Sababu Kuu 3 Zinazosababisha Watu Kughairisha Mambo

Dukebryshere

New Member
Nov 1, 2017
3
0
Takribani 80% huwa wanaacha kuendelea na mipango yao waliyojiwekea baada tu ya miezi mitatu ya kwanza mwaka unapoanza.Hii imewafanya watu wengi sana kujikuta wakiwa na hamasa na shauku kubwa mwaka unapoanza na kujikuta shauku yao ikiishia njiani.Unaweza kujikuta kuwa wewe ni mtu ambaye kila mwaka huwa unaanza mwaka kwa kishindo lakini baada ya muda kidogo tu unajikuta umeshakata tamaa na hauendelei tena na kufuatilia utekelezaji wa malengo yako.

Ili usiwe mmoja wa wale ambao kila wakati huwa wanaghairisha mambo na hujikuta wanaanza upya kila wakati ni lazima ujue sababu zinazowafanya watu wengi kuwa na tabia hiyo na wewe ujigundue huwa unaghairisha mambo kwa sababu zipi na ujue namna ya kujitoa kutoka katika tabia hiyo:

Sababu ya kwanza ni kusubiri kuwa na kitu kikubwa ili waanze kufanya kile ambacho wanataka kukifanya.Tatizo kubwa sana ambalo watu wengi sana limewakwamisha ni tabia ya kusubiri kuwa na vingi.SIku zote kumbuka kuwa hauwezi kuwa na vingi kama vile vichache ambavyo unavyo umeshindwa kuvitumia kwa ufanisi.Siku zote kama wewe utakuwa ni mtu wa kudharau kile kidogo ulichonacho basi hautaweza kupata kikubwa unachokitafuta.Kila wakati jiulize-Hivi katika hiki kidogo nilichonacho nitaweza kuanza kufanya nini?Siku zote jitahidi kuona namna unavyoweza kuanza na kile kidogo ulichonacho bila kucheleweshwa kwa kusubiri kile ambacho hauna.

Jaribu kujiuliza-Hivi mimi ni mmoja wa wale ambao wanachelewa kuanza kwa sababu naamini nilichonacho ni kidogo nabado nasubiria niwe na kikubwa?Kuna wati kwa sasa ni mwaka zaidi ya watatu wanasubiria kuwa na vingi na katika kipindi hiko wenzao wameshaanza kufanya kile amabcho wao wanasubiri na sasa wamefika mbali sana.Anza na kiddogo ulichonacho na anza pale ulipo.

Sababu ya pili ya watu kughairisha ni kwa sababu ya uoga wa kujaribu.Kuna watu wengi sana ambao wanashindwa kuanza kufanya kitu ambacho wanakitamani sana katika maisha yao kwa sababu wanaogopa kuanza kufanya.Hofu ya kufanya kitu kipya imewazuia watu wengi sana kuanza kufanya na kuendelea kughairisha kila siku.

Unachotakiwa kujua ni kuwa hadi pale umeanza kufanya kitu ambacho umekuwa unaogopa kukifanya ndipo utakapoanza kuwa na ujasiri wa kukifanya.Kuna watu wanaghairisha kufanya biashara kwa sababu wanaogopa kupata hasara,kuna watu wanaogopa kuishi ndoto zao kwa sababu wanahofia kujaribu kitu kipya n.k

Sababu ya tatu kusubiri sapoti ya kila mtu kabla ya kuanza kufanya kile wanachotaka.Kuna watu wengi sana ambao wanaghairisha kufanya mambo ambayo wangetakiwa wawe wameshaanza kuyafanya kwa sababu tu wanasubiri wapate sapoti ya watu mbalimbali katika maisha yao.Na wanaamini kuwa hawataweza kuanza kufanya kitu wanachotaka kukifanya hadi kila mtu amewasapoti na amekuwa upande wao.Hii imewafanya kuwa watu ambao wanasubiri kusapotiwa na kama wasipopewa sapoti basi wanabakia kuwalumu na kuendelea kusubiri.

Kumbuka kuwa bila kujali sababu gani inakuzuia kuanza kufanya unachokitaka itakubidi ufanye bidii kadiri unavyoweza ili uweze kuanza.Mafanikio yako yako katika kuanza.Chochote ambacho unataka kufanya,tafuta hatua ya kwanza ya kufanya na uichukue leo bila kuchelewa,Ukiendelea kila wakati kughairisha utajikuta unakuwa Mr/Mrs Tommorow.

Utakuwa mtu wa kila wakati kusema utafanya ila haufanyi.
 
Back
Top Bottom