Sababu moja wapo kwa nini niliacha kuangalia filamu za kibongo

Wabongo bana! Kwa kupenda kuponda vitu vya nyumbani! Hata hao mnaowaangalia na kuwapenda walianza mdogo mdogo kama bongomovie!
 
Nitaangalia muvi ya bishanga mzee kamba ulaya na yule mama hizi za wengine ni ushuuuziii
 
Bongo movie action jambazi anavua viatu kabla hajaingia ndani kufanya uhalifu akihofia kuchafua nyumba ya mtu
 
Mimi baadhi nawakubali ila zingine fix nyingi jambazi anavua viatu kuingia ndani au unakuta mwanamke katoka usingizini ana make up ya nguvu yaani hawaendeni na uhalisia....yuko kijijini kavaa mlegezo na jinsi kali. ..
 
Muhogo mchungu,Gabo na JB na wa vichekesho wote naangalia kama Maringo saba na timu yake wengjne hawa hamna kitj
 
Kama umezoea kuangalia movies za mbele,ukija ukacheck na ya kibongo dah ndo utagundua kuna utofauti mkubwa sana.

Na sio kwamba hatuangalii za bongo eti kuonekana 'classic' kama ambavyo akili yako inakutuma,ila kwa kweli hazivutii yani kuangalia....

Yani hata hazishawishi at all,uhalisia zero kabisa.

Siwezi kujilazimisha kuziangalia eti kisa tu 'kussuport' kazi za bongo....

Tena ingekua vizuri tugome kabisa kuziangaliaili wajifunze na watoe vitu vikali.
 
Niliacha kuangalia pale Wema Sepetu aliposema yeye bado bikra.
 
Huwa naenjoy vitu kama "siri ya Mtungi" au "siri ya Familia"...Kuna Ile nyingine huwa naona yupo Yusuf Mlela na wakenya inaitwa Kashfa. Dah ila movie zetu zingine bwana hata umaliziaji tu ni shida. Yaani unaweza kuta umekaa mbele ya TV unasubiri unadhani labda tangazo limeingilia... Unasubiiiiri...inaanza nyingine au kipindi kingine...unabaki |-O.
Alafu yale mambo ya "watch out for Party 2"...tutaacha lini?
 
hakuna cha kujifanya mzalendo wala nini. wabongo tuko nyuma sanaaa.movies hazina uhalisia, muvi ikianza tu unajua mwisho ukoje. madirector ni hewa kabisa hawajui ku direct waigizaji.bongo movies time wastagr ni kubwa mno.mtu ataonyeshwa tangu anaoga mpaka anavaa anakunywa chai anawasha gari anafunguliwa geti anarudi rivasi anatoka nje geti linafungwa yaaani daaaah utumbo mtupu. angalia muvi za mbele wau ni mathinker bana.stori inatungwa inatungika mpaka unaikubali.
director na script writers wa movies kama prison break au the last ship utazdhani sio binadamu manake wana akili mpaka wamepitiliza.very creative.
sawa teknolojia yetu iko chini ndio nakubali.sasa hata kutunga story na kudirect vinatushinda?
angalia bongo movie ikiisha then wakati maandishi yanapanda utakuta director ni fulani,then script writer ni yeye yeye,then main character ni yeye yeye,then location manager yeye yeye yaani daaah. sasa ubora wa muvi zetu utapanda lini kwa staili hii?
 
Back
Top Bottom