Sababu tano kwanini unatakiwa kutumia viazi mviringo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Je, umeshawahi kufikiria kuacha kutumia viazi? Nina habari ambayo inaweza kukushangaza kuhusu viazi mviringo. Siyo tu kwamba viazi mviringo ni vitamu na vinabei nafuu, kuna faida nyingi za kiafya mabazo mtu anaweza kuzipata iwapo atatumia viazi mviringo.

Hizi ni sababu kuu tano.

1. Hauwezi kuwa mnene iwapo utatumia viazi mviringo
Ingawa viazi mviringo vina wanga, kwa upande mwingine matumizi yake yanaweza kusaidia katika program za kupunguza unene au uzito. Chuo Kikuu cha Califonia kimefanya tafiti zilizoonyesha kwamba unaweza kupunguza uzito bila kupunguza matumizi ya viazi mviringo.

Wanasayansi walifanya tafiti na kugundua kwamba kunauwezekano mkubwa kwa watu kupunguza uzito wa mwili kwa kupunguza kiwango cha mlo wote wanaotumia bila kuzingatia kuacha ulaji wa aina fulani tu ya chakula.

2. Viazi mviringo vinamfanya mtu kuhisi ameshiba
Kiazi kidogo kinaweza kuupatia mwili cha nguvu za kutosha kuliko vyakula vingine kama vile vitokanavyo na nafaka, samaki, nyama matunda na mbogamboga. Hii itasaidia katika kupunguza kiwango cha mlo utakao fuata.

3. Viazi mviringo vinakiwango kikubwa cha madini ya potassium.
Kiazi kidogo cha mviringo kinaweza kikawa na gramu 620 za madini ya potassium. Hiki ni kiwango kizuri ambacho iwapo kitatumika kitasaidia katika mzunguko wa damu na kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya mzunguko wa damu kama vile presha na magonjwa ya moyo. Mtu mzima nahitaji gramu 4,700 za madini ya potassium kila siku kwahiyo iwapo utatumia viazi mviringo kila mara itakuweka katika position nzuri.

4. Viazi mviringo vina vitamini C kwa wingi
Kiazi mviringo chenye saizi ya kawaida kinauwezo wa kukupatia asilimia 45 ya kiwango cha vitamini C unavyohitaji kwa siku. Watafiti wanaamini kwamba vitamini C ni muhimu katika mwili wa binadamu kwani husaidia katika kupambana na maradhi na kuimarisha ngozi na fizi. Kama unatatizo la kutoka damu kwenye fizi tumia viazi lafu TUONEEEE.

5. Viazi mviringo vina madini ya chuma.
Ingawa viazi mviringo havitumiwi kama chanzo kikuu cha madini ya chuma, kiazi mviringo chenye saizi ya kawaida kinaweza kuupatia mwili asilimia 6 ya kiwango cha madini ya chuma kinachotakiwa kwa siku. Hii ni habari nzuri kwa wasiotumia mazao ya nyama (Vegetarian). Madini ya chuma ni muhimu kwenye mwili wa binadamu kwani husaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu na usafirishaji wa hewa ya oksijeni mwilini.
 


anything you lose from being honest, you never really had to begin with.
 
Mmmmh ngoja niongeze spidi ya kula

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Wanaume wa dar watagurahi hapa maana vinatengeneza chakula Chao kikuu(vibanzi au chips)

Sent from my HUAWEI Y625-U32 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ungeweka zinaongeza nguvu za kiume vingekimbiliwa kinoma.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Wanaume wa dar watagurahi hapa maana vinatengeneza chakula Chao kikuu(vibanzi au chips)

Sent from my HUAWEI Y625-U32 using JamiiForums mobile app

Hapa nafikiri (upeo wangu) chips haziingii kwani mara vitu vyakukaanga hupoteza ubora wake kwa ukuaji Wa afya, hapa full mchemsho au kuivisha kwa mvuke
 
Grams 4700!??? Yaani kilo nne karibia tano!?

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom