Sababu kubwa kwa nini Tanzania tumekuwa tunatia sahihi mikataba mibovu

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,260
2,000
Nimeshitushwa na taarifa ya Barrick Gold inayokanusha kwamba hawajafikia makubaliano kwamba Watailipa Tanzania, bali walichosema ni kwamba wako tayari kufanya na mazungumzo na Tanzania ili kufikia muafaka juu ya suala la Acasia.

Sasa jiulize, hivi ujumbe wa Tanzania haukuelewa walichoongea Barrick Gold hadi kukimbilia kutoa press release kwamba Tanzania italipwa fidia na Acasia? Ni aibu sana kwa press release kutoka Ofisi ya Raisi kukanushwa namna hii. Inatufanya Watanzania tuonekane hatuna akili na hatujui kiingereza.

Sasa ni wazi kwamba sababu zilizoifanya Tanzania iingie mikataba mibovu ni pamoja na zifuatazo;
  1. Kutoilewa kwa ufasaha lugha ya kiingereza na lugha ya kisheria na kimikataba wakati wa mazungumzo na wawekezaji
  2. Kutoilewa sekta inayohusika katika huo mkataba (mfano madini, mafuta, usafirishaji wa anga, uzalishaji umeme, nk)
  3. Rushwa za moja kwa moja na kulainishwa kwa zawadi kubwa na ndogondogo
  4. Kuwathamini sana wazungu na kuamini kila wanachosema wanapodai wanaweka maslahi ya Tanzania mbele na ushirikiano
  5. Kutokuwa na uzoefu wa kufanya mazungumzo (negotiations) yanayohusu mikataba ya kimataifa
  6. Kushinikizwa na viongozi wa juu, na hasa Ofisi ya Raisi
  7. Kutokuwa na uzalendo na Tanzania
Ushauri wangu kwa Raisi Magufuli ni kwamba aanzishe kitengo maalum katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambacho kazi yake itakuwa ni kupitia kila aina ya mikataba ya serikali na nchi au mashirika ya nje, na kutoa ushauri kwa BUnge na serikali. Kitengo hiki kiwe na watu waliobobea katika sheria za mikataba (law of contract) pamoja na commercial laws, na serikali ihakikishe kinapewa mafunzo hata zaidi. Iwe wazi kwamba hakuna mktaba wa serikali na nchi au shirika lolote utapelekwa Bungeni au kuidhinishwa bila kuwa umepitiwa na hiki kitengo. Mkataba unapoenda Bungeni basi uwe na ushauri na mapendekezo kutoka kitengo hiki.
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,474
2,000
Kushinikizwa na viongozi wa juu, na hasa Ofisi ya Raisi
Mhh, hapa! Kweli hata kama una nia njema ukishinikizwa umeshinikizwa tu. Mfano aliyesaini mkataba wa 'terrible teen' na bombadia sidhani kama alipata muda wa kutumia reasoning binafsi zaidi ya kusukumwa na 'uzalendo'!
 
Jirani yetu mmoja alikuwa kila mwaka akishika nafasi za juu kwenye list ya Transparent International kama mla na mtoa rushwa mkuu. Sasa mwaka ambao hawakutokea watu wakawa wanashangaa nini kilijiri wakati rushwa inazidi kushamiri ...mara, kumbe waliweza kupenya na 'kumhonga' aliyekuwa anacompile hiyo repoti!!
Sasa usije kushangaa ukishaunda hicho kitengo yale yale majamaa yaliyoingia mikataba ya awali ndio yanaenda 'kuwaona' na kuwahakikishia apartments mbili tatu Mikocheni au Mbezi then 2030 watakaokuwepo watakuwa wanashangaa kuwa "wajumbe walikuwa wanajua sana mambo ya mikataba na walikuwa best students Harvard University!".
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,260
2,000
Mhh, hapa! Kweli hata kama una nia njema ukishinikizwa umeshinikizwa tu. Mfano aliyesaini mkataba wa 'terrible teen' na bombadia sidhani kama alipata muda wa kutumia reasoning binafsi zaidi ya kusukumwa na 'uzalendo'!

Hahah! Mkuu, hapo rudi kwenye namba 2 na 3 - kutoielewa vema sekta inayohusika, na kuamini kila wanachokuambia wazungu kwamba wanataka kukusaidia. Unaweza ukawa na uzalendo lakini ukaishia kutia sahihi mkataba bogus kwa sababu huielewi vema sekta inayohusika, au wazungu wamekuona wewe mtupu wakakudanganya na kukupa ndege bogus ukafikiri umefuma dili la maana.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,260
2,000
Jirani yetu mmoja alikuwa kila mwaka akishika nafasi za juu kwenye list ya Transparent International kama mla na mtoa rushwa mkuu. Sasa mwaka ambao hawakutokea watu wakawa wanashangaa nini kilijiri wakati rushwa inazidi kushamiri ...mara, kumbe waliweza kupenya na 'kumhonga' aliyekuwa anacompile hiyo repoti!!
Sasa usije kushangaa ukishaunda hicho kitengo yale yale majamaa yaliyoingia mikataba ya awali ndio yanaenda 'kuwaona' na kuwahakikishia apartments mbili tatu Mikocheni au Mbezi then 2030 watakaokuwepo watakuwa wanashangaa kuwa "wajumbe walikuwa wanajua sana mambo ya mikataba na walikuwa best students Harvard University!".

Kuna mambo mengine MKuu, ni beyond control. Ushauri unaoletwa na hicho kitengo, changanya na akili za Wabunge, na zako kama raisi, kama bado tutaishia kuwa na mikataba mibovu, basi twafwaaaa!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom