Sababu nne za CHADEMA kushinda Igunga

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111

Na mwandishi wetu.

WASOMAJI wapendwa, ni bahati mbaya sana kwamba wiki moja tu baada ya kuahidi kujitahidi kuhakikisha kalamu inakuwa hewani kila wiki, nikajikuta napata safari ya ghafla kuja huku Igunga kushuhudia mnyukano wa miamba ya siasa za Tanzania katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga.

Bahati mbaya huku mtandao unashika kwa shida na tovuti inapatikana kwa shida pia kwa hiyo wiki ya kwanza nikajikuta nimeshindwa kutuma makala.

Mpaka sasa niko Igunga na huenda nikakaa huku mpaka matokeo yatoke. Kwa sababu hiyo kila wiki nitajitahidi kuwadokeza yanayoendelea.

Wasomaji mtakumbuka huko nyuma kila uchaguzi vyama vya upinzani vilikuwa vikilalamika kwamba vinaonewa na CCM, chama tawala, kwa kuvihujumu ikitumia nguvu ya dola kwa maana ya jeshi la polisi, usalama wa taifa, maofisa wa tume ya uchaguzi, viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, mabalozi wao wa nyumba kumi kumi na hata wakati mwingine wakizidiwa sana walitumia vijana wahuni wa kukodi wavuta bangi wanaofundishwa kwanza mazoezi ya kupiga na kushambulia watu.

Tuliwaona kule Busanda ambako walipewa majina ya kishari kama ‘ninja’. Ninachotaka kukizungumza hapa ni majibu yaliyokuwa yakitolewa na CCM kwa tuhuma hizo za upinzani. Wapinzani wakilalamikia hujuma za CCM walikuwa wakiambiwa: “Kawaida yao wapinzani kulalamika tu kwa kila kitu.”

Uchaguzi wa Igunga ukafika, CHADEMA inaelekea imechoka kulalamika kila siku. Na kuna historia kwamba malalamiko ya upinzani wakati wa uchaguzi huwa hayashughulikiwi na jeshi la polisi, tume ya uchaguzi wala TAKUKURU. Kuna mbinu ya kuwapuuza mpaka uchaguzi uishe; kwamba kila lalamiko la chama cha upinzani linawekwa kwenye faili-linawekwa pembeni halifuatiliwi.

Baada ya uchaguzi hakuna mwenye kufuatilia tena maana wapinzani watakuwa wakiuguza madonda ya kushindwa uchaguzi, kwa kuporwa pengine.

Mwisho wa siku madai ya CCM yanakuwa ya kweli kwamba wapinzani kazi yao kulalamika tu! Maana ni kweli kwamba baada ya uchaguzi hakuna wa kufuatilia. Kama madai yao yana ukweli mbona hawafuatilii haki yao hata baada ya uchaguzi? Hitimisho la kweli kwa hoja ya uwongo!

Katika uchaguzi wa Igunga CHADEMA ina sababu kubwa na za msingi za kushinda. Niligusia moja tu katika makala yangu moja hapo nyuma lakini leo nitazitaja zote: Ya kwanza ni kwamba wamepania kuvunja rekodi ya CCM ya miaka takriban 16.

Katika muda huo wa miaka 16 haijapata kutokea uchaguzi mdogo kwenye jimbo ambalo aliyeondoka ni mwana CCM halafu chama cha upinzani kikashinda. Mara ya mwisho hilo lilitokea mwaka 1996 pale Augustine Lyatonga Mrema aliposhinda uchaguzi mdogo wa Temeke kupitia NCCR (jimbo lililoachwa wazi baada ya kutenguliwa matokeo yaliyompa ushindi Kihiyo wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995; uchaguzi mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi na baadaye mwaka huohuo John Momose Cheyo akashinda uchaguzi mdogo wa jimbo la Magu kupitia UDP baada ya kufariki kwa Lupondije wa CCM.

Pili CHADEMA wanataka kuandika historia kwamba si lazima kiongozi mkuu wa chama ndiye ashinde uchaguzi mdogo kwenye jimbo lililokuwa linashikiliwa na CCM. Tukumbuke kwamba Mrema na Cheyo wote walikuwa wenyeviti wa taifa wa vyama vyao wakati wanashinda hizo chaguzi ndogo.

Tatu, CHADEMA inataka kuonyesha kwamba inaweza kushinda kila uchaguzi mdogo wa bara baada ya uchaguzi mkuu wa 2005.
Katika hili naomba niseme wazi kwamba huu ni msimamo wao binafsi kama chama kwamba tokea uchaguzi mkuu wa 2005 wamekuwa wakishinda uchaguzi mdogo Tanzania Bara katika kila jimbo isipokuwa Tunduru.
Kote, kuanzia Kiteto mpaka Tarime, Busanda mpaka Biharamulo, walishinda isipokuwa walidhulumiwa ushindi wao Kiteto, Busanda na Biharamulo.

Nne, CHADEMA inataka kuthibitisha kwamba sasa iko tayari kutwaa dola; kwamba katika jimbo ambalo lilikuwa ni ngome ya CCM, CHADEMA ikiwa haijawakilishwa hata kwa kukosa mgombea wa ubunge katika chaguzi zote tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, lakini leo wanaingia na kushinda ubunge. Na hili hata CCM wanalijua.

Katika makala yangu ya wiki chache zilizopita, nilieleza kwamba kuna taarifa za ‘kiintelijensia’ zinazodai kwamba CCM imefanya vikao vya ndani ikakiri kwamba “kama ni uchaguzi kwa maana ya uchaguzi wa kupiga kampeni za kistaarabu na hatimaye kwa uhuru na haki wananchi wakapiga kura, tayari CHADEMA imeshinda. Lakini hilo likitokea maana yake chama chetu kitakuwa kimehalalisha hatua ya kwanza kuelekea kuanguka na kupoteza dola nzima mwaka 2015. Kwa sababu hiyo ni lazima tutumie mbinu mbadala kuhakikisha tunatwaa ushindi hata kwa nguvu,” mwisho wa kunukuu.
Sababu ya nne ni kwamba kumbe hata CCM inajua kwamba CHADEMA ikitwaa ubunge wa Igunga imeanza hatua moja ya kutwaa dola. Na kama mjuavyo safari moja huanzisha nyingine! Hivyo ni dhahiri kwamba safari ya Igunga itaanzisha safari ya kata nne za udiwani Arusha; itaanzisha safari ya jimbo lingine la uchaguzi mdogo ambalo sijalijua na pengine na lingine na lingine.

Na hatimaye safari hizo zote zitaanzisha safari ya 2015 kushuhudia kwenye Viwanja vya Jangwani (sipendekezi uwanja wa taifa maana utaangushwa na umati wa watu watakaojitokeza kushuhudia Rais wa tano kupitia CHADEMA akiapishwa). Katika viwanja vya Jangwani, sote tutamshuhudia Rais Kikwete akikabidhi madaraka kwa Rais Dk. Slaa.
Walikuwa na sababu za kutosha kujipinga na uwezo wa kujipanga pia walikuwa nao. Nilimuuliza kiongozi mmoja wa CHADEMA hapa Igunga baada ya kuona CCM inaanza kuyumbayumnba na alisema kuhusu ushindi wao hapa Igunga: “Nia ya kuwashinda tunayo, sababu ya kuwashinda tunayo na uwezo wa kuwashinda tunao; tutawashinda Igunga!”
Naam, hivi sasa Watanzania wamesikia CCM ikilalamika kwenye vyombo vya habari na kwa tume ya uchaguzi. Ndani ya wiki moja kwa mfano, CCM imepeleka malalamiko mawili kwenye tume ya maadili ya jimbo kwanza ikilalamika kwamba CHADEMA imewakashfu viongozi wa chama na serikali na kwamba CHADEMA wamemmwagia tindikali kijana wa CCM.
Ndani ya wiki hiyo hiyo, Nape kazungumza na vyombo vya habari akidai CHADEMA imepeleka magaidi Igunga na kutangaza jino kwa jino.

Januari Makamba naye kazungumza huku akilialia tu bila hata kueleweka anataka Watanzania wamfanyeje, wamwonee huruma na kuipa kura CCM ama wawafukuze CHADEMA kwenye uchaguzi wa Igunga. Lakini ndani ya wiki hiyohiyo yafuatayo yametokea: Mosi Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupilia mbali rufaa ya CUF (kimsingi rufaa ya CCM nyuma ya CUF) ya kumwekea pingamizi mgombea ubunge wa CHADEMA.

Juzi Jumatatu, Kamati ya Maadili jimbo la Igunga imetupilia mbali malalamiko ya CCM dhidi ya CHADEMA kwamba ndiyo waliommwagia kijana wa CCM tindikali na kamati ya maadili imedai uthibitisho ambao CCM imeshindwa kuutoa. Halafu tume hiyo ikatupilia mbali madai ya CCM kwamba CHADEMA imewakashfu viongozi wa chama na serikali.
Katika hilo CHADEMA ilitaka kujua chama hicho ni chama gani ambacho viongozi wake wamekashfiwa na serikali hiyo ni serikali ipi ni ya Mapinduzi ya Zanzibar, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ama ni serikali ya mtaa wa Majengo, mjini Igunga, ama hata ni Serikali ya Jamhuri ya Kenya? CCM wakakosa majibu. Lakini kamati ya maadili ikaenda mbali pale ilipoamuru kwamba Nape Nnauye ajieleze kwa kufafanua kwamba aliposema sasa ni jino kwa jino na kwamba CCM inatangaza vita Igunga alimaanisha nini? Kazi kwake!

Lakini mchana uleule wa juzi, mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora nayo ikatoa uamuzi wa kuwaachia kwa dhamana viongozi wa CHADEMA waliodaiwa kumsulubu mkuu wa wilaya. Kesi yao itaanza kusikilizwa Oktoba, 10 baada ya uchaguzi wa Igunga Oktoba 2. Tunasubiri tuone kama na wao hawatapuuzia kufuatilia kesi iliyotokana na uchaguzi baada ya uchaguzi.
Wakifanya hivyo wamethibitisha kauli yangu kwamba sasa wao ndio wapinzani. Kazi yao kulalamika tu. Hayo yote yakatiwa viungo na uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi wa Arusha kutupilia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na waliokuwa madiwani watano kupitia CHADEMA. Hawa ni madiwani waliopigiwa upatu sana na CCM kiasi cha kufikia mahali wakataka waendelee kuwa madiwani kwa nguvu mpaka hapo mahakama itakapoamua kesi. Sasa mahakama imeamua. Tunasubiri msimamo wa Mkuchika.

Ni nini lakini kilitokea?


Kutokana na sababu nilizozitaja hapo juu, CHADEMA iliamua kujipanga kama jeshi la myamvuli. Ikaingia vitani ikiwa imedhamiria kuibana CCM kila kona. Iliweka mpango wa kufika Igunga mara tu baada ya kusikia habari kwamba Rostam Aziz alikuwa amejivua gamba; likatoka na ngozi na hatimaye kuvuja damu ya ubunge mpaka ikaisha.
Walipeleka timu ambayo imeishi ndani ya jimbo la Igunga siku 47 kabla ya kampeni za ubunge kuanza. Wakiwa Igunga wameweza kuweka mtandao wa chama ndani ya kata zote 26 na vijiji vyote 98.

Kinachotambulishwa kama jeshi la magaidi lililoingizwa na CHADEMA kutoka nje ya Igunga ni uwongo mtupu! Nimefuatilia jimbo zima nikagundua kwamba baada ya chama kukubalika mpaka ngazi ya vijiji, CHADEMA waliwahamasisha wanavijiji wote kujiundia kamati zao za ulinzi na usalama. Kwa hiyo katika kila kijiji na kitongoji, wananchi wa eneo hilo ndio walinzi na wana usalama wa CHADEMA. Hawaruhusu upuuzi wowote kwenye eneo lao.

Ni bahati mbaya kwamba CCM ilichukua vijana watanowatano kutoka kila kijiji ikawapeleka kwenye makambi ya kuwafundisha ugaidi ili waje wawashambulie wana CHADEMA na kung’oa mabango ya mgombea wao na bendera za chama hicho. Pia waliandaliwa kutumika kwa kushirikiana na vijana waliotoka nje ya jimbo hili kuwatisha wananchi wote wanaoiunga mkono CHADEMA na kuwalisha mkong’oto wale wote wanaokataa amri zao.

Lakini kwa kuwa CHADEMA inatumia wananchi wenyewe wa eneo husika kama walinzi, ina maana wanawafahamu vijana hao wote wanaotumiwa na CCM kigaidi. Vijana hao wanakabiliwa na nguvu ya umma ya kijiji mpaka wanashindwa kufanya lolote. Lakini pia inakuwa rahisi kuwakamata watu wote wanaojihusisha na kuihujumu CHADEMA. Mkuu wa wilaya aliyeamua kuisaidia CCM alinaswa vivyo hivyo na wananchi ambao walimripoti kwa viongozi wa chama. Mabalozi waliokuwa wanaandikisha kadi za kupiga kura walikamatwa kwa intelijensia ya nguvu ya umma kijijini.
Kwa ujumla CCM wamebanwa kila kona. CHADEMA wamekaba mpaka penalti na sasa CCM imekubali kuwa chama cha upinzani kwa kulalamika kila siku.

Kwa herini CCM!
 
.......Tunashukuru kwa thread yenye hamasa,mshiko na yenye uhalisia kabisa...nadhani utaendelea kutupatia taarifa muhimu toka Igunga..
 
oya mnao quote tandiko lote mnakera tunachoka ku scroll dowm. Kama vp weka post yako tu inatosha.
 
I like to hear the good news like this!!!!!, I know ccm soon you will be running out of Members and that is going to happen soon , I first though it could take a long time for the entire country to accept OPPOSITION party, I realize that was wrong thought. It is going to happen soon.

Tanzania needs to be rebuild, and that will only happen if we could dare to remove ccm from being a political power in this country !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vancomycin! mkuu kwanza hongera kwa uchambuzi yakinifu! yaani unashusha nondo kama Mzee wetu Mwanakijiji.
Anywayz pamoja na hayo yote uliyoyasema,lakini mimi ninaswali moja na nitashukuru kama utalijibu kwa faida yangu
na wanaJF wote wa jukwaa la siasa! Nalo ni -:
Kuna habari zimezagaa kuwa sasahivi hapo Igunga ccm wamemwaga sumu ya udini na ugaidi dhidi ya CDM.
Udini ni kubadilisha ule mtandio wa yule mama uliyomdondoka kwa bahati mbaya na kuwa Hijabu aliyovuliwa
kichwani makusudi na wanachama wa CDM. Na pia ccm wanamwaga sumu ya ugaidi dhidi ya CDM kwa kuwa ilimchukuwa
yule mama DC na kumweka chini ya ulinzi kwa mahojiano ya kama dk 10 na pia baada ya CDM kusema this time itaimalisha
ulinzi wake kwa kutumia wanachama wao ili wasionewe tena na ccm....matokeo yake ccm wameibuka na neno 'Ugaidi'
So kwa haya mambo 2 yanayo ubiliwa na ccm kila kukicha, Je wewe unaona CDM inaweza shinda hapo Igunga? unavyo
ona wananchi wa Igunga wanamuamko kiasi kwamba hawezi kufall kwenye propaganda za udini na ugaidi zinazomwagwa na ccm?
Je muamko wao unaunaje? Na hizi habari za kusema huyo mama( DC) leo alikuwa anawaambia waislaam wa Igunga waandamane
kwa kuwa alivuliwa hijabu na CDM, Je ni za kweli? na kama ni za kweli je CDM wategemee kuvuna nini? Ahsante
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom