Sababu kubwa ya CCM kukata rufaa/ kulalamika!

TheDealer

JF-Expert Member
Nov 19, 2012
2,424
1,129
Sababu kuu ni hii kwa mjibu wa Januari Makamba na Abbas Mtemvu!

''KWA NINI WAMEKATAA KURA KUHESABIWA MARA YA PILI, MBONA WAPINZANI HUSUSANI NYAMAGANA KURA ZIMEHESABIWA MARA MBILI. HIYO NI HAKI KWA KILA MGOMBEA''

Hiyo hapo juu ndio hoja kuu ya CCM ya kukata rufaa ama kulalamika. Ukweli ni kuwa popote pale ambapo kura zimehasabiwa mara mbili CCM wameibuka washindi, hakuna popote pale ambapo kura zimehesabiwa mara mbili wapinzani wakaibuka kidedea! Maboksi ya kura yanakuwa chini ya umiliki wa CCM/serikali ya CCM mara baada ya kura kuhesabiwa. Wana uwezo wa kufanya lolote!

Kabla ya Wenje - Nyamagana kukubali kura kuhesabiwa mara mbili, tayari alikuwa ameshinda. Kabla ya kafulila kukubali(sina uhakika) kura kuhesabiwa mara mbili tayari Kafulila alishinda. Kafulila alikomaa kura zake zizihesabiwe mara mbili, sijui hili lilifikia wapi!

NEC hapo awali kabla ya kuanza kwa uchagzui walisema kuwa ile sheet ya idadi ya kura ndio ziende katani na jimboni na halmashauri. Hakuna haja ya kupeleka ma boksi!

NB: Haya ndio majimbo yanayokusudiwa kukatwa rufaa na CCM:
1. Kawe
2. Mikumi
3. Ndanda
4. Temeke (sina uhakika)
 
Hahahahahhaha naimani ata judge atashangaaa kuyaona ma ccm yakilalamika coz jeshi lao, tume yao, majengo ya manispaaa yao, wakurugenzi wao mpaka mabox wamenunua wao dah kweli pumzi ikikata kinachofata ni kuwekewa oxygen
 
tena makamba ametuboost anaweza kutuambia jimbo lake iweje idadi ya wapiga kura ya ubunge ni tofauti na ya urais wakati mpiga kura anapewa karatasi tatu
 
Wanakati rufaa kwani waliwekeza fedha nyingi kuhonga wapiga kura wakidhani watu wanaishi kwa tisheti,kofia na kanga.wengine wamekopa benki sasa hawajui watarejeshaje mkopo baada ya mrija kukatwa ghafla.kilichobaki ni kutafuta ushindi wa mezani na huruma ya mahakama baada ya kura kuwakataa ,na pia baada ya mbinu chafu kudhibitiwa.
 
Back
Top Bottom