SABABU: Ujio wa Obama na timu ya watu 700

Liganga

Senior Member
Jul 4, 2007
165
125
Heshima kwenu wale wote mnaotumia muda wenu na
akili zenu kuwajuza wananchi. Ningependa kidogo muelewe
na ntaweka baadhi ya vithibitisho kutoka vyanzoa mbalimbali
nini hasa ni sababu ya safari hii.


KWANZA:
Yapata miaka 3 iliyopita bara la ulaya na America yalikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi
na kuporomoka kwa mabenki na makampuni kadhaa. Jambo hili lilichangiwa kwa kiasi kikubwa
na bidhaa za kifedha (Financial products) ambazo ni aina mpya ya wizi na uchotaji wa mabilioni
ya fedha. Matukio haya yaliathiri kwa kiwango kikubwa masoko makubwa ya fedha na miradi mingi
inayotegemea uwekezaji kupitia masoko hayo. Matukio haya yaliwaacha pia wawekezaji wengi wakiwa
hoi na hasara kubwa, pia ilizaa kukosa imani na uwekezaji katika bidhaa makaratasi (yaani zile
zinazoendeshwa kwa speculations na financial models) au zisizo na soko nje ya soko kuu (disposal
market). Wahanga wakubwa wa mtikisiko wa uchumi yaani MABILIONEA kwa sasa wameamua kuelekeza
nguvu zao kununua bidhaa ambazo ukua thamani kila jua lichwapo, katika hilo bidhaa kubwa na ambayo
kihistoria imekuwa ikiongezeka thamani kila siku na kwa kanuni za kikomasi -> DEMAND & SUPPLY
haitakaa iporomoke thamani.


Bidhaa hiyo si kitu kingine bali ni ARDHI, hii ni bidhaa peke duaniani ambayo huwa imebeba bidhaa
nyingi nyingi na zenye thamani kubwa (mfano: madini, wanyama, majengo, akiba kubwa ya maji safi
yaliyochini)Pia tafiti nyingi zimeonesha kuwa kutokana na ongezeko kubwa la watu duniani, inakadiriwa
kuwa ndani ya miaka 20 ijayo ardhi na maji safi vitakuwa ni adimu sana duniani. Mabilionea hawa
wameanza kumiminika Africa, sehemu pekee iliyobaki ulimwengu yenye ardhi nzuri kwa shughuli
nyingi za kimaendeleo pamoja na kilimo. Africa pia inasababu nyingine kuu ya kuvutia hawa
Mabilionea, watu wake wengi ni maskini na viongozi wake wengi wanauchu mkubwa wa pesa.Hapa chini
nimeweka linki ya dokumentari ya Aljazeera ambayo inaongelea uporaji ardhi mkubwa na pia naweka
na video ya taarifa za kiintelijensi za mikakati ya mataifa makubwa:

Uporaji ardhi: Our Man in Sudan - Witness - Al Jazeera English
Intelijensia: imeambatanishwa


PILI:
Obama ni nani??? Watu wengi wameaminishwa Obama ni rais anayeweza leta mabadiliko na atakuwa na
nia njema na Africa kutokana na rangi yake na pia kuwa na mzazi aliyetokea Africa. Hapa ndio watu
wengi na waafrica kwa ujumla waliposhindwa kungamua mikakati mikubwa na ya mbali inayopangwa na hawa
mabilionea wakubwa (Capitalists) wanaotawala dunia. Mtashangaaa sana lakini, ukweli huwa ni mgumu
kukubalika vile vile kizazi chetu kinatumikishwa sana kiasi mwisho wa siku huwa akina muda wa
kuchakatua matukio na taarifa mbalimbali zaidi ya kutegemea magazeti, televisheni na blogu kuwajuza.
Ni wachache usumbua akili kuunganisha na kutafiti habari.

Dunia yetu inaendeshwa na mabilionea wachache na si serikali tunazoaminishwa kuwa zipo kuendesha
nchi zetu. Siasa kama vilivyosekta nyingine nayo iliishabinafsishwa. Obama ni chambo kilichowekwa
kuwezesha maliasili nyingi za kiafrica kupatika kirahisi bila kuhitaji nguvu ya ziada na mikakati
mizito. Je Obama ni mwafrika?? jibu lake lina utata maaana hata cheti chake cha kuzaliwa na taarifa
za mahali alipozaliwa vimejaa taarifa zinazochanganya sana. Cheti chake cha kuzaliwa kinaonesha
kazaliwa hospitali inayoitwa Kapi'olani Maternity & Gynecological Hospital, siku ya kuzaliwa ni
1961 Agosti 4, baba mzazi akiwa na Umri wa Miaka 25, mzaliwa wa nchi ya Kenya.

Lakini historia na kumbukumbu zingine zinaonesha kuwa hospitali hiyo haikuwa inatumia jina hilo
wakati Obama anazaliwa. Mwaka 1961 kulikuwa na hospitali mbili zilizojulikana kama Kapi'olani
Maternity Home na KauiKeolani Children's Hospital zilizokuja kuungana mwaka 1978 na kuanza kuitwa
Kapi'olani Maternity & Gynecological Hospital. Vile vile cheti hiko kinatamka baba mzazi ni raia wa
Kenya, lakini hakukuwa na nchi inayofahamika kama KENYA kabla ya mwaka 1963. Sehemu iyo ya Africa
mashariki ilijulikana kama British East Africa Protectorate. Kumbukumbu pia zinaonesha kuwa Obama
amewahi kuchapisha kitabu kinachohusu maisha yake na baba yake. Kwenye kitabu hicho Obama anamsifu
babayake kwa kujitolea kupigana kwenye vita ya pili ya dunia, WW II. Kwa waliosoma historia
wanatambua kuwa WW II ilikuwa kati ya mwaka 1939 na 1945. Hisabati ya haraka haraka inatuambia kuwa
mtu mwenye umri wa miaka 25 mwaka 1961 atakuwa na umri wa miaka 3 mwaka 1939 na kufikia mwaka 1945
atakuwa ametimiza miaka 9. Je, na ntaomba msaada wa wanajeshi walipigana vita hii (veterani)
watueleze kama na watoto wa miaka 3 walienda vitani kipindi kile au hata wala wa miaka 9 walikuwa
mstari wa mbele pia. Tunatambua kuwa mkoloni aliswaga watu wote waliokuwa na nguvu na kuwapeleka
vitani na kwenye mashamba yao, huku nyuma akiicha wazee, wanawake, wale dhaifu, walemavu na watoto.

Cheti hiko cha kuzaliwa kinamtambulisha mtoto kama ni wa jamii ya African-American wakati miaka
iyo raia wote wa marekani waliokuwa na rangi nyeusi waliitwa na kutambuliwa kama Negroes hadi miaka
ya 1970 mikakati yao ya kudai usawa ilipozaa matunda na kutambuliwa rasmi kama African-American.


TATU:
Wachina wameisha ikamata dunia. Tambueni ya kuwa muhimili wa nguvu za uchumi wa dunia uliishaamia
Asia. Miaka ya nyuma mataifa makubwa kiuchumi yaliungana na kuanzisha G5 baadae ilitanuka na kuwa
G8. Natumaini wote mwaelewa nini maana na makubariano ya wanachama wa G5, kimsingi haina tofauti
sana na yale yaliyojiri pale Berlin 1884 chini ya Bw. Bismarck, dhana kuu ikiwa ni kutoingiliana na
kuharibiana mikakati ya biashara zao ili wote kwa pamoja wafaidi. Waliokuwa mezani miaka ile ya
1884 walikuwa wajerumani, waingereza, wafaransa, wareno n.k Maana hawa ndio waliokuwa na nguvu
kubwa miaka ile, top 5 ya mataifa yenye uchumi mkubwa wakati huo ilikuwa ni iyo.

Kwa mlinganisho, top 5 ya leo ndio iyo G5 na imelazimika kupanuka na kuwa G8 ili kudhibiti hao watatu
wasiwapoke nafasi zao.Baada ya manyanyaso na taabu ya kujitanua, mataifa chipukizi ya Asia yaani
China na India yaliamua kutafuta mkakati wa kujikwamua kwenye makucha ya kibebure ili wapate nafasi
ya kukuza chumi zao kwa spidi kubwa isiyodhibitika na gavana za magharibi. Waliazimia kuungana na
mataifa makubwa kiuchumi na raslimali kutoka kila bara ili kuweza kuwa na msuli mkubwa. Hapo ndipo
walipozikaribisha Afrika ya kusini na Brazil. Pia ili kuweza kuhimili geo-political influence na
military muscle (samahani kwa kiingereza hapo)waliikaribisha Russia, taifa peke duniani nje ya
africa lenye utajiri lukuki wa rasilimali na ambalo linanguvu kubwa kijeshi duniani (zaidi ya Marekani).
Machache hujulikana kuhusu nguvu za kijeshi za Russia kutokana sera yao ya usiri,
na haya tuyajuayo ni kupitia mataifa ya magharibi.

Huu ndio ukawa mwanzao wa muungano wa BRICS (Brazil, Russia, India, China & South Africa) katika
safari ya kuiteka na kuimiliki dunia toka wanyanganyi wa magharibi waliowapora maendeleo na
teknolojia miaka ya 1770. Fanya utafiti kuhusu uwezo wa bara la Asia miaka iyo, nguv ya japan kule
Asia-Pasifiki, pamoja na teknolojia zilizokuwapo pale Forbiden city. China ndio taifa kubwa katika
kila nyanja ndani ya BRICS na hivyo ndio kiranja mkuu. Siku za hivi karibuni wachina wamewasha
indiketa yao na kuanza kuchomoka kwa kasi zaidi ya zile Scania za Marcopolo kule Chalinze-Segera.

Baada tu ya uongozi mpya kushika hatamu ulianza kufanya safari na makubaliano muhimu kibishara na
kiustawi na mataifa ambayo yatawezesha ustawi wao wa haraka, kwa kuanza kufunga mikataba na mataifa
yote yenye utajiri mkubwa (Tanzania, South Africa, Russia, Congo-Brazzaville) wa rasilimali
zinazoitajika kwa kiwango kikubwa China na sasa uongozi huo baada ya kuishapata uhakika wa chakula
(malighafi) chakutosha kulisha viwanda vyake, umeangia katika raundi ya pili ya kuhakikisha inapata
"masoko bila masharti" na hivyo kuanza ziara mabara ya Ulaya na Amerika na kufunga mikataba ya
moja kwa moja (bilateral) na mataifa yenye masoko makubwa (Hungary, Bulgaria, Turkey, Belgium,
Romania, German, Mexico, USA etc). Mojawapo ya safari muhimu kuliko zote ilikuwa ni ile ya nchi ya
Switzerland, ambayo inafahamika kama muhimili mkubwa wa masuala ya biashara kubwa za kifedha na
mihamala (transactions)ya rasilimali kama(mafuta & heavy metals) na commodities kama (ngano,
mchele, pamba, chai, kahawa). China imefanikiwa kuingia mikataba ya moja kwa moja na nchi hii na
kufungua ukurasa mpya wa mahusiano pamoja na kubadilisha mizani ya mtiririko wa bishara duania.

Lengo kuu la china ni kuitafuta sarafu mbadala kwenye biashara za kimataifa ili kuondokana na dola
kwenye mzunguko wa biashara za kimataifa. Kwa muda mrefu imekuwa ni agenda ya BRICS kuanzishwa
sarafu mpya ya kibiashara na kuachana na zile za magharibi (Euro & Dollar) ambazo ni dhana nyingine
za mfumo wa kibeberu. Naomba ujifunze kuhusu athari za sarafu za kigeni katika biashara yoyote.
Kwa ufupi china imefanikiwa kukubaliana na switzerland kuruhus kutumika kwa sarafu ya china katika
biashara kubwa moja kwa mojabila kubadilishwa na sarafu yoyote.


HITIMISHO:
Kwa waliomudu kutazama taarifa ya habari juu ya mkutano wa Obama na Xi, utaona jinsi Obama
alivyojawa na wasiwasi hata sauti yake ilikuwa kama inatetemeka. Pili mkutano ule haukuwa pale
Washington kama vile viongozi wengine wanapokuwa wameenda USA kukutana na raisi wa Marekani,
mkutano huu unafanyika California, eneo lilipendekezwa na Xi na watu wake. Obama na timu yake
wameitwa kukutana na Xi, na si vinginevyo, Tazama Aljazeera na utaona hata maelezo ya habari hiyo
leo yanaandikwa tofauti. Nimeambatanisha screenshot. China sasa ndio SUPER POWER!!!
View attachment 96829

TAFAKARI:
Kwa kutumia mfano wa timu za mpira (wengi wetu ni wadau)
China = Barcelona (Young, inteligent players, financially sound and ambitious)
USA = Real Madrid (Ageing giant, talented players, financially fit, has lost bearings)
Tanzania = Taifa Stars (Rookie, money-hungry players,ambitious coach -> JK and highly hopeful fans)

Je, tutaweza kupata ushind au draw na timu hizi mbili ambazo zimeisha omba mechi na sisi??
Je, ile mechi tuliocheza na Barcelona sirini, matokeo yake yalikuwaje??
Je, huu mpambano wetu na Real apo Julai 1, utaishaje???
Je, tumejiandaaje na mpambano huo na Real??


Nafungua ukurasa mpana wa fikra, mjadala na kukaribisha maoni endelevu.
 
Huo ni mtizamo wako tu, Rais wa mataifa yaliyoendelea wakisema waje kufanya ziara huku mnafikiria kunyang'anywa ardhi na rasilimali zingine ila nyie Rais wenu akienda huko mnaona poa tu eti anaenda kutafuta masoko na fulsa za uwekezaji...SAWA lakini mara nyingi tuwe tunaangalia mambo (hizi ziara) kwa mtazamo CHANYA na kujitengenezea fulsa za kupata chochote potential kupitia ziara hizo na sio daily kulalamika kama MAHAYAWANI. utajiri wa china au marekani haunihusu mimi maana hata TZ yetu ina mazuri yake na mabaya yake.
 
Duh hongera kaka kwa uchambuzi wa kitafiti kweli Tanzania sasa tumegeuka uwanja wa mapambano wa Mataifa haya yenye nguvu kubwa ya kijeshi na kiuchumi duniani.
 
C&P, conspiracy theories za ki-TEA PARTY na akina LUSH RIMBAUGH (eg. Obama alizaliwa Mombasa lakini mama yake akabadilisha documents ahesabike amezaliwa Marekani ili hapo baadaye aje agombee urais :shock:)
 
Hawa mabepari hawafanyi kazi ya KANISA wanapishana kuja TZ mwenye akili timamu anajua kinachoendelea.
Ni mwendo wa kukwapua rasilimali za mataifa changa kama Tz mwisho wa siku tutabakiwa na mashimo tuu kama kule Buhemba na migodi mingine ambayo soon inafungwa uku inchi ikiwa imeambulia almost patupu!
Kwa nature ya viongozi tulio nao na ulafi wao lazima tuwe wapole unless kuwe na mabadiliko siku za mbele uko otherwise we are in horrible situation
 
Huo ni mtizamo wako tu, Rais wa mataifa yaliyoendelea wakisema waje kufanya ziara huku mnafikiria kunyang'anywa ardhi na rasilimali zingine ila nyie Rais wenu akienda huko mnaona poa tu eti anaenda kutafuta masoko na fulsa za uwekezaji...SAWA lakini mara nyingi tuwe tunaangalia mambo (hizi ziara) kwa mtazamo CHANYA na kujitengenezea fulsa za kupata chochote potential kupitia ziara hizo na sio daily kulalamika kama MAHAYAWANI. utajiri wa china au marekani haunihusu mimi maana hata TZ yetu ina mazuri yake na mabaya yake.


Ungejiita chief mangungo,maoni yako yangekuwa Na urali sawia kabisa!!!
 
Huo ni mtizamo wako tu, Rais wa mataifa yaliyoendelea wakisema waje kufanya ziara huku mnafikiria kunyang'anywa ardhi na rasilimali zingine ila nyie Rais wenu akienda huko mnaona poa tu eti anaenda kutafuta masoko na fulsa za uwekezaji...SAWA lakini mara nyingi tuwe tunaangalia mambo (hizi ziara) kwa mtazamo CHANYA na kujitengenezea fulsa za kupata chochote potential kupitia ziara hizo na sio daily kulalamika kama MAHAYAWANI. utajiri wa china au marekani haunihusu mimi maana hata TZ yetu ina mazuri yake na mabaya yake.

Nakushukuru kwa kuwa wa kwanza kuchangia.

Vile vile nikurudishe apa kwenye TAFAKARI na kukusisitiza upasome japo mara tatu

na utapata jua dhima ya mjadala mzima ni nini. Mwandishi hana lengo la kulalama

bali kutaka watu wakune akili. Aina ya lugha, hoja na maneno kwa kiasi kikubwa

ueleza upeo wa mtu. Nakusihi rudia kusoma mara tatu na tuendelee na mjadala.
 
Je, kuna wakuwazuia timu hizo; Wameamua kuja wana kuja bila kizuizi na watakacho watafanya bila huruma!
You know WHY?
jibu:-
1. Siye ni vilema ( name it.)

2. Walipa kodi wao wamechoka kutulea.
Tutaomba hadi lini na Rasilimali zinaonekana....!
 
Mhuuuuuuuuuuuuuuuu acha niheme maana?

kwa mtindo huu. blueprint jr hana chake

duu pole sana mwanangu.
 
A very good analysis , mimi mwenyewe nilitaka kushangaa , umati wote huo unakuja Tanzania kufanya nini ? angalau sasa naanza kujua sababu , Asante sana mkuu .
 
Obama vs Jimping, and the battle field is Tanzania! Nothing else is there but Land, Natural Gas (NatGas) and Uranium! wakati Intelligence sevices za hao jamaa zikiwa busy kutafuta information juu hizo raslimali za TZ sijui kama TISS imejipanga ku-counter mashambulizi! Otherwise, ama raslimali zetu zitachotwa kwa bei cheee au zitageuka kuwa laana itakayogharimu uhai wa watanzania!
 
Mangungo wa Msovero alikua na akili kuliko viongozi wetu akina Fast Jet wa sasa hawa wa sasa wanahongwa vitu rahisi sana wakati Mangungo alipewa vitu vya dhamani sana kwa wakati huo
 
At least basi safari hizi zingekuwa zinawanufaisha Watanzania na kuwaondolea umasikini wao!!, lakini hapana. Badala yake tunaingia katika vitabu vya rekodi vya Guiness kwamba Tanzania ndio nchi pekee Duniani kuwahi kutembelewa na Marais wa Marekani waliopo madarakani From Clinton, Bush and now Obama
 
Liganga, huu ni uchambuzi mzuri na makini "think out of the box"

Ni rejee kwenye TAFAKARI hapo juu ambapo kinadharia naona mwamuzi wa kati ndio amebeba hatma ya mchezo huu. Kwa hakika mechi hii inahitaji mchezo wa kiu-ungwana (fair play) ili mashabiki wafurahie.

Obama na Rais XI: vituo vingi vya habari vimetangaza ni mkutano utakaojadili mambo ya Cyber Protection na kuangalia namna nzuri ya kuzuia Udukuzi unaofanywa na Uchina kwa taifa la marekani kiasi cha kuhatarisha biashara kubwa za wawekezaji wa Kimarekani, kuna madai ya siri za kampuni ya GOOGLE kuingiliwa na makampuni ya Uchina kwa Masada wa jeshi la nchi hiyo, mfano mwingine anaolalamikia Marekani ni jinsi Uchina alivyoiba siri za ndege zake aina ya F-35 na sasa Uchina anatengeneza mwenyewe.

Yapo mambo kadha wa kadha Merekani anadai kuchezewa faulo na Uchina. Nami nimalizie kwa kusema Uchina ni Barcelona katika soka!

Copy kahtaan
 
Last edited by a moderator:
Obama vs Jimping, and the battle field is Tanzania! Nothing else is there but Land, Natural Gas (NatGas) and Uranium! wakati Intelligence sevices za hao jamaa zikiwa busy kutafuta information juu hizo raslimali za TZ sijui kama TISS imejipanga ku-counter mashambulizi! Otherwise, ama raslimali zetu zitachotwa kwa bei cheee au zitageuka kuwa laana itakayogharimu uhai wa watanzania!

Vita iliishakwisha sahivi ni kuomba kutochukuliwa mateka, na ikitokea
umekuwa mateka ni kuomba mtekaji wako awe anaheshim the Geneva convention

Fuatilia yanoyojiri pande za California, Xi yupo pale na watu wake wana
dictate the future, Obama na timu yake wanasikiliza na kuomba nafasi japo
wawe na pakupumulia.

USA has failed in many endeavours in the recent decade, even its biggest
inteligence department has also flooped in many recent Ops. A deal went
bad in Benghazi and they lost a key agent (the ambassdor). Things are going horribly wrong
down in Damascus and now Barshad has regained the upper hand. Russia has applied brakes on
Israel Ops in the ares following delivery of SAM 300 system in the region.

Ukiishapanga matukio yote aya, utagundua wamarekani sasa ni kama Heavyweight boxer
aliyebananishwa kwenye kona ya ulingo, hana nafasi ya kutupa ngumi zaidi ya kujikinga
na mashambulizi ya mpinzani wake na kumkumbatia ili apate ahueni na kupumua.
 
Kwa kuwa ni wazungu wanakuja hakuna tabu,ingekua ni dege la mfalme wa uarabuni anakuja na umati wote huo pangechimbika kwa matusi
 
Hongera sana mkuu kwa uchambuzi wako mzuri!

Nashkuru.

Tuzidi kulichangia taifa. Hatuitaji sote kuketi pale magogoni,
chumba cha mashariki ili kuchangia mustakhabali wa nchi yetu.

Hata kupitia mtandaoni tupeleke mawazo yetu na michango pia.
Nuru ipo karibu, taifa linaenda kupona toka mikononi mwa walanguzi
 
Back
Top Bottom