Sababu kuu kwa nini timu ya taifa ya Argentina haina mtu mweusi

Hivi hiyo nchi ndiyo inapita kwenye mdororo wa uchumi kiasi cha pesa yake kutumika chooni kama toilet paper
 
Hivi ukiandika "mtu mwenye asili ya bara la Afrika" unapungukiwa nini? Hili neno MTU MWEUSI limekaa kishenzi shenzi. Tafadhali sana!!!
 
Mtoa mada katoa mada nzuri tu lkn ina mtizamo wa ki historia zaidi kuliko alivyo husisha na mambo ya Soka, ila mengi ni ukweli kuhusu madhira aliyopitia Mtu Mweusi Argentina, ni taarifa zipo hizo ilikuwa ni mbinu ya ku cleanse rangi nyeusi
 
Ni swali ambalo wanamichezo mbalimbali huwa wanajiuliza karibu kila siku, kwa nini timu ya taifa ya Argentina 🇦🇷 haina mtu mweusi?.

Kwanza kabisa tofauti na imani ya wengi baada ya Afrika bara la Amerika Kusini ndiyo lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takribani milioni 120.

Pamoja na hayo yote kitu kimoja cha kushangaza nchi ya Argentina 🇦🇷 tofauti na nchi zengine za America kusini ndiyo nchi pekee yenye watu weusi wachache mno. Hili lilitokeaje?.

Watu weusi walikwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya Paraguay wakiwa na vifaa duni, vita hivyo vilidumu kwa miaka mitano (1865-70), Pia viongozi wa Argentina wa wakati huo walifanya hivyo pia kwenye vita dhidi ya Brazil iliyodumu kwa miaka mitatu.
Baada ya vita hivyo kuisha ambapo Argentina ilipigika vibya mno, Watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague”.
Watu weusi wengi sana walikufa huku serikali ikiwanyima kwa makusudi matibabu dhidi ya ugonjwa huo.
Maisha ya watu weusi yalikuwa magumu mno mwanzoni mwa miaka ya 1900 wakipitia matatizo kama ukosefu wa chakula cha kutosha,wakiishi katika mazingira hatarishi, wakibaguliwa katika huduma zote za jamii. Kutokana na ugumu huo wa maisha wengi wakaamua kuhamia katika nchi jirani za Brazil, Paraguay, Chile n.k.
Watu pekee waliokuwa angalau wanathaminiwa ni waafrika(weupe) hao hawakubaguliwa sana ila walilazimishwa waowane na wazungu na hivyo kuzaa watoto machotara. Pia hao machotara ilikuwa ni lazma aowane na mzungu na siyo mtu mweusi au chotara mwenzake. Hili lilikuwemo ndani ya sera za Argentina “White-Washing the country “ ikiwa ni tafsiri ya kutoka lugha ya kispaniola.
Hivyo hatimaye mpaka sasa watu weusi nchini Argentina ni chini ya laki mbili wakiwa takribani asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800.

Waasisi wa taifa la Argentina waliamini ili taifa lao liendelee lazma liwe na wazungu wengi na WaAfrika wawe chache tu kama sio kuondolewa kabisa.

Timu ya taifa la Argentina

View attachment 1499249

Baadhi ya watu weusi katika Karne ya 19 .

View attachment 1499254View attachment 1499255View attachment 1499256

Mbona unateseka hivyo! Messi anakuumiza nafsi ee,,,pole sana mwanawane.
 
Ni swali ambalo wanamichezo mbalimbali huwa wanajiuliza karibu kila siku, kwa nini timu ya taifa ya Argentina haina mtu mweusi?.

Kwanza kabisa tofauti na imani ya wengi baada ya Afrika bara la Amerika Kusini ndiyo lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takribani milioni 120.

Pamoja na hayo yote kitu kimoja cha kushangaza nchi ya Argentina tofauti na nchi zengine za America kusini ndiyo nchi pekee yenye watu weusi wachache mno. Hili lilitokeaje?.

Watu weusi walikwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya Paraguay wakiwa na vifaa duni, vita hivyo vilidumu kwa miaka mitano (1865-70), Pia viongozi wa Argentina wa wakati huo walifanya hivyo pia kwenye vita dhidi ya Brazil iliyodumu kwa miaka mitatu.
Baada ya vita hivyo kuisha ambapo Argentina ilipigika vibya mno, Watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague”.
Watu weusi wengi sana walikufa huku serikali ikiwanyima kwa makusudi matibabu dhidi ya ugonjwa huo.
Maisha ya watu weusi yalikuwa magumu mno mwanzoni mwa miaka ya 1900 wakipitia matatizo kama ukosefu wa chakula cha kutosha,wakiishi katika mazingira hatarishi, wakibaguliwa katika huduma zote za jamii. Kutokana na ugumu huo wa maisha wengi wakaamua kuhamia katika nchi jirani za Brazil, Paraguay, Chile n.k.
Watu pekee waliokuwa angalau wanathaminiwa ni waafrika(weupe) hao hawakubaguliwa sana ila walilazimishwa waowane na wazungu na hivyo kuzaa watoto machotara. Pia hao machotara ilikuwa ni lazma aowane na mzungu na siyo mtu mweusi au chotara mwenzake. Hili lilikuwemo ndani ya sera za Argentina “White-Washing the country “ ikiwa ni tafsiri ya kutoka lugha ya kispaniola.
Hivyo hatimaye mpaka sasa watu weusi nchini Argentina ni chini ya laki mbili wakiwa takribani asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800.

Waasisi wa taifa la Argentina waliamini ili taifa lao liendelee lazma liwe na wazungu wengi na WaAfrika wawe chache tu kama sio kuondolewa kabisa.

Timu ya taifa la Argentina

View attachment 1499249

Baadhi ya watu weusi katika Karne ya 19 .

View attachment 1499254View attachment 1499255View attachment 1499256
Hapa bongo wanajeshi wangapi wana asili ya Asia/wahindi,cheki Polisi,jwatz,magereza,TISS,
Walioteuliwa wote na Maghu,umeona hata mmoja mwenye asili ya Asia?
 
Si ndio hapo sasa, moja kati ya mada za kipumbavu ni hii chief. Mtu kabla ya kuongea/kupost anapaswa afikirie kwanza,
 
Ohoo.......
Ila hata Spain watu weusi ni nadra sn tofauti na mataifa mengi ya ulaya
Spain pia kuna ubaguzi ila sio wakiwango cha Argentina. Argentina ilinuwia kuondoa watu weusi wote katika ardhi yao.Ni vile tu haikuwezekana.
 
Hao watu laki 2 waje Tanzania tuendeshe maisha kwenye bara letu kuliko kuishi maisha ya kubaguliwa.
Ni heri kuishi maisha huru kwenye nchi masikini kuliko kuishi maisha ya kitumwa kwenye nchi tajiri
Kwani Tanzania kuna uhuru?
 
Spain pia kuna ubaguzi ila sio wakiwango cha Argentina. Argentina ilinuwia kuondoa watu weusi wote katika ardhi yao.Ni vile tu haikuwezekana.
Huwezi kupingana na Mungu..... Hitler tu alishindwa azma yake ya kuwaangamiza wayahudi
 
weusi wa Argentina wangeweka historia kama David trezeguet angeamua kufata asili ya babab yake na pia Pierre Aubamayeng angeamua kufata utaifa wa mama.
 
Back
Top Bottom