Hili halina ubishi, Watanzania wengi wanapinga ongezeko la tozo mbalimbali kuanzia kwenye mafuta mpaka kwenye miamala ya simu. Hii tabia ya kupinga haijaja ghafla, bali ni matokeo ya muda mrefu.
Sababu kubwa zinazowafanya Watanzania kupinga tozo hizi, ni kukosekana kwa uwazi (Transparency) na uwajibikaji (Accountability) katika nchi kwa muda mrefu. Haya masuala yanaonekana ni madogo ila ndiyo yametufikisha hapa.
Kwa mfano, miaka na miaka, wananchi wamekuwa hawawekwi wazi kuhusu mambo yanayohusu nchi kama vile; ukopaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nchi. Mnamkumbuka yule aliyekuwa anasema, "leo tunajenga kwa fedha za ndani", kesho anasema "tunakopa kwa faida".
Kuhusu accountability, kuna baadhi ya maeneo ndani ya nchi yana hali ngumu sana kimaisha, mfano, hakuna umeme, maji, barabara nk.
Kukosekana kwa mambo haya mawili (transparency and accountability) kumewaathiri sana Watanzania kisaikolojia, hivyo kutokubali kirahisi rahisi tozo zinazoongezeka, hata kama zina nia ya dhati ya kuliendeleza taifa.
Wananchi wangekuwa wepesi kuzikubali tozo, endapo tangu zamani wangekuwa wanaona matokeo chanya katika maisha yao. Leo, hii mwananchi haiamini serikali, kwa sababu anaona kama inamdanganya pale inaposema tunaongeza tozo ili kujenga barabara za vijijini. Hii ni kwa sababu, kwa miaka mingi mwananchi huyu amekuwa akiishi maisha magumu na anaiona serikali haina msaada kwake.
Wito wangu kwa viongozi, tuwe na uwazi na uwajibikaji kwa wananchi, ili huko mbeleni iwe rahisi kuwachangisha wananchi.
Leo, mnasema mmeongeza tozo ili kupata hela ya kujenga barabara za vijijini na mijini zenye ubora. Najua hilo limeishapita na Watanzania watazoea, ila sasa hizo barabara zijengwe jamani. Wananchi siyo wajinga kihivyo. Mwaka 2025 wananchi watawauliza kama hamtakuwa mmezijenga hizo barabara.
Watanzania tubadilike. Madhara ya kukosa uwazi na uwajibikaji wa serikali ni makubwa sana, kama inavyoonekana sasa. Hakuna kuaminiana tena Tanzania kati ya serikali na wananchi, kwa sababu huko nyuma wananchi waliisha-experience maumivu, rejea: escrow, richmond, epa, etc. Leo hii wananchi wanaona hizo tozo zinaenda kuwanufaisha viongozi wa serikali hata kama si kweli. Ni kwa sababu wananchi waliishapigwa sana huko nyuma.