Sababu kuu kwanini hakuna aliyewajibishwa hadi sasa kuhusu sakata la escrow

hata raisi akisuasua kuwajibishwa kwa watuhumiwa kuko palepale. maana waliotoa maamuzi ni wananchi kupitia uwakilishi wa wabunge wao.

Hata rasimu ilipitishwa na wabunge kwa vijembe na matusi kwa kisingizio cha kutumwa na wananchi japo sikuwahi kumwona mbunge wangu akisumuon wapiga kura wake ili wamwambie wanataka katiba ya aina gani,bunge limekuwa likipitisha mambo feki (binafsi) kwa kisingizio cha wananchi na hicho ndo kilichotokea katika escrow Pac wanatumwa na wafanyabiashara alafu wanakuja kuishinikiza serikali eti wananchi wamesema, mbona hawawataji mabwana zao wa kunyimwa vitalu?
 
Sababu ni moja tu nayo ni kuwa dhamira yake inamsuta kuwatoa wenzake kafara ili hali akijua aliwatumia kufanikisha deal.

Kwasababu hiyo,ndio maana kuna siku nilianzisha uzi hapa na kusema hao wote ni mabalozi watarajiwa nikiwa na maana kwamba hawezi kuwaacha hivi hivi.

Hamna kitu kibaya kwenye maisha kama kuishi na "guilty conscience" na hiki ndio kinamtesa JK.
 
Kama maono haya ndio yanatoka nyumba kuu na ndio mtizamo basi madhara ya analysis hiyo ni makubwa kwa Kiongozi mwenyewe, Serikali anayoingoza na Chama chake.Kushindwa kutekeleza maazimio ya Bunge ni pigo kubwa sana kwa vyote vitatu nilivyo sema hapo mwanzo na uenda ukawa ndio msiba wa CCM.

Wahisani wako macho wanasubiria kuona utekelezaji wa maazimio ya Bunge la 16/17.Na kwa kuwa Rais mwenyewe amekuwa ni mfano wa Kiongozi anae onyesha kujali sana ujenzi wa Demokrasia.Kwa hilo basi haimaanishi ni kiwango gani viongozi wamejiudhuru kwa kuwajibika basi JAPAN ingekuwa Nchi ya ajabu Duniani ambayo ndani ya Muda mfupi Waziri Mkuu amebomoa Baraza lake la Mawaziri mara kadha wa kadha.

Hakika 100% ikitokea hayo uyasemayo yakawa ndio utekelezaji basi tegemea Majukwaa Na vyombo vya habari kupaza Sauti kama ilivyokuwa Operation Tokomeza...na hatimae kumfanya Rais kutekeleza maagizo ya Umma kupitia vyombo vya habari na hasa hasa hizi Social Media.Kitu ambacho naamini JK hayuko tayari kukumbana na aibu ya kuwa hatembei kwenye maneno yake ambayo daima amekuwa akiyasisitiza na hata kuhutubia Bungeni na Kusisitiza kuwajibika kwa kila muhimili.Bunge limetimiza wajibu wake [Kama Mwakilishi wa Umma, uliomchagua Yeye Kama Rais] sasa ni wajibu wa Rais kutekeleza Maazimio.

Hii habari ya Kumwaga Mboga hiyo ni Tishia Nyau...au Tishia Toto, hakuna mwenye ubavu huo kwa hao waliotamkwa kuwa wanatakiwa kujihudhuru, HAKUNA anaeweza kujitutumua kusema lolote wanalojua ambalo hawakulisema wakati tuko kwenye shika ni mshike [Bunge La 16/17] leo aje kufunua mdomo wake eti anajua A na Z.......ALIKUWA WAPI HAKUYASEMA HAYO WAKATI ULE AJE ASEME HAYO LEO H WAKATI YUKO NDANI NA HAYUKO NJE YA ULAJI? SWALI LITAKUWA WHY NOW ?KWANINI SASA NA SI WAKATI ULE?

Unapokuwa kwenye issue hizo za mambo makubwa pale unapooona uendani na kile usichokiamini unapaswa kusema YOUR IN OR YOUR OUT.Kama uko IN dont speak Nonsense/This means dont shout kwa kuwa it was your choice to EAT THE CAKE.Na kama ukula keki kwanini ukusema kwenye kiti moto cha Bunge la 16/17 kuwa umeona A na Z na kuwa Unajua fulani na fulani ndio wametafuna keki yetu ya Taifa peke yao, wewe uvimbiwe leo ututapikie tukuchulie kuwa ni ugonjwa au HAAA WAPI SIE TUKWAMBIA NI URAFI HUO.

Na Kama umechagua au ulichagua kuwa Nje ya Ulaji basi your Ok to SHOUT tena kwa sauti kubwa kuwa KKUNA HARUFU YA UFISADI ILIPITA Kama ambavyo alivyopata kufanya yule Katibu Mmoja wa Wizara yeye alipiga Mwano/Mbija tena na Kiapo cha juu kuwa kuna mgao wa Millioni Mia Ulimtembelea na yeye aliamua Kuukata.

Kama umekula Keki unataka Kutapika uchafulie wengine HEWA ahaaa sheria asilia [Natural Justice ] haiko hivyo uwo utakuwa USALITI na Daima msaliti anastahiki zake!!Kinachotakiwa baada ya kuona Watanzania wanakutoa Jasho na hauna jinsi ya kupumua NENDA KWA PADRI WAKO/SHEIKH WAKO AU MCHUNGAJI WAKO AU KIONGOZI WAKO WA KIMILA KWAMWAMBIE KUWA UNAITAJI KUPUMUA KWA YALE ULIYONAYO MDOMONI.

Hii ya kusema watasema haina mashiko anaestahiki kuwawajibisha akiendelea kukaa na hili LITAVUNDA na yale mazuri alionayo yatafumua mengi yasiyostahiki....Manake kudeal na jambo la Umma latakiwa Busara na Busara ni kutekeleza maazimio.

Watanganyika tuwe na akili;tusome alama za nyakati katika Biblia.

Nani atashinda, Hasira ya Yesu mjibu dua?
{UFU 6:1~17
 
Pengine watanzania wanatega masikio kusikia "mawaziri wapya" na watendaji wengine kuwajibishwa lakini kwa utafiti wangu niliofanya nimegundua sababu za kuchelewa huko.

1. Sakata zima la escrow limeibuliwa na wapinzani sasa kama Rais atakubali kuwawajibisha ni kama amekubali kuongozwa "kuburuzwa" na wapinzani.

2. Uchaguzi huu wa serikali za mitaa. Pengine Rais anangoja upite kwanza huu..

3. IMPACT YA WATUHUMIWA kwa uchaguzi ujao.. pia hii inaleta delay hii maana watuhumiwa wengine wamesema "watamwaga mboga" pengine itahitajika "hekima" ya namna ya kuwapumzisha bila kuleta "madhara" kwenye chama mwakani.

4. Rais mwenyewe.. hapa Rais anajisikia "hatia" na pengine na "aibu" ya kubadili badili watu katika kipindi chake..

5. Muda uliobaki.. pia tuelewe umebaki muda mchache kupata viongozi wengine kupewa ofisi...

6. Nani atafaa kuchukua nafasi zao?

Kwa hiyo pengine tukasubiri hadi miguu izamie tumboni.

cc Pasco Mzeemwanakijiji MSALANI
Aibu kubadilibadili?atamzidi netanyau anaevunja serikali na kuitisha uchaguzi mkuu kila baada ya miaka 2?
 
Mleta mada Rais hawezi kumuhukumu mtu kwa kelele zenu na huyo Mengi wenu kwanza itv wamechukua eneo lawananchi pale mikocheni

ndugu.. big_in mi nimetoa sababu tu.. hayo ya itv na mengi yanakujaje hapa? hebu pumzisha akili kwanza kabla hujachangia.
 
Last edited by a moderator:
Sababu ni moja tu nayo ni kuwa dhamira yake inamsuta kuwatoa wenzake kafara ili hali akijua aliwatumia kufanikisha deal.

Kwasababu hiyo,ndio maana kuna siku nilianzisha uzi hapa na kusema hao wote ni mabalozi watarajiwa nikiwa na maana kwamba hawezi kuwaacha hivi hivi.

Hamna kitu kibaya kwenye maisha kama kuishi na "guilty conscience" na hiki ndio kinamtesa JK.

hilo nalo neno.
 
Pengine watanzania wanatega masikio kusikia "mawaziri wapya" na watendaji wengine kuwajibishwa lakini kwa utafiti wangu niliofanya nimegundua sababu za kuchelewa huko.

1. Sakata zima la escrow limeibuliwa na wapinzani sasa kama Rais atakubali kuwawajibisha ni kama amekubali kuongozwa "kuburuzwa" na wapinzani.

2. Uchaguzi huu wa serikali za mitaa. Pengine Rais anangoja upite kwanza huu..

3. IMPACT YA WATUHUMIWA kwa uchaguzi ujao.. pia hii inaleta delay hii maana watuhumiwa wengine wamesema "watamwaga mboga" pengine itahitajika "hekima" ya namna ya kuwapumzisha bila kuleta "madhara" kwenye chama mwakani.

4. Rais mwenyewe.. hapa Rais anajisikia "hatia" na pengine na "aibu" ya kubadili badili watu katika kipindi chake..

5. Muda uliobaki.. pia tuelewe umebaki muda mchache kupata viongozi wengine kupewa ofisi...

6. Nani atafaa kuchukua nafasi zao?

Kwa hiyo pengine tukasubiri hadi miguu izamie tumboni.

cc Pasco Mzeemwanakijiji MSALANI

Namba 6, mwambieni JK aniteue mimi nafasi ya Muhongo!
 
Back
Top Bottom