Sababu mlipuko wa bei, Covid-19 na kupanda kwa gharama za Mafuta kwenye Soko la Dunia, hizi sababu haziingii kotekote!!

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Kwa mujibu wa Rais Samia, ongezeko la gharama za uendeshwaji wa maisha limetokana na mlipuko wa Covid-19 na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la Dunia, hatukatai ila sababu hizi hazina mashiko katika maisha yetu watanzania!

Imagine Gas kupanda, sababu Covid-19 na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia

Sukali , maharage, sabuni nk sababu Covid-19 na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia

Miamala nayo sababu Covid-19 na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia

Kila kitu the same reasons Covid-19 na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia

Nchi itapigwa mnada by Job Ndugai
 
Hazina mashiko kabisa, Tuanze na mafuta kwanza, tozo za serikali peke yake kwa lita ni TZS 952, karibu nusu ya bei ya lita. Ubunifu umeisha hadi serikali ikitaka hela ni kuongeza tozo tu kwenye mafuta? Naskia Zambia hapo lita ya mafuta ni TZS 1700, na yanapita bandari ya daslam hapa...
 
Kuja kufika December 2022,mama atakuwa kachoka sana tena sana.Saiv anachofanya ni bora liende,hatoi critical analysis ya matatizo wala haoneshi solution yeyote.Kwa miezi nane kachoka hiv vipi safar ya miaka ilobaki?
 
Back
Top Bottom