Therefore, ametimiza malengo yake na hana kinyongo na yeyote kati ya wasaidizi wake.

  Proof 1; Kama malengo yake yangekuwa ni kuinua uchumi, kujenga misingi imara ya utaifa, kulinda rasilimali zetu, na hivyo kuboresha maisha ya watanzania, basi pasingetosha. Asingekuwa na Malima, Ngeleja, Wasira, Mponda, Nkya, Sofia, Nundu, Shukuru nk katika baraza lake.
  Proof2; Asingekuwa na hofu ya 2015. Hofu yake kwa sasa ni jinsi 2015 inavyokaribia kwa kasi, na kila tatizo linapotokea anasema ni wabaya wake wa kisiasa wenye malengo ya 2015. ie hata kashfa za TBS, UDA, SONGAS nk anaamini zinazushwa na wabaya wake wa 2015.

  Conclusion; Tumejifunza katika aina hii ya utapeli wa kisiasa, tuwe makini 2015.
   
Loading...