Sababu saba kwa nini uzito wako utakuja kukuua ndani ya miaka mitano

Melkiad Jr

New Member
Nov 9, 2018
3
1
SABABU SABA KWA NINI UZITO WAKO UTAKUJA KUKUUA NDANI YA MIAKA MITANO.
Uzito ni moja ya tatizo kubwa sana kwa sasa katika afya za walio wengi na madhara ya UZITO uliopitiliza ni makubwa na yanatisha sana kiafya katika maisha ya watu wengi.
Ikiwa watu wataelimishwa juu ya madhara mbalimbali yatokanayo na uzito ni dhahiri kabisa wengi wataepukana na madhara hayo na wengi watakuwa wakichukua hatua za mapema katika kukabiliana na tatizo la uzito.
Uzito unapopitiliza katika afya ya mtu huwa kuna baadhi ya changamoto ambazo mtu huanza kuzipitia au kuzihisi kwenye mwili wake.

Sote tunajua kuwa tunatakiwa kufanya mazoezi, kula mboga za majani na matunda kwa wingi na kupunguza idadi ya vyakula vilivyo kaangwa, vyenye chumvi na vitamu tamu mfano vyakula vyenye sukari. Lakini pamoja na kujua hayo yote bado tunaendelea kuyafanya na mwisho wa siku tunapata madhara mengi sana na siku zote tatizo sio kujua bali ni kwenye utekelezaji wa kile unachokijua.

Na watu wengi hawana tabia ya kufanya mazoezi mpaka waambiwe na daktari kuwa wapunguze mwili ila bila hivyo wataendelea na mifumo yao mibovu ya maisha lakini tambua kuwa mazoezi ni afya na sio tu kupunguza mwili na ni muhimu sana kwani faida zake ni maradufu.

ZIFUATAZO NI SABABU SABA KWA NINI UZITO WAKO UTAKUJA KUKUUA NDANI YA MIAKA MITANO USIPOCHUKUA HATUA.
1. Kuwa na uzito una hatarisha maisha yako kwani wana sayansi wanasema kuwa watu wenye uzito huwa wanakufa mwaka mmoja mapema kabla na wenye uzito mkubwa zaidi wanakufa miaka mitatu mapema.

2. Uchovu wa mwili na maumivu ya viungo.
Uzito unapokuwa mkubwa vile vile mtu huandamwa na uchovu wa mara kwa mara. Mfano kusinzia sinzia ovyo, kuamka umechoka sana, hufanya akili yako kutofikiri kwa haraka yaani unajikuta umekuwa mzito kufikiri. Kuwa na uzito mkubwa unasababisha ukiwa unapandisha ngazi uwe una hema ovyo, unachoka mapema na ukienda kulala unakoroma sana. Pia maumivu ya viungo kama vile kiuno, magoti, miguu, uti wa mgongo, nyonga n.k

3. KUPANDA KWA KIWANGO CHA MAFUTA MABAYA KWENYE MISHIPA (Cholesterol).
Hii husababisha mtu kupungukiwa na damu na baadhi ya sehemu kutokusambaziwa damu katika kiwango kinachotakiwa,na mwisho wa siku mtu anaandamwa na tatizo la ganzi katika baadhi ya sehemu zake za mwili pia matatizo ya moyo kama vile moyo kuzungukwa na mafuta mabaya(Cholesterol).

4. MATATIZO KATIKA MFUMO WA UPUMUAJI.
Suala la kukoroma sana au kifua kubana nalo hujitokeza kwa mtu huyu. Hii inaweza kutokana na njia zake za pua kuzingirwa na nyama zilizoongezeka kutokana uzito wa umbo lenyewe ambalo ameshalibeba huyu mtu.

5. MATATIZO YA SUKARI NA PRESHA MWILINI.
Kupitia suala la kuwa na uzito uliopitiliza mtu huanza pia kuandamwa na changamoto ya sukari mwilini mwake kuongezeka,jambo linalopelekea baadhi ya viungo vya mwili kama INI, KONGOSHO, MAPAFU na moyo wenyewe kushindwa kufanya kazi zake kiufasaha. Matatizo ya presha ya damu hii huanza kujitokeza ndani ya afya ya mtu kama vile matatizo ya kupanda au kushuka kwa presha yake ya damu mwilini ambayo husababishwa na uzito anaokuwa nao tayari kwa wakati huo.

6. MATATIZO YA KUKOSA CHOO MUDA MREFU.
Mwili unapokuwa na kilo kubwa sana kuliko unazopaswa kuwa nazo kutokana na urefu wako na kilo zako tambua kuwa hata mfumo wa chakula unakuwa duni katika kufanya kazi ya umeng'enyaji wa vyakula unavyokula. Matokeo yake mwili unakuwa unapaki vyakula hivyo kwa muda mrefu tumboni na kusababisha kuwa na tatizo la kutokupata choo.
Pia uzito mkubwa unakufanya uwe na muonekano mbaya yaani unaonekana mzee kuliko umri wako, mwili unatoa harufu ukimaanisha kuwa ndani umeshaoza na unakuwa na changamoto ya ngozi.

7. Mfumo wako wa uzazi uko kwenye hatari kubwa sana.
Kama wewe ni wanaume wenye uzito mkubwa fahamu kuwa hata tendo la ndoa mara nyingi inakuwa ni shida kulifanikisha,kwani wataalamu wa afya wanasema tendo la ndoa kwa ustadi mkubwa huwa linaratibiwa sana na mzunguko mzuri wa damu ndani ya mwili wa mtu na kama wewe una tumbo kubwa limelalia sehemu za uzazi linakwenda kulalia mishipa midogo ya uzazi na ndio maana vilio haviishi majumbani. Sasa usipopunguza uzito wako uko kwenye hatari kubwa ya damu kushindwa kusafiri kwenye misuli na ukweli ni kwamba ili misuli itune ni lazima kuwe kuna usambazwaji mzuri wa damu katika eneo hilo.
Hivyo ndio maana mwanaume anaweza akawa anakula vizuri na uwezo wa mbegu kuzalishwa ukawa uko juu kabisa,lakini kutokana na uzito alioubeba ambao mara nyingi ndio unakuwa ni chanzo kikuu cha kudhoofisha mfumo wa mzunguko wa amu mwilini mwa mtu basi bado tendo la ndoa kwa mwanaume huyu likawa ni tatizo kwake.

Ningependa kusikia kutoka kwako ndugu msomaji ebu niambie ni sababu ipi kubwa kati ya hizi unayo ambayo inakuweka kwenye hatari kubwa na umepanga kufanya nini juu ya changamoto hiyo ?
 

Attachments

  • 43011308_538560129923512_4963008725422964736_n.jpg
    43011308_538560129923512_4963008725422964736_n.jpg
    24.5 KB · Views: 58
Back
Top Bottom