Sababu Tanzania Kutohudhuria Mikutano ya EAC, SADC

Mkutano wa wakuu wa nchi huwa una changamoto nyingi,mojawapo ni lugha barrier!
KISWAHILI KILISHAINDINISHWA SIKU NYINGI KUWA LUGHA RASMI YA MIKUTANO YOTE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI,SADC NA AFRICAN UNION

NCHI ZA sadc ziko BURUNDI NA CONGO wanaongea kifaransa,Mozambique na Angola wanatumia Kireno nk

mikutano ya African UNION kuna nchi zinatumia kiarabu,kiingereza,nk hueleweki hoja yako

Lugha ipi ambayo ni barrier? wakati lugha kuu za mikutano ni Kiswahili,kiingereza,kiarabu,kireno na kifaransa.Waweza tumia lugha yeyote katika hizo
 
Atembelee kule akafanyaje? Nyie chadema mkiitwa wajinga mtakakataa?

Nini maana ya kuwa na Uhusiano wa Kimataifa? Nini maana ya kuwa na Mabalozi wetu katika Nchi tulizo na Mahusiano nazo na Nini maana ya kuwa na Mabalozi wa kigeni nchini Tanzania? Hamtaki kukubali Ukweli mmebakiza kumtetea Jiwe kwa hoja dhaifu!!
 
Uongo wa kiprof. huu. Ramaphosa alimpigia simu mkulu na mkulu akamwambia hatohudhuria kwa sababu za kilogistic. Sasa unawezaje wewe prof kusema mkutano ulikuwa wa nchi zinazopakana na SA tu. Kwani Tz tunapakana na SA?
ulimuona huyo Ramnaphosa wakati akipiga? ulihakiki hiyo namba kuwa anampigia magufuli? nyie ndio huwa mnafungwa jela kirahisi
 
Siasa ya sasa hivi bhana yani viongozi wanatuona sisi niwatoto wakati kilakitu vipo wazi tunaviona mtandaoni huku.
 
View attachment 1449851

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametoa sababu za Tanzania kutoshiriki kwenye mikutano ya kikanda ukiwemo mkutano wa Korido ya Kaskazini wa Jumuiya ya Afika Mashariki unaohusisha nchi nne pamoja na mkutano wa SACU uliotishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Profesa Kabudi alitoa ufafanuzi huo jana Mei 13,2020 Bungeni Mjini Dodoma.

Profesa Kabudi alianza kwa kuelezea mkutano uliohusisha nchi nne ambazo zinaunda Korido ya Kaskazini ambapo alisisitiza mkutano huo haukuwa unaihusu Tanzania ingawa ilikuwa na taarifa za kufanyika kwake.

"Mkutano ambao umefanyika ni wa Korido ya Kaskazini na walitutaarifu na tulijua, kwanini walitutaarifu lakini kwanini tuhudhurie mkutano wa Korido ya kaskazini? Ni wa kwao , ule haukuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Na sitaki kurudia aliyoyasema Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2012, hayo yamepita tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya hii ya Afrika Mashariki. Wana yao na sisi tusiwe sehemu ya hayo, ndwele si sifa lakini Tanzania haijawahi kuacha kusimamia maslahi yake pamoja na udogo wa nchi hii kiuchumi.

"Nchi hii imefanya mambo makubwa sana kwa hiyo nataka kuwahakikishia mkutano ule wa zile nchi nne ulikuwa ni mkutano wa majadiliano wa Korido ya kaskanini,lakini sisi na Rwanda tumekuwa na centre Corido , ndio maana sisi na Burundi hatukwenda, kwasababu Burundi ni Centre Corido.Kwanza utafanyikaje bila sisi kualikwa.Kwanza nilitaka hilo lieleweke na watu wasikuze,"alisema Profesa Kabudi wakati anatoa ufafanuzi.

Kuhusu mkutano ulioitishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Profesa Kabudi alisema kuwa Rais huyo hakuitisha mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),kwani mikutano ya SADC inaitishwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa kushiriana na Mwenyekiti .

Alisema kuwa mkutano uliotishwa na Rais Ramaphosa ulikuwa ni mkutano wa nchi ambazo ni majirani wa Afrika Kusini(SACU)ambao wengi wao wako SACU ukiondoa Zimbabwe ingawa inapakaa na Afrika kusini, Msumbuji na Angola na ndio maana nchi nane hazikuhudhururia.

Profesa Kabudi alizitaja nchi ambazo hazikuhudhuria mkutano huo wa SACU ni Tanzania, Zambia, Malawi,Madagasca, Mauritius, Comoro na DRC

Umeshindwa kuweka Video yake unawalisha JF members upupu wako. So sad.
 
Kama ni uzushi unaweza kuthibitisha with reference kuwa Rais Magufuli anaweza kutema yai kama alivyofanya Mhe.Mbowe juzi alipohojiwa na BBC English service.

Huu ni mwaka wa 5 Rais Magufuli yuko Ikulu lakini hajawahi kutembelea nchi yoyote ya Ulaya, Asia, Marekani n.k.!
Kulikoni??

FYI Mbowe alifeli licha ya kuwa anafanyiwa na msaidizi wake wakati ule Balile (UK) alipotaka kuwa angalau na ka-degree.
 
Kama ni uzushi unaweza kuthibitisha with reference kuwa Rais Magufuli anaweza kutema yai kama alivyofanya Mhe.Mbowe juzi alipohojiwa na BBC English service.
Mbowe ni form six division zero na ni mbunge.Magufuli ni PHD holder na ni Raisi wa nchi nani zaidi kuliko mwenzie hapo?
 
ulimuona huyo Ramnaphosa wakati akipiga? ulihakiki hiyo namba kuwa anampigia magufuli? nyie ndio huwa mnafungwa jela kirahisi
Acha kushabikia uongozi mbovu, corona haitakuacha kwasababu hiyo tunapaswa kusema pale tunapoona mambo hayaendi vizuri hata kama ulizaliwa ccm au chattle.

Sililiza anachosema Ramaphosa hapa kama unajua kiingereza:
 
Atembelee kule akafanyaje? Nyie chadema mkiitwa wajinga mtakakataa?
Alafu mwanangu ww unakulaga pesa za bure. Haunaga hoja kabisa wala reference. Hautafuti ushahidi wwte kutete hoja zako. Wala hata kusoma vitabu kutafuta maarifa hausomi. Unaamka huna hili wala lile unaingia popote hata bila kusoma na kupachika neno laolote la kupinga na kutukana.

Hao jamaa nawashauri watafute mtu mwenye uwezo wa kutete matendo yao dhalimu.
 
Magufuli anafurahi sana hii crap inavyomtetea.
Hawa jamaa sijui wanatuonaje yaani?
 
Hivi jamani tuwe wakweli, Nchi ya Kenya walikuwa na Lock down au Curfew?. Kwa sababu Kenya waliweka muda wa kutotoka kuanzia saa moja jioni mpaka Saa kumi na mbili asubuhi(07:00pm-06:00am) , lakini mchana wote watu wanazagaa mitaani wakiwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
 
Hivi kwanini watanzania hatutaki kuwa positive? Kuna shida gani hivi, kwanini kila kiongozi akiongea lazima kuongelea swala la 'maadui zetu'? Watu gani kila saa mnawaza mna maadui tu jamani, badala ku focus kwenye issues kila mara ni kupeleka lawama kwa maadui, maadui hao 2020 maadui gani. Tunapoteza focus wakuu. Tunakuwa kama watu wachawi bwana, mchawi ndio ambae hata ukimsalimia tu lazima atasema unamsalimia umdhuru. Haiwezekani tukawa na mawazo ya maadui tuuuuuuu kila siku na kila mara. Na bahati mbaya maadui wenyewe hawatajwi! Utaambiwa tu maadui zetu, mara tupo vitani na maadui zetu mara vita za kiuchumi na mabeberu, hivi kweli kwenye nafsi zenu mnaamini mna vita na wamarekani au EU kwenye uchumi? Marekani aache kuwa na vita kiuchumi na wachina au warusi aje kuwa na vita na Watanzania, watu ambao hadi vyoo anawasaidia bure, angekuwa na vita na nyie angewapa dawa za ukimwi bure muendelee kuishi? Angewapa vyandarua msiumwe na mbu msife na marelia, unawezaje kumsaidia adui yako vitani apone? Mnawaita mabeberu wana vita kiuchumi na nyinyi ila mnajua kabisa bajeti yenu ya mwaka asilimia 60 wanajazia pesa zao muweze hata kulipa mishahara yenu, tangu lini adui yako vitani akakusaidia uweze kuishi?

Hebu tuache sababu, tupambane na maisha yetu.
Umenena vema kabisa.
Tupambane kwenye uhalisia, hivi vita na maadui wa kufikirika tuachane navyo. Hizi ni fikra za kizamani sana, enzi ya mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na ubabe wake wote ila jamaa anaINFERIORITY mbaya sana.

Watu wenye tabia za kuwa na INFERIOITY COMPLEX huwa na msongo wa mawazo na msaada unaoshauriwa kwao ni COUNSELLING Failure to that it can lead them to commit suicide.....!
 
View attachment 1449851

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametoa sababu za Tanzania kutoshiriki kwenye mikutano ya kikanda ukiwemo mkutano wa Korido ya Kaskazini wa Jumuiya ya Afika Mashariki unaohusisha nchi nne pamoja na mkutano wa SACU uliotishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Profesa Kabudi alitoa ufafanuzi huo jana Mei 13,2020 Bungeni Mjini Dodoma.

Profesa Kabudi alianza kwa kuelezea mkutano uliohusisha nchi nne ambazo zinaunda Korido ya Kaskazini ambapo alisisitiza mkutano huo haukuwa unaihusu Tanzania ingawa ilikuwa na taarifa za kufanyika kwake.

"Mkutano ambao umefanyika ni wa Korido ya Kaskazini na walitutaarifu na tulijua, kwanini walitutaarifu lakini kwanini tuhudhurie mkutano wa Korido ya kaskazini? Ni wa kwao , ule haukuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Na sitaki kurudia aliyoyasema Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2012, hayo yamepita tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya hii ya Afrika Mashariki. Wana yao na sisi tusiwe sehemu ya hayo, ndwele si sifa lakini Tanzania haijawahi kuacha kusimamia maslahi yake pamoja na udogo wa nchi hii kiuchumi.

"Nchi hii imefanya mambo makubwa sana kwa hiyo nataka kuwahakikishia mkutano ule wa zile nchi nne ulikuwa ni mkutano wa majadiliano wa Korido ya kaskanini,lakini sisi na Rwanda tumekuwa na centre Corido , ndio maana sisi na Burundi hatukwenda, kwasababu Burundi ni Centre Corido.Kwanza utafanyikaje bila sisi kualikwa.Kwanza nilitaka hilo lieleweke na watu wasikuze,"alisema Profesa Kabudi wakati anatoa ufafanuzi.

Kuhusu mkutano ulioitishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Profesa Kabudi alisema kuwa Rais huyo hakuitisha mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),kwani mikutano ya SADC inaitishwa na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa kushiriana na Mwenyekiti .

Alisema kuwa mkutano uliotishwa na Rais Ramaphosa ulikuwa ni mkutano wa nchi ambazo ni majirani wa Afrika Kusini(SACU)ambao wengi wao wako SACU ukiondoa Zimbabwe ingawa inapakaa na Afrika kusini, Msumbuji na Angola na ndio maana nchi nane hazikuhudhururia.

Profesa Kabudi alizitaja nchi ambazo hazikuhudhuria mkutano huo wa SACU ni Tanzania, Zambia, Malawi,Madagasca, Mauritius, Comoro na DRC
Ni Uongo. Asome ripoti ya mwisho (Final Communique). Inasema ni viongozi wa EAC waliokutana, na inatoa maelekezo kwa watendaji wa EAC na serikali za ndani ya EAC. Hiyo northern corridor haipo kabisa.
 
Back
Top Bottom