Sababu kwanini bei ya mafuta ni nafuu DRC na Zanzibar lakini Tanzania Bara ni ghali

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
Sababu ya kwanza: DRC kuna shughuli nyingi sana za uchimbaji madini kama shaba na madini mengine. Makampuni makubwa ya kibepari yamefunga mitambo yao ya kupasuwa miamba huko.

Shaba na madini mengine yanayochimbwa huko yanahitaji kusafirishwa hivyo basi wamiliki wa malori wanapeleka malori yao huku kwa maelfu. Maana yake nini malori yakiwa mengi kama hivyo, mahitaji ya mafuta yanakuwa makubwa.

Kwa wafanyabiashara wa mafuta huku DRC ndiyo kwenye soko, wanapeleka shehena kubwa huko kwa hiyo kunakuwa na ushindani wa bei kuvutia wateja kwa hiyo kwa vyovyote vile bei lazima ishuke.

Tanzania Bara hakuna soko la hivyo. Vifaa vinavyohitaji mafuta ni vichache au havili sana. Fikiria mfanyabiashara wa mafuta analeta shehena kwa ajili ya kuhudumia IST na bodaboda.

Haileti maana, shehena itakaa sana ghalani na hiyo ina maanisha ni hasara kwa mfanyabiashara. Kwa hiyo itoshe tukusema kuwa soko la mafuta hapa Tanzania Bara ni dogo na kwa hiyo wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wanaona haina maana kuweka shehena zao hapa.

Zanzibar.
Hawa siwaongelei sana ila niseme tu kuwa tusisahau hawa wenzetu wana mafungamano na Oman na wanayo bandari na Bi Royal Tour ni wa kwao kwa hiyo si ajabu kuwa kwao bei iko chini.

Pamoja na yote, mamlaka ziangalie jinsi ya kudhibiti hizi bei zishuke.

#NguvuMoja
 
Wewe umeongea kulingana na ufahamu wako na sio mfumo wa ugavi wa mafuta unavyokuwa.

Kwanza unapaswa kuelewa kwamba mahitaji ya mafuta Tanzania bara ni mkubwa kuliko hiyo DRC.

Ebu fikiria ni malori mangapi yanayoanzia na kumalizia safari za usafirishaji bidhaa katika bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara kila siku?.

Mbali na kwenda DRC,tunasafirisha bidhaa kwenda nchi za Malawi,Zambia,Rwanda na Burundi.
Pamoja na Uganda kwa kiasi fulani kupitishia ziwa victoria kwa meli za Mizigo MV Kabarega na MV Umoja.
Baada ya mizigo kusafirishwa kwa treni kutoka bandarini Dar es salaam hadi Mwanza.

Kuna mabasi mangapi yanayoanzia na kumalizia safari za usafirishaji abiria kila siku jijini Dar es salaam na kwenda mikoani?

Je DRC inao mtandao wa Barabara kulinganisha na Tanzania bara?

Je DRC inavyo viwanda vingi vya uzalishaji kuliko Tanzania bara?

Je unaujua mzunguko wa mabasi makubwa,Dalaladala na Bajaj hadi Bodaboda nchini na unatumia mafuta kiasi gani kwa siku?

Ingawa DRC inao utitiri wa madini ardhini kwao,lakini bado haijaipiku Tanzania bara kwa ukubwa wa migodi ya kisasa yenye kutumia mitambo mikubwa na yenye mahitaji makubwa ya mafuta kila siku.

Pia ukumbuke DRC haina bandari na hivyo asilimia kubwa ya shehena yao ya mafuta inapitia Tanzania bara na kenya,hivyo kutufanya malori yetu mengi yatumie kiasi kikubwa cha mafuta ili kuisafirisha shehena ya wakongomani hadi kwao.
Na hivyo kuongeza idadi ya matumizi kuliko DRC?

Rudi kafanye utafiti wako safari ingine uje na utafiti wa

"Tanzania na DRC ni nchi gani inao walaji wengi wa Ugali?"

Labda tutakuelewa huko!
 
Ila duh Africa alieturoga katupata sana, yaani maadini yote tulionayo hayo ila bado sisi ni maskini
 
Sababu zako hazina kichwa wala miguu
Ngoja mdau akupandishe mitozo
Iliyoko kwenye litany 1
Kalunya

Ova
 
Wewe umeongea kulingana na ufahamu wako na sio mfumo wa ugavi wa mafuta unavyokuwa.

Kwanza unapaswa kuelewa kwamba mahitaji ya mafuta Tanzania bara ni mkubwa kuliko hiyo DRC...
Sidhani Kama hizi sababu ni za kweli tatizo kubwa ni mlundikano wa Kodi na tozo kwenye mafuta no more no less
 
Hakika... Ila isiwe sababu ya huku Bara kuburuzwa namna hii...
 
Drc wanatumia bandari yetu.

Hivyo hizo.lori hazikwepi kuweka mafuta hapa.

Tunahudumia Zambia, Malawi, Rwanda na Burundi hivyo kama kushuka kwa bei ya mafuta ni kutokana na demand basi Tanzania bei ndio ingepaswa kuwa chini zaidi.
 
Wangekuwa na kodi kedekede kama sisi bei ingekuwa kubwa tu.

Tanzania mafuta yana kodi na tozo zaidi ya 20.
 
Back
Top Bottom