Sababu kuu kwa nini timu ya taifa ya Argentina haina mtu mweusi

Tz boy 4tino

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,598
1,815
Ni swali ambalo wanamichezo mbalimbali huwa wanajiuliza karibu kila siku, kwa nini timu ya taifa ya Argentina 🇦🇷 haina mtu mweusi?.

Kwanza kabisa tofauti na imani ya wengi baada ya Afrika bara la Amerika Kusini ndiyo lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takribani milioni 120.

Pamoja na hayo yote kitu kimoja cha kushangaza nchi ya Argentina 🇦🇷 tofauti na nchi zengine za America kusini ndiyo nchi pekee yenye watu weusi wachache mno. Hili lilitokeaje?.

Watu weusi walikwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya Paraguay wakiwa na vifaa duni, vita hivyo vilidumu kwa miaka mitano (1865-70), Pia viongozi wa Argentina wa wakati huo walifanya hivyo pia kwenye vita dhidi ya Brazil iliyodumu kwa miaka mitatu.

Baada ya vita hivyo kuisha ambapo Argentina ilipigika vibya mno, Watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague”.

Watu weusi wengi sana walikufa huku serikali ikiwanyima kwa makusudi matibabu dhidi ya ugonjwa huo.

Maisha ya watu weusi yalikuwa magumu mno mwanzoni mwa miaka ya 1900 wakipitia matatizo kama ukosefu wa chakula cha kutosha,wakiishi katika mazingira hatarishi, wakibaguliwa katika huduma zote za jamii. Kutokana na ugumu huo wa maisha wengi wakaamua kuhamia katika nchi jirani za Brazil, Paraguay, Chile n.k.

Watu pekee waliokuwa angalau wanathaminiwa ni waafrika(weupe) hao hawakubaguliwa sana ila walilazimishwa waowane na wazungu na hivyo kuzaa watoto machotara.

Pia hao machotara ilikuwa ni lazma aowane na mzungu na siyo mtu mweusi au chotara mwenzake. Hili lilikuwemo ndani ya sera za Argentina “White-Washing the country “ ikiwa ni tafsiri ya kutoka lugha ya kispaniola.

Hivyo hatimaye mpaka sasa watu weusi nchini Argentina ni chini ya laki mbili wakiwa takribani asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800.

Waasisi wa taifa la Argentina waliamini ili taifa lao liendelee lazma liwe na wazungu wengi na WaAfrika wawe chache tu kama sio kuondolewa kabisa.

Timu ya taifa la Argentina

2DBDEDB7-F662-49C3-ACEB-7A638AE7D4A5.jpeg


Baadhi ya watu weusi katika Karne ya 19 .

8C01A988-C07E-4F01-ACA3-F71521C72CB2.jpeg
1596D4FE-F382-4D0F-AAFD-1D2742D69E23.jpeg
EAB271E3-7E20-4B8D-B36C-8B4C893C63A1.jpeg
 
Hao watu laki 2 waje Tanzania tuendeshe maisha kwenye bara letu kuliko kuishi maisha ya kubaguliwa.
Ni heri kuishi maisha huru kwenye nchi masikini kuliko kuishi maisha ya kitumwa kwenye nchi tajiri
Ni kweli bora wangerudi tu.
 
Ngada Boy upo?
Hilo li timu la Bueno Aires silipendi kabisa, Bora mngeangamia na kuteketezwa na Coronavirus COVID-19

Huenda ukatangulia wewe kabla yao, yamewashinda yakwenu huko evryday mnakatana mapanga na kunyofoleana sehemu za siri kwa imani za kishirikina, eti maagizo kutoka kwa wataalamu, mkijisahau kidogo watapita na wake zenu 😁😁 Mleta mada amekosa cha kupost, ni chuki tu hizo.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom