Sababu tano talaka kuweza kuwa mwisho wa Diamond Platnumz

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Divorce act inahusu watu walio nje ya ndoa pia: NENO TARAKA LIMETUMIKA KWA KUKOSEKANA KWA TAFSIRI YA KISWAHILI
NOTE: PLEASE, SOMA ARTICLE NZIMA KABLA YA KU COMMENT ILI KUELEWA MADA.
Vyanzo vya ushaid vimeandikwa chini ya article
thanls


Sio ajabu kupenda kusoma kuhusu utajili wa wasanii na mahusiano yao.Mwanzo na tamati imekuwa kivutio. Kufikia mpaka wasanii kuyatumia kama njia ya matangazo, kwanzia shilole, diva, jokate, na wengineo: ugomvi umefikiliwa kama nafasi ya kukuza jina na sio vinginevyo. Mtazamo huu haukuwa tofauti kwa wanaume; mpaka sasa.

Kuvunjika kwa mahusiano kati ya diamond na zari kunaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa diamond platnumz. Shangaa hii si mara ya kwanza diamond kujunjika kimahusiano na mtu, mwanzo ikiwa wema, hii itakuwa mara ya kwanza na mtu anayeweza kumuumiza, sio kisifa, bali kiuchumi.

Mi nasema, kunatofauti kubwa kati ya diamond na msanii wa kawaida. Zaidi ya kuwa msanii, ye ni mfanya biashara mahili , mwenye makusudi. Diamond anajua jinsi ya kutumia nafasi, kuwekeza fedha sehemu nyeti, kukuza jina, na kuvuna matunda, ndo maana mpaka sasa, bidhaa tatu zenye mafanikio; zina jina lake. Na mpaka sasa yupo kwenye process ya kufungua tv na radio station; ambayo itamuongezea umaarufu, na mwishowe, fedha zaidi za kuwekeza. kwahiyo waweza sema: kitu muhimu kinachomjenga diamond ni fedha, na uwekezaji wa hizi fedha. Bila fedha mafanikio yatakua magumu; na ni hiki kilicho hatarini pale zari alipotangaza kumuacha diamond. Tena mi nasema: hatari ilianza pale diamond aliponunua nyumba na kuhamishia familia yake south africa. Sababu kubwa ikiwa ni sheria, hasa hasa sheria namba 70 ya mwaka 1979 (SA GOV, 1979).

Baada ya zari, kutanganza mwisho wa mahusiano, akitaja uaminifu kama sababu; sheria ya utengani ya south afrika inampa option nyingi kupata haki yake. Elewa kwamba anaweza kupuuzia na kudeal na issue nje ya mahakama, lakini hii si bila diamond kutoboa mifuko. Namaanisha, sheria ya huko si kama ya nyumbani; kwani; chini yake watoto hupewa kipao mbele, anayefuata ni mwenza wa kipato cha chini; hawa mara nyingi ni wanawake, ikiwa ni kawaida kwa wanawake kutooa wanaume chini ya uwezo wao kiuchumi, na wanaume kuoa wanawake wa kipato kidogo.

Vitu vinavyozingatiwa ni; mali zilizovunwa, support ya watoto, utunzwaji wa watoto, na alimony (SA GOV, 1979). Kiwango cha fedha kitakachozingatiwa kuhusu mazingatio hayo; itakuwa juu ya zari: kwani ye ndo atakuwa mlezi, na ye ndio wa kipato cha chini.

Kwa undani, malipo ya kwanza, yataenda kwenye support za watoto kwa mwezi yakihusisha elimu. chakula, nyumba, na afya yakizingatia hadhi ya maisha waliyoyazoea kabla ya kutengana. Hii ni ngumu, kwani hadhi ya maisha huwa inategemea na mtazamo wa mtu; mara nyingi wanawake huwa wanaona wanalipwa kidogo, wakati wanaume wanaona wanalipa sana. Mahakama itaangalia ushaidi wa kiasi gani watoto walighalamikiwa kabla ya kutengana, na kuangalia kipato cha baba. Kwa maisha ya kiwango cha chini, mtoto wa south afrika mmoja, anaghalimu million 19 ya tanzania kwa mwaka, kwa mtoto wa msanii mkubwa, atakaehitaji malezi ya juu, shule binafsi, afya binafsi, nguo, na chakula; hii namba inaweza fika 30 (Hawthorne, 2017). Zaidi ya hapo, kuna watoto wawili, kwahiyo 60, na bado ada na chuo mbeleni. Na zaidi ya hapo, mahakama utoa fomu itakayo hitaji malipo ya; burudani, petrol, pocket money, insurance, na savings.

Haya malipo ufanywa tofauti na malipo ya mtoto. Elewa kwamba, wakati diamond na zari wakiwa pamoja, malipo haya mara nyingi yalifanywa na wazazi wote; kwa sababu ya utengano, mahakama huwa uhitaji mzazi mmoja kulipa peke yake. Malipo haya yatafanyika hadi watoto wafikie umri wa miaka 21. Na hata kama akioa: mahusiano mapya hayaluhusiwi kudhulu mahusiano ya zamani.

“Parties cannot use self-created reduced circumstances to reduce their maintenance obligations”

Ya pili, ni mali zilizo vunwa (SA GOV, 1979). Hii itakua ngumu kwani hawakuoana, kwahiyo inaweza bidi kwenda mahakamani, na mara nyingi mahaka ukabidhi asilimia 50 ya kila kitu anachomiliki mwanaume; kila kitu nyumba, magari, bank accounts, nakadhalika. Na kwasababu zali ni mlezi, nyumba ya southafrika: shangaa diamond bado itabidi aendelee kuilipia: zali ataendelea kuishi na kumiliki.


Ya tatu ni watoto, hawa atapewa mwanamke. Shangaa sheria inakataza upendeleo wa jinsia, karibia mda wote, watoto hupewa mwanamke (SA GOV, 1979). Lakini kibaya zaidi, mwenye dhamana ana uwezo wa kumnyima mwenza mida ya kutemebelea watoto na kama hataweza, anaweza kusukuma mahakama kuzuia mwenza asione watoto wake moja kwa moja, mpaka wafike umri au awaone chini ya usimamizi. Watoto hutumiwa kama siraha nzuri kwenye mda wa majadiliano, ili kumsukuma mwenza kuongeza malipo

Ya nne ni alimony (SA GOV, 1979). Shangaa diamond hakumuoa zari, bado ataitajika kulipa “spouse maintanance”; hii ni kuruhusu mwanamke aendelee maisha aliyo yazoea wakati yupo ndani ya mahusiano mpaka pale atakapoweza kujimudu kiuchumi tofauti na malipo ya watoto, haya ni ya moja kwa moja mpaka, mwanamke akioa, akipata kazi itakayo mruhusu kujitegemea, au akifariki (SA GOV, 1979). Mara nyingi wanawake hutaja bei ya juu ili kusukuma majadiliano yenye faida. Asilimia 30 ya case uishia mahakamani, hii uongeza bei ya kesi kwa mwanaume. Avarage cost ni million 30; ukizingatia wanasheria (Hawthorne, 2010). Ugomvi utokea pale unapofika mda wa makadilio: kwani ni vigumu hasa hasa kwa wasanii; kwani wataalamu watahitajika kutoa ushahidi: je msanii anaingiza na aweza ingiza shii ngapi, accountants kuangalia mabo ya kodi, na wanauchumi kuhusu bonuses na faida za biashara, hawa wote watakwa kulipwa na watachukua mda wa mahakama. Zaidi ya hapo, ni kawaida kwa wanawake kuchagua kutofanya kazi, au kuoa ili kuendelea kupata malipo maisha yao yote

Ya mwisho ni malipo ya wanasheria (SA GOV, 1979). Diamond akiamua kupinga, atapewa siku 20 kuaandaa team ya wanasheria na kwenda mahakamani. Cost inatofautiana kutoka kesi mpaka kesi, avarage cost ya kesi huwa ni million 20, kesi hizi uchukua mpaka miezi 16, na kwa mida mingine wanaume huwa wanafilisika, kabla ya kushidnwa kesi. Kwa wanawake ni vyepesi kwani wanasheria huwa wapo tayali kutoa support pro bono; wakitegemea malipo pale tu watakaposhinda kesi, na kutotaka malipo wakishindwa kesi. Na mara zote, tofauti na Tanzania, wanawake huwa hawashindwi kesi, na sio ajabu kwa wanaume kufilisika

Kwahiyo, kwa sasa. uchumi wa diamond upo chini ya huruma wa zari. Kama ana nia, anawezekana kumsukuma mahakamani na ikamgharimu nusu ya mali zake. Malipo ya watoto mpaka miaka 21, matunzo ya mwenza mpaka kifo, malipo ya nyumba mpaka miaka 21, na gharama za wanasheria kuendesha kesi kwa pande mbili. Malipo haya yatapanda akiendelea kufanikiwa, na mara chache sana hushushwa lakini ni baada ya kesi mahakani. Kwa msanii ayetegemea fedha kukuza jina, biashara na sanaa yake; gharama hii itamuumiza kwa njia moja au nyingine. Na sio kitu cha ajabu, wasanii kufilisika baada ya kutengana na wenza

References (VYANZO)
Hawthorne, T., 2010. How much maintenance? [Online] Available at: How much maintenance? [Accessed 11 January 2018].

Hawthorne, T., 2017. How much does it cost to raise a child in SA? [Online] Available at: How much does it cost to raise a child in SA? [Accessed 05 January 2018].

SA GOV, 1979. Divorce Act 70 of 1979. [Online] (1) Available at: http://www.justice.gov.za/legislation/acts/1979-070.pdf [Accessed 10 January 2018].
 
Taraka ya nini wakati hawa ni washkaji tu wamekutana mtaani wakazaa watoto.Hakuna sehemu inapoonyesha wameoana
 
Back
Top Bottom