Sababu kwanini hutakiwi kujichanganya na watu 'uliowapiga gap' kubwa kimaisha

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,106
27,087
Mwenyezi Mungu amekujaalia Neema. Unatembea na neema ya Mungu. Umesoma soma kidogo. Una kazi yako, shughuli au biashara inayo kuingizia kipato. Una ndoto za kutoboa kimaisha. Una dream big. Unaamini siku moja utakuwa juu kimaisha.

Hutakiwi kujichanganya kiasi cha kuzoeana kupita kiasi na watu ambao maisha yao yapo chini sana kupita maisha yako more especially wale wasiojishughulisha kabisa. Wale waliokwisha kubali yaishe. Wameshakubali kwa vitendo kwamba wao hawawezi kufanikiwa katika maisha yao.

NI hatari sana ku-socialize na watu wa aina hii. Kwanini?

Sababu zipo nyingi but leo for the purpose of this thread nitakupa sababu moja ambayo ndio imenifanya niandike uzi huu.

Ukijichanganya na kuzoeana sana na watu uliowapita kimaisha kwa gap kubwa, mwisho wa siku wataanza kukuona wewe ni sawa na wao kimaisha wakati sio kweli. Wataanza kuona kua wewe haustahili kuwa katika level hiyo ya kimaisha. They will start to size you up.

Siku ukitoboa zaidi they will hate that fact kwa sababu wanaona wewe haustahili kuwa na maisha hayo wala kutoboa zaidi.

They will need you either to at least stuck where you are in the life or go down to their level.

They will need and prefer you as their partner in sufferance.

Hujawahi kujiuliza hili swali? Kwa watu wa mtaani kwako it's okay Kwa Mo Dewji kununua nyumba ya bilioni kumi but wewe Kijana Engineer ambae umegraduate miaka kumi au kumi na tano iliyopita kununua nyumba ya milioni Mia tano is not okay. They will hate that.

Sababu ni ndogo sana chief. Umezoeana nao kupita kiasi. They think you is them.

But hapo hapo mtaani kwenu kuna mzee mmoja mtu mzima tajiri. Yeye hajichanganyi nao kabisa na anafanya vitu vikubwa sana tu mara kumi ya unavyovifanya wewe but they don't have any problem with it.

Sababu ni moja tu. Hajichanganyi nao. Hawamuoni kama mwenzao.

Imenitokea Mimi personally. For about 4 or 5 yrs nilikuwa najichanganya sana na hohehahe wa kitaani kwetu. Nilikuwa nikitoka mishemishe zangu hapa mjini, nje ya nchi au mkoa, nikirudi home basi mara nyingi nilikuwa na-hang out na homeboyz wa kitaa kwenye bar za kitaa.

Kuhang out na hawa jamaa kuliwafanya wanishushe to their levels of grace. Kuna vitu ambavyo nilikuwa navifanya ambavyo to the level of my grace ni vitu vya kawaida sana but nikawa surprised jamaa wakawa kama wanabisha vile.

Mwanzoni nilikuwa naendesha gari ya mawazo and it was just okay to them kwasababu ni aina ya gari ambayo watu wengi walikuwa wanaweza kuimiliki.

Baadae nikanunua gari nyingine kali ya bei za level za watu kama Kiduku Lilo, hee nikaanza kuona watu wananinunia.

Yani hata kubishana na watu nikawa nashindwa tena kwa sababu nikibisha ntaonekana ninawadharau kwakuwa naendesha gari kali.

Gari wakalizoea. Tatizo la pili ni pale nilipojenga nyumba yangu.

Nyumba niliyojenga ni zile ambazo watoto wa mjini wanaziita "Stop Nonsense" au Mwana ukome. Sijisifu but nimejenga nyumba kali.

Mimi kwa kiwango cha neema za Mungu katika maisha yangu ninaona ni nyumba ya kawaida but jamaa wa kitaa wanaona, nope haiwezekani.

Taratibu watu wanaanza kunipunguza. Hawataki kukubaliana na ukweli. They don't even talk to me anymore cause they think they don't know anything that me and them can talk about. The me that they put in their expectations is far much different from the real me.

Mimi ndo Kwanza am starting to count my blessings. The Lord Blessings have left me lyrically inclined. And I know watakuwa wananiloga sana; ningekuwa fala fala sasa hivi my life would be a reflection of their bad intentions.


Moral of the story:
Kama Mungu amekupa neema katika maisha usijichanganye kabisa na watu ambao umewapiga gap kubwa kimaisha. They best thing u can do to them is help them but not to hang out with them. Jichanganye nao kwenye Mambo muhimu kama msiba etc but sio Ku hang out now. Usizoeane nao kabisa.

Kuwa kama wafanyavyo matajiri na watu wenye uwezo mkubwa kimaisha duniani. Matajiri wengi huwa hawajichanganyi na masikini kabisaaa isipokuwa kwenye ishu muhimu kama misiba n.k.

Be around people who reflect who you are and what u want to be. These poor people are full of negative energy. If you hang out with them they will end up sucking ur positive energy.

The most best way to help poor people is not to be poor like them.

Usiogope kuambiwa unaringa. Usiogope kuambiwa umebadilika. Kubadilika ni moja kati ya sifa za pesa.
Whoever says money have not changed them, have not got enough of it.

Psalm 18:18-21 Bwana alikuwa tegemeo langu, akanitoa akanipeleka PANAPO NAFASI akaniponya Kwa kuwa alipendezwa na Mimi.
 
You can’t fly with the eagles if you continue to scratch with the turkeys. Surround yourself with positive, goal-oriented people who are ambitious and excited about accomplishing wonderful things with their lives.

Epuka wale jamii ya “usisahau na ya kutolea” au “ bata wapi weekend hii mchizi wangu”?
 
niliwahi kujiuliza kwanini tajiri mkubwa nchini mzee said salim bakhresa licha ya kwamba ni "mswahili", ila kamwe huwezi kumuona kwenye vibaraza na vijiwe vya kahawa vya kariakoo akipiga soga. sasa nimepata jibu kwanini anaishi masaki badala ya kariakoo kwa waswahili. asante sana mleta mada.

NB: nadhani sote tunajua social behaviour za wazee wangu pwani hususani kariakoo.
 
Back
Top Bottom