Sababu kubwa ya Watanzania wasomi kutokurudi Tanzania kikazi ni kutokujua kuomba rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu kubwa ya Watanzania wasomi kutokurudi Tanzania kikazi ni kutokujua kuomba rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Dec 6, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Watanzania wenzangu ni wakali na kuambiana ukweli wa roho. Wazee wengi wa Tanzania na ndugu na jamaa mbalimbali wamekuwa wakishangaa vijana wengi huku nje je wanafanyanini huku wakati Tanzania vijana wenzao wanaendelea!? maswali kama haya ni ya kawaida kwa vijana waliosoma huku

  1. Unafanya nini huku wakati wenzako wanajenga?
  2. Kuna kazi zinalipa Tanzania je ni kwa nini mnawafanyia kazi wazungu huku?
  3. Ulaya na Marekani hakuna kitu?
  4. Kijana aliyemaliza chuo hapa Tanzania anawazidi nyie huko ulaya na marekani kimaisha

  Maswali ni mengi yasiyoisha hasa kama una mapungufu mengine kama kutokuoa n.k

  Mimi nikasema kuna ukweli basi ngoja nifuatilie kazi za bongo nione kama nayoambiwa ni ya kweli!. Ukweli ni kwamba watu wengi hawaishi kwa mshahara na wanavyopata pesa sikuweza kuelewa vizuri hata kwa marafiki na ndugu wa karibu!. Sasa nilipoanza kuuliza kwa undani jamani nitaishije bongo mbona gharama za kila kitu ziko juu na mshahara ni mdogo sana je nyie mnafanyanini? nilikuja kugundua mishahara yao siyo mikubwa ni TSH 1M-2M za kitanzania sasa unawezaje kuwa na gari, kodisha nyumba, kujenga n.k!!!. Nilipouliza zaidi ndiyo nilipo kasirisha watu zaidi lakini nikajua ukweli nini!!
  1. Ndugu zetu walioko Tanzania hawatujui vizuri kwasababu wote ni ndugu na tunaongea kiswahili lakini kunatofauti sana ya kijana aliyeenda chuo Tanzania baada ya kidato cha sita na aliyekuja ughaibuni mfano US. Kwa vijana tuliokuja US miaka ya tisini tulipomaliza Form 6 na tumeishi miaka kumi na huku kusoma na kufanya kazi tunaongea tu lakini wengi wetu hatujawahi kuomba rushwa au kuibia kazi kuanzia tuzaliwe!, hatuna semina za kudanganya huku, hakuna safari ya uongo huku, na hakuna mtu ayekupa pesa kwa lolote kwenye kazi za kampuni kubwa pesa huioni hata!. Hivyo wengi wetu ni washamba wa rushwa! hatujui kuomba wala kutoa na hiki ni kitu ambacho watu wengi wa bongo hawafahamu. Kwasababu unaongea kiswahili kama wenyewe, ni ndugu au rafiki wanasahau kwamba kuna vitu vya kijanja kijanja hujui hata kama unajua kuviongea.
  2.Tabia ya siri sisi huku tumezoe kuwa wakweli na kuongea vitu waziwazi vya kimaendeleo. Mtandao kama huu mambo yote hapa watu wa nje wanaweza kuongea waziwazi bila kujificha wenzetu wa kule kufisha vitu ni utamaduni hii ni kwasabau (a) wanafanya vitu vya kijanja kijanja hivyo hutaki watu wengi wajue (b) watu wanaogopa kuigwa hivyo wakipata kitu ambacho wengine hawajui wnaita "Line" na "Line" yako huwezi kuweka waziwazi!. Hivyo hata kwenye familia utashangaa vitu vingi hawkuambii kwenye simu ni kwasababu ya utamaduni wa siri kwenye mambo mengi ya maendeleo.

  Hivyo ndugu labda upate kazi nzuri inayokupa mshahara mkubwa wa kutosheleza mahitaji yote muhimu uwe makini sana na kudandia vijikazi vya Tanzania kwani gharama za maisha ni za juu na wengi wa watanzania wanaorudi ni wa shamba wa rushwa. Kuna wale waliokuja huku baada ya chuo wenyewe wanajua kidogo huo utamaduni lakini wengi wa wale walikuja baada ya form 6 Tanzania ni kugumu!. Vile vile kazi nzuri hazipo nyingi kwani hata kazi ni "Line" ya mtu!.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Pole ndugu yangu!

  tatizo ni kuwa hakuna hata mmoja anayeelewa au atakayefanyia kazi malalamiko yako! mwisho wa siku ni kuwa uwe na fedha uishi! kuwa zimepatikana vipi...hakuna anayejali hilo hata takukuru watakushangaa!

  Ninachoweza kusema ni kuwa ni kweli kabisa ethics za mtanzania wa nje na wa ndani ni tofauti. nje hata kama na tabia hiyo unayo utamfanyia nani?? nenda afrika kusini au india uone kama watanzania huko hawatoi na kupokea rushwa! inategema uko wapi!

  Kingine mnajisahau mno....mwisho mnaishia kwenye frustration kama hizi, nje ni sehemu ya kwenda kidogo kama miaka yako minne na kurudi nchini. kwa mfano kwa sisi mafundi tukienda nje na kurudi channel zote za kupata fedha zinakuwa hamna! hakuna anayekujua kwa sababu ''ULIJIUA' ulipoenda nje!! kutengeneza network na kuanza upya sio rahisi!

  Nina rafiki yangu nimemwacha ughaibuni na anapata mshahara wa serikali na kuutunza benki, mimi nikarudi fedha ile ile kwa wakati ule ule nikajenga nyumba, nondo mm 12 las december ilikuwa elfu 11, leo hii ni sh. elfu 17! ni mfano tu...kila kitu kinapanda na utakuta fedha yako yako uliyodunduliza huko haina thamani tena! hapa ni ujanja tu

  All in all siyo sahihi ku-generalize mambo......mawaziri na wasomi wengi walisoma nje enzi hizo na walirudi na leo ndio wezi wa kutupwa!
  wako ambao hawajawahi kwenda ulaya na wako humu ndani na hawaijui rushwa!

  Mwisho in develiping countries like this...kuna opportunity nyingi za kutengenza fedha tofauti na ulaya...zipo tu tena hauhitaji rushwa unahitaji akili ...au copy an paste kitu gani kiko London hakiko Tanzania!

  kuna sector za kilimo ambazo vijana wengi wanakimbilia na kutengeza pesa ya kufa mtu...siyo wezi! angalia films na miziki ilivyowatoa vijana...hizi zote rushwa?

  muwe waangalifu mnapotoa concern zenu humu na hasa kama hizi ambazo ni za kibaguzi , hata kama una frustration zako sema , omba msaada usaidiwe!!! nimekaa abroad kama wewe ila nikakumbuka Tanzania haraka...na hata sasa bado nachechemea maumivu ya kukaa nje....ila opportunities is there to grab them!

  ukikaa muda mrefu nchi siyo yako una kuwa ''second hand citizen'' ukirudi kwenye nchi ya wazazi wako unashangaa unakuwa tena ''second hand citizen''.....NA NDICHO UNACHOKUTANA NACHO SASA....pambana acha excuse na kunyoosha vidole, yes we have corrupt and we have clean people......they are every where in this planet even in USA! (take note here)

  Pambana rudi nyumbani life is in Tanzania...uliza upewe CLEAN DEALS THERE ARE PLENTY OF THEM...ask bakhresa will confirm the same!! tena nyingi hazihitaji usomi.......matajiri wengi nchi hii hawajaenda shule taka kidogo!

  another biggest problem kwa wasomi wengi ..they were tuned to be employed and they dont take risk!
   
Loading...