Sababu Kubwa 2 za Kuukataa Mchakato huu wa Katiba Mpya

Asante Mkuu wangu Mzee Mwanakijiji, na hiyo ndio thamani ya maneno yenye hekima, hayaozi. Ninakubaliana nawe kwa nguvu zangu zote unaposema TUNAWEZA KUSUBIRI! Lakini pia nitoe kama angalizo;
1. Tunachoweza kusubiri kwa miaka mitano au zaidi si kuanza kwa mchakato wa upatikanaji wa katiba, bali ni kuipata katiba yenyewe. Hivyo huu ni wakati muafaka wa kuanza mchakato huo. Kama unavyoamini mwenyewe nafasi ya WANANCHI katika hilo, hao wananchi WAPO tangu jana na leo.
2. Kusubiri miaka mitano au zaidi kupata katiba mpya, si kwa sababu ya kusubiri chama fulani na uongozi makini kusimamia mchakato huo, chini ya mifumo iliyopo(demokrasia) kupata chama na uongozi bora ni MCHEZO WA BAHATI NASIBU katika nchi za watu weusi, hatuwezi kuweka rehani maisha ya watoto wetu kiasi hicho. Hakuna guarantee ya kupata chama na uongozi imara hata baada ya miaka hiyo 5. Pia, WATU makini huunda KATIBA makini, ambayo itazaa UONGOZI BORA. Hakuna nafasi ya chama katika hilo, katiba inaweza kuamua namna bora ya kupata uongozi imara hata NJE YA VYAMA. Watu hao makini MPO! Kwanini tusubiri chama? Binafsi naona kama ni kuwalisha sumu mbaya wananchi kuwa nje ya vyama hakuna wawezalo kufanya.
3. Ninapounga mkono haja ya kuvumilia kupata katiba mpya tusikurupuke, ni kutokana na UNYETI WA JAMBO LENYEWE. Katiba si kitu cha kufanyia majaribio, tunaweza kuwaweka utumwani watoto wetu kwa zaidi ya vizazi 20 baada yetu, kwa papara zetu leo.
"Tuna uwezo na watu ambao wanaweza kuangalia ni jinsi gani kutengeneza mfumo mzuri wa kusimamia uandikishwaji wa katiba mpya bila kuwanyang'anya wananchi madaraka yao" pamoja sana mkuu kwa hili. KATIBA BORA INAWEZA KUPATIKANA HATA KAMA KUTAKUWA NA CHAMA NA UONGOZI MBOVU KAMA WA LEO, HATUHITAJI KUSUBIRI MTU FULANI AU CHAMA. Dhana ya wawakilishi(under democracy) ndiyo inayotunyonga. MLIJIDANGANYA kufikiri muwaitao wawakilishi wenu wata play mbadala yenu. Imeshathibitika HAIWEZEKANI, na TUICHEZE WENYEWE SASA. Ukishafungwa na kanuni za kulinda ama kufuata ama kutetea demokrasia, katika fikra zako za kuwakomboa wanaafrika hawa wa Tanzania, UMESHAPOTEA TAYARI.
Ubunifu haujawahi kufika mwisho. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU. Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
CCM wakitaka mabavu katika hili powa tu, tuwaaachie waje na katiba yao halafu tukutane nao mtaani. Ninachotahadharisha tu wapenda mageuzi wote tukatae huu upuuzi mapema tusijidanganye eti tutaikataa ikishaletwa mezani wakati wasimamizi wa hiyo kura ya maoni ni NEC ya CCM!
 
Mwanakijiji wewe uko ulaya, acha kutuhadaa watanzania, tuache tupate katiba mpya

Kwani mnataka kuandika Katiba ya Watanzania walioko Tanzania tu? Tumia vizuri chembe za Ubongo ulizojaliwa na Mwenyezi Mungu... usifanye zikaonekana haramu!
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, pole!,
Its too little too late!,
Kama unaukumbuka uzi wangu huu, [h=3]Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele![/h]na tulibishana sana nini juu ya Chadema kufanya makosa?!. Wewe ndio ulikuwa mtetezi wao mkuu kuwa hawakukosea kitu!. Kinachoendelea sasa, is just a part payment, of a price Chadema has to pay!.

Chadema imeishafanya kosa, maji imeishayavulia nguo!, imebaki kuyaoga tuu!.

Hata hivyo, kufanya kosa, sio kosa!, kosa kurudia kosa!.
Kujitoa sasa ni kurudia kosa!, hili ndilo litakuwa kosa kubwa zaidi!.
Pasco.
 
Ipo haja ya kuchapana kisawa sawa kwanza ndiyo tuheshimiane, tukiisha heshimiana tutaandika katiba mpya itakayo linda maslahi ya nchi na vizazi vyetu vijavyo!
 
Mheshimiwa sana Mwanakijiji,

Kwanza nakupongeza kwa hoja nzuri ambayo imebadilisha kabisa msimamo wangu wa NEUTRAL.Kwani awali nilikuwa siwaelewi kwa kiasi kikubwa CHADEMA waliposema kuwa wanajitoa katika mckakato huu!

Sasa nawaelewa iwapo tu msimamo wao umejengwa katika msingi huu wa sheria ya kusimamia mchakato mzima na ndo kusema kuwa udhaifu wa chaguzi wajumbe ya mabaraza ya katiba kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilayani kumbe unatokana na udhaifu wa sheria yenyewe.Kwa hili sasa nawaunga mkono CHADEMA na naungana na upande wanaotaka katiba ya kweli.....si hii inayopalilia ulaji wa watawala waliopo ili waendelee kuwepo milele.CHADEMA jitoeni,waacheni watengeneze katiba yao......Tuko nyuma yenu
 
Je wapo ambapo wanauunga mkono mchakato huu? Kwanini wanafanya hivyo wajaribu kutushawishi na sisi wengine...
 
WATANZANIA wameweza kusubiri kwa karibu miaka ishirini sasa kuweza kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya.
Bahati mbaya subira hii inataka kuchukuliwa kama papara au haraka ya kukubali kila kinachowekwa mezani.
Nina uhakika wa kutosha kuwa Watanzania wanaweza kusubiri miaka mingine mitano ili kije chama na uongozi ambao utasimamia mchakato wa katiba mpya kwa misingi ya usawa, uwazi, haki na kukubali kuwa wananchi ndio msingi wa utawala wote na ambao kwao madaraka yote hutoka.

Bahati mbaya sana kuna watu ambao wanaamini kuwa kwa vile tumeshakubaliana kama taifa tunastahili katiba mpya, basi mchakato wa kufikia katiba hiyo uwe ule ambao wao wameamua bila kujali kanuni za msingi za kuiandika.
Matokeo yake ni kuwa mswada wa kwanza uliopendekezwa na watawala wetu kusimamia mchakato wa kuandika katiba hii tuliupiga vita na kulazimisha urudishwe na kufikiriwa upya.
Sasa watu makini wangetarajia kuwa waandishi wa mswada ule wangefikiria vizuri na kusikiliza kwanini tulipinga awali. Kinyume chake wameandaa mswada mwingine ambao japo umefanyiwa mabadiliko, bado una matatizo yale yale na hivyo unatuachia uchaguzi mmoja tu - yaani kuupinga.

Sasa tusiupinge bila kuainisha sababu hasa za kuupinga ni nini. Kuna kanuni kubwa mbili ambazo naamini mtu yeyote ambaye atapitia mswada huo wa sheria anaweza kuziona zikiwa zimevunjwa toka mwanzo kabisa wa mchakato unaopendekezwa.
Kwanza ni kutoheshimu mamlaka ya wananchi kujitungia katiba yao, na pili vipengele vingi vya mswada unaopendekezwa vinathibitisha hilo la kwanza.

Kutoheshimu mamlaka ya wananchi

Hili jambo nimewahi kuliandika huko nyuma, lakini kwa vile kuna uwezekano kwamba baadhi ya watu hawaamini jambo hili, si vibaya kurudia tena. Katika nchi ya kidemokrasia mamlaka yanatoka kwa wananchi. Yaani, madaraka hayapo kwa rais, kwa Bunge au kwa jeshi bali kwa wananchi. Ni wao ndio wanaamua serikali gani wanataka wawe nayo, iweje, na iongoze vipi. Wananchi ndio msingi wa madaraka yote nchini. Kwa maneno mengine katiba inatakiwa itoke kwa wananchi. Siyo katika kuipigia kura tu, bali katika uandikaji wake.

Katiba ambayo haitoki kwa wananchi na ambayo haiweki ushiriki wa juu kabisa wa wananchi toka mwanzo, haiwezi kudai kuwa ni katiba ya wananchi hao. Sheria hii inaweka nguvu kubwa sana mikononi mwa rais - hili watu wengi wameishalionesha. Kwa upande wangu hata hivyo tatizo ni zaidi ya kuwa “rais anapewa madaraka makubwa”. Tatizo langu kubwa ni kwamba rais anachukua madaraka ya wananchi kuandika katiba.

Hili ni kweli kwa kuangalia vipengele mbalimbali vya mswada huo:
Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar…ataunda tume (Ibara ya 5);
Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar atateua wajumbe wa tume (Ibara ya 6.1);
Katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa tume, Rais atazingatia masuala yafuatayo…(e) vigezo vingine ambavyo rais ataona vinafaa;
Hadidu za rejea za tume zitatolewa na rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar. Ibara ya 8.1 na 8.1 inasema Rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar anaweza kuongeza muda wa tume kukamilisha ripoti yake kwa muda usiozidi miezi mitatu;
Kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake, kila mjumbe wa tume na katibu ataapa au kula yamini mbele ya Rais (Ibara ya 11);
Katibu wa Sekretariati ya Tume atateuliwa na Rais baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar (Ibara 13.2);
Baada ya tume kumaliza kazi yake itawasilisha ripoti yake kwa Rais na Rais wa Zanzibar (Ibara ya 18.1);
Baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar… Rais atamuagiza Waziri kuwasilisha mswada wa Katiba katika Bunge la Katiba (Ibara ya 18.2);

Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar…ataunda Bunge la Katiba (Ibara ya 20.1);
Rais atachapisha majina ya watu atakaowateua kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba (Ibara ya 20.4);
Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba kabla ya kushika madaraka yao wataapa au kula yamini mbele ya Rais (Ibara ya 20.5).
Sasa, kwa mtu yeyote ambaye amewahi kupita kwenye majengo ya shule anaweza kukiona kitu kimoja kilicho wazi sana - mchakato wa katiba mpya unamhitaji rais ili kufanikiwa na kuwa halali.
Lakini siyo kumhitaji rais tu bali kumfanya kuwa ndiye kiini cha mchakato mzima.
Naweza kusema kwa ujasiri wa ukweli mchakato unaopendekezwa ukikubaliwa utamfanya rais kuwa ndiye mwanzo na mwisho wa mchakato wa kuandika katiba mpya na siyo wananchi.

Sasa swali ambalo litaundwa mara moja ni kuwa; “sasa unataka tume aunde nani au iundwe vipi bila rais?” Kwa wengine hili ni swali la kiakili, lakini ukitambua kuwa katiba tunayotaka kuiandika ni ya wananchi, basi jibu haliwezi kuwa mbali hivyo.
Ninaamini kuwa tuna uwezo na watu ambao wanaweza kuangalia ni jinsi gani tutengeneze mfumo mzuri wa kusimamia uandikishaji wa katiba mpya bila kuwanyang’anya wananchi madaraka hayo.
Binafsi nina mapendekezo yangu, lakini ninaamini kuwa wapo watu katika nchi yetu wenye uwezo wa kufikiria namna gani mchakato uwe bila kumfanya rais mfalme wa mchakato huu.

Ili kuweza kufikia hilo, maswali mawili yanatakiwa yajibiwe na hapo ndipo mapendekezo mbalimbali yanaweza kutolewa.
La kwanza – je, tunaweza vipi kuunda tume ya kusimamia mchakato wa kuandika katiba mpya bila kumpatia rais madaraka ya kufanya hivyo?
Jibu la swali hili litaonesha tuna uwezo gani wa kufikiria nje ya vile tulivyozoea. Kwa muda mrefu imekuwa ni rahisi kwa watu kumrundukia madaraka na majukumu rais kwa sababu hatuoni njia nyingine ya kufanya mambo.
Swali pili – je, katika mchakato huo tutahakikisha kuwa wananchi wanashiriki kwa kiwango cha juu kabisa (maximum participation of the people) badala ya ilivyo sasa?
Kwa mfano, mswada huu ukikubaliwa katiba mpya itapitishwa na kwa asilimia 50 ya wapiga kura ya maoni. Yaani, nusu tu ya wananchi wakisema “ndiyo” kwenye kura ya maoni basi tutakuwa na katiba mpya. Na kuna mtu aliamini kuwa hiyo ni ‘brilliant idea’!

CCM itatunga na kupitisha katiba mpya

Hili linatuleta kwenye sehemu ya pili ambayo kimsingi ni kuwa kile kipengele cha kusimamia mchakato wa katiba kinavunja ile kanuni ya kwanza hapo juu - kwamba vinaondoa madaraka ya wananchi kuandika katiba.
Mswada huu ukipita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa kimeuteka rasmi mjadala wa katiba kwani kitasimamia mchakato mzima kupitisha peke yake, tena kwa kutegemea wananchi wake tu - wananchi wengine wote watakuwa wasindikizaji.

Angalia mambo haya mawili yaliyofichwa kiaina ndani ya mswada huu:
Katiba mpya kuwa halali ikipitishwa na asilimia 50 tu ya wapiga kura ya maoni.
Mswada huu unatuambia kuwa matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa.
Kwamba, matokeo hayo yataamuliwa “kwa msingi wa kuungwa mkono kwa asilimia inayozidi hamsini ya jumla ya kura zote” zitakazopigwa Zanzibar na Tanzania bara.
Yaani, asilimia 50 ya Watanzania wanaweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa taifa letu na tukasema ni uamuzi wa “Watanzania”.
Katiba mpya si uchaguzi wa rais au mbunge, ni kuamua kubadilisha kwa kiasi kikubwa sana maisha yetu na ya watoto wetu. Kweli tunataka asilimia hamsini kati yetu waamue hatima hiyo?
Mfumo wa hilo linaloitwa “Bunge la Katiba” ukikubaliwa, CCM itakuwa imeteka rasmi mchakato mzima wa katiba na kwa kweli hakuna kitakachowazuia kuupeleka wanavyotaka wao.
Fikiria kuwa pendekezo la sasa hivi lilivyo ni kuwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano na Wawakilishi wote wa Zanzibar watakuwemo kwenye Bunge la Kutunga Katiba. Hii ina maana ya kwamba, tayari Chama Cha Mapinduzi kitajipa uwiano usio wa kawaida katika baraza hilo.

Bunge letu linatakiwa liwe na wabunge 357; kati ya hawa 258 wanatoka Chama Cha Mapinduzi na upinzani unao 80. Tukiwajumlisha na wale 10 wanaoteuliwa na rais ambapo mmoja ni kutoka CUF, tunaweza kuona kuwa wabunge wenye kuhusiana na rais ni wengi zaidi.
Kwa vile wawakilishi wote kutoka Zanzibar nao wanapendekezwa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba, ni wazi kuwa CCM inajiongezea wajumbe wengine 30 na upinzani 19 kutoka Zanzibar. Hapa sijali muafaka kati ya CCM na CUF.
Kwa misingi hiyo, kwenye Baraza la Kutunga Katiba Chama Cha Mapinduzi kitakuwa na wajumbe wasiopungua 297. Upinzani utakuwa na wajumbe 110.

Kwa kuangalia uwiano huo tu, ni kuwa CCM tayari itakuwa na wingi wa wajumbe kwa uwiano wa karibu 3:1. Sasa tunaambiwa pia kuwa kutakuwa na wajumbe wengine 116 kutoka taasisi mbalimbali kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya mswada huo.
Sasa cha kutufanya tufikirie ni kuwa ni rais ndiye atakayewateua watu hao 116. Je, itakuwa ni makosa sana kufikiria kuwa atachagua watu ambao wanakubaliana naye au wale wenye mrengo wa chama chake? Je, akiwateua watu wengi (kati ya hao 116) ambao wanaelekea kukubaliana naye kuna mtu anaweza kumuuliza?

Kimsingi kwa mfumo unaopendekezwa ni wazi kuwa Bunge la Katiba litakuwa na wajumbe wasiopungua 523. Hii ni idadi ndogo sana ya
Baraza la Kutunga Katiba.

Binafsi naamini kwanza kabisa wabunge na mawaziri wasiwe sehemu hii kwa sababu moja kubwa, tayari wao wanawajibika na majukumu yao ya kikatiba na majimbo yao. Kuwaongezea hili ni kuwapa majukumu zaidi yasiyo na sababu.
Baraza la Kutunga Katiba lisiwe na watu wasiopungua 2,000 ambao watatoka miongoni mwa wananchi na wakiwakilisha sehemu kubwa ya wananchi wetu (cross section).

Kwa mtindo ambao unapendekezwa na mswada, kuna uwezekano mkubwa kwamba baraza hili litakuwa ni la wasomi watupu.
Fikiria kuwa hao wajumbe 116 watatoka kwenye makundi matano, yaani asasi zisizo za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na makundi yenye mahitaji maalumu.
Sasa nina uhakika kuna mtu amejiaminisha huko waliko kuwa katiba mpya inahitaji kuandikwa na wasomi peke yao. Ndugu zangu, tukikubali hili tutakuwa tumenyang’anya haki ya wananchi kujiandikia katiba yao.

Wananchi wengi wa Tanzania siyo wasomi sana na siyo wote wako kwenye hizo taasisi tano.
Binafsi ninaamini ni lazima chombo kitakachoandika katiba kiwe kinawakilisha jamii yetu nzima (must represent the cross-section of our society).

Je, wakulima na maskini wanawakilishwa vipi? Je, makundi madogo (minority groups) wanawakilishwa vipi?
Tusije kugeuza mchakato wa katiba kuwa mchakato wa watu ambao tayari wana kiu ya madaraka na wameonja madaraka wakatutengenezea kitu cha kuzidi kuwapa wao madaraka ya kuwatawala wengine.
Hivyo basi, hata kama nisingeingia ndani na kuvichambua vipengele vyote vya mswada huo, naweza kusema kwa uhakika wa dhamira yangu kuwa ni miongoni mwa miswada mingine mibovu ambayo inaandikwa na watu ambao tunaamini wana akili timamu, na wasomi.
Na kama hawa ndio ambao watakuja kutuandikia katiba mpya, basi tunajitumbukiza wenyewe kwenye shimo ambalo tunajua hatuwezi kutoka.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba kwa vile CCM haijawahi kuwa na ajenda ya katiba mpya na sasa inaonekana wamekusudia kabisa kuliburuza taifa zima kama mtu huru, nakataa kuburuzwa hivyo na binafsi ninaukataa mchakato huu unaoongozwa na chama hicho kwa misingi ya geresha ya kisiasa.

Nakataa mara moja na daima mchakato mzima ambao unapendekezwa na mswada huu, na ni matumaini yangu wengine nao wataukataa hivyo hivyo.

Kama CCM haiwezi kubuni mfumo bora wa kusimamia mchakato wa katiba mpya na badala yake kuturudishia kitu kile kile ambacho tumekikataa miezi michache iliyopita, ni jukumu letu kukataa siyo tu kuunga mkono mchakato huu bali pia kushiriki endapo utapitishwa - na uwezekano wa kupita ni mkubwa kwani wao ni wengi, rais wao na vyombo vyote vyao.

Ninachoweza kusema ni kwamba kama CCM na serikali yake watalazimisha kutulisha katiba mpya kwa nguvu, ni wajibu wetu kukataa kushiriki kwenye mijadala yao na kwa hakika kwenye kura ya maoni watakayoitisha.

Kama tumeweza kusubiri miaka 20, nina uhakika tunaweza kusubiri miaka mingine mitano kwani tunajua ni kina nani kweli walipigania katiba mpya. Wanaotaka katiba mpya ya CCM waendelee na mchakato wao, wanaotaka katiba mpya kwa ajili ya Watanzania wote wasubiri wakati wao. Kwani miaka minne iliyobakia si mingi.

h.sep3.gif

blank.gif

M. M. Mwanakijiji
WATANZANIA wameweza kusubiri kwa karibu miaka ishirini sasa kuweza kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya.
Bahati mbaya subira hii inataka kuchukuliwa kama papara au haraka ya kukubali kila kinachowekwa mezani.
Nina uhakika wa kutosha kuwa Watanzania wanaweza kusubiri miaka mingine mitano ili kije chama na uongozi ambao utasimamia mchakato wa katiba mpya kwa misingi ya usawa, uwazi, haki na kukubali kuwa wananchi ndio msingi wa utawala wote na ambao kwao madaraka yote hutoka.
Bahati mbaya sana kuna watu ambao wanaamini kuwa kwa vile tumeshakubaliana kama taifa tunastahili katiba mpya, basi mchakato wa kufikia katiba hiyo uwe ule ambao wao wameamua bila kujali kanuni za msingi za kuiandika.
Matokeo yake ni kuwa mswada wa kwanza uliopendekezwa na watawala wetu kusimamia mchakato wa kuandika katiba hii tuliupiga vita na kulazimisha urudishwe na kufikiriwa upya.
Sasa watu makini wangetarajia kuwa waandishi wa mswada ule wangefikiria vizuri na kusikiliza kwanini tulipinga awali. Kinyume chake wameandaa mswada mwingine ambao japo umefanyiwa mabadiliko, bado una matatizo yale yale na hivyo unatuachia uchaguzi mmoja tu - yaani kuupinga.
Sasa tusiupinge bila kuainisha sababu hasa za kuupinga ni nini. Kuna kanuni kubwa mbili ambazo naamini mtu yeyote ambaye atapitia mswada huo wa sheria anaweza kuziona zikiwa zimevunjwa toka mwanzo kabisa wa mchakato unaopendekezwa.
Kwanza ni kutoheshimu mamlaka ya wananchi kujitungia katiba yao, na pili vipengele vingi vya mswada unaopendekezwa vinathibitisha hilo la kwanza.
Kutoheshimu mamlaka ya wananchi
Hili jambo nimewahi kuliandika huko nyuma, lakini kwa vile kuna uwezekano kwamba baadhi ya watu hawaamini jambo hili, si vibaya kurudia tena.
Katika nchi ya kidemokrasia mamlaka yanatoka kwa wananchi.
Yaani, madaraka hayapo kwa rais, kwa Bunge au kwa jeshi bali kwa wananchi. Ni wao ndio wanaamua serikali gani wanataka wawe nayo, iweje, na iongoze vipi.
Wananchi ndio msingi wa madaraka yote nchini. Kwa maneno mengine katiba inatakiwa itoke kwa wananchi. Siyo katika kuipigia kura tu, bali katika uandikaji wake.
Katiba ambayo haitoki kwa wananchi na ambayo haiweki ushiriki wa juu kabisa wa wananchi toka mwanzo, haiwezi kudai kuwa ni katiba ya wananchi hao.
Sheria hii inaweka nguvu kubwa sana mikononi mwa rais - hili watu wengi wameishalionesha. Kwa upande wangu hata hivyo tatizo ni zaidi ya kuwa “rais anapewa madaraka makubwa”. Tatizo langu kubwa ni kwamba rais anachukua madaraka ya wananchi kuandika katiba.
Hili ni kweli kwa kuangalia vipengele mbalimbali vya mswada huo:
Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar…ataunda tume (Ibara ya 5);
Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar atateua wajumbe wa tume (Ibara ya 6.1);
Katika kufanya uteuzi wa wajumbe wa tume, Rais atazingatia masuala yafuatayo…(e) vigezo vingine ambavyo rais ataona vinafaa;
Hadidu za rejea za tume zitatolewa na rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar. Ibara ya 8.1 na 8.1 inasema Rais kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar anaweza kuongeza muda wa tume kukamilisha ripoti yake kwa muda usiozidi miezi mitatu;
Kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake, kila mjumbe wa tume na katibu ataapa au kula yamini mbele ya Rais (Ibara ya 11);
Katibu wa Sekretariati ya Tume atateuliwa na Rais baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar (Ibara 13.2);
Baada ya tume kumaliza kazi yake itawasilisha ripoti yake kwa Rais na Rais wa Zanzibar (Ibara ya 18.1);
Baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar… Rais atamuagiza Waziri kuwasilisha mswada wa Katiba katika Bunge la Katiba (Ibara ya 18.2);
Rais, baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar…ataunda Bunge la Katiba (Ibara ya 20.1);
Rais atachapisha majina ya watu atakaowateua kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba (Ibara ya 20.4);
Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba kabla ya kushika madaraka yao wataapa au kula yamini mbele ya Rais (Ibara ya 20.5).
Sasa, kwa mtu yeyote ambaye amewahi kupita kwenye majengo ya shule anaweza kukiona kitu kimoja kilicho wazi sana - mchakato wa katiba mpya unamhitaji rais ili kufanikiwa na kuwa halali.
Lakini siyo kumhitaji rais tu bali kumfanya kuwa ndiye kiini cha mchakato mzima.
Naweza kusema kwa ujasiri wa ukweli mchakato unaopendekezwa ukikubaliwa utamfanya rais kuwa ndiye mwanzo na mwisho wa mchakato wa kuandika katiba mpya na siyo wananchi.
Sasa swali ambalo litaundwa mara moja ni kuwa; “sasa unataka tume aunde nani au iundwe vipi bila rais?” Kwa wengine hili ni swali la kiakili, lakini ukitambua kuwa katiba tunayotaka kuiandika ni ya wananchi, basi jibu haliwezi kuwa mbali hivyo.
Ninaamini kuwa tuna uwezo na watu ambao wanaweza kuangalia ni jinsi gani tutengeneze mfumo mzuri wa kusimamia uandikishaji wa katiba mpya bila kuwanyang’anya wananchi madaraka hayo.
Binafsi nina mapendekezo yangu, lakini ninaamini kuwa wapo watu katika nchi yetu wenye uwezo wa kufikiria namna gani mchakato uwe bila kumfanya rais mfalme wa mchakato huu.
Ili kuweza kufikia hilo, maswali mawili yanatakiwa yajibiwe na hapo ndipo mapendekezo mbalimbali yanaweza kutolewa.
La kwanza – je, tunaweza vipi kuunda tume ya kusimamia mchakato wa kuandika katiba mpya bila kumpatia rais madaraka ya kufanya hivyo?
Jibu la swali hili litaonesha tuna uwezo gani wa kufikiria nje ya vile tulivyozoea. Kwa muda mrefu imekuwa ni rahisi kwa watu kumrundukia madaraka na majukumu rais kwa sababu hatuoni njia nyingine ya kufanya mambo.
Swali pili – je, katika mchakato huo tutahakikisha kuwa wananchi wanashiriki kwa kiwango cha juu kabisa (maximum participation of the people) badala ya ilivyo sasa?
Kwa mfano, mswada huu ukikubaliwa katiba mpya itapitishwa na kwa asilimia 50 ya wapiga kura ya maoni. Yaani, nusu tu ya wananchi wakisema “ndiyo” kwenye kura ya maoni basi tutakuwa na katiba mpya. Na kuna mtu aliamini kuwa hiyo ni ‘brilliant idea’!
CCM itatunga na kupitisha katiba mpya
Hili linatuleta kwenye sehemu ya pili ambayo kimsingi ni kuwa kile kipengele cha kusimamia mchakato wa katiba kinavunja ile kanuni ya kwanza hapo juu - kwamba vinaondoa madaraka ya wananchi kuandika katiba.
Mswada huu ukipita Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa kimeuteka rasmi mjadala wa katiba kwani kitasimamia mchakato mzima kupitisha peke yake, tena kwa kutegemea wananchi wake tu - wananchi wengine wote watakuwa wasindikizaji.
Angalia mambo haya mawili yaliyofichwa kiaina ndani ya mswada huu:
Katiba mpya kuwa halali ikipitishwa na asilimia 50 tu ya wapiga kura ya maoni.
Mswada huu unatuambia kuwa matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa wingi wa kura zitakazopigwa.
Kwamba, matokeo hayo yataamuliwa “kwa msingi wa kuungwa mkono kwa asilimia inayozidi hamsini ya jumla ya kura zote” zitakazopigwa Zanzibar na Tanzania bara.
Yaani, asilimia 50 ya Watanzania wanaweza kubadilisha kabisa mwelekeo wa taifa letu na tukasema ni uamuzi wa “Watanzania”.
Katiba mpya si uchaguzi wa rais au mbunge, ni kuamua kubadilisha kwa kiasi kikubwa sana maisha yetu na ya watoto wetu. Kweli tunataka asilimia hamsini kati yetu waamue hatima hiyo?
Mfumo wa hilo linaloitwa “Bunge la Katiba” ukikubaliwa, CCM itakuwa imeteka rasmi mchakato mzima wa katiba na kwa kweli hakuna kitakachowazuia kuupeleka wanavyotaka wao.
Fikiria kuwa pendekezo la sasa hivi lilivyo ni kuwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano na Wawakilishi wote wa Zanzibar watakuwemo kwenye Bunge la Kutunga Katiba. Hii ina maana ya kwamba, tayari Chama Cha Mapinduzi kitajipa uwiano usio wa kawaida katika baraza hilo.
Bunge letu linatakiwa liwe na wabunge 357; kati ya hawa 258 wanatoka Chama Cha Mapinduzi na upinzani unao 80. Tukiwajumlisha na wale 10 wanaoteuliwa na rais ambapo mmoja ni kutoka CUF, tunaweza kuona kuwa wabunge wenye kuhusiana na rais ni wengi zaidi.
Kwa vile wawakilishi wote kutoka Zanzibar nao wanapendekezwa kuwa wajumbe wa Bunge la Katiba, ni wazi kuwa CCM inajiongezea wajumbe wengine 30 na upinzani 19 kutoka Zanzibar. Hapa sijali muafaka kati ya CCM na CUF.
Kwa misingi hiyo, kwenye Baraza la Kutunga Katiba Chama Cha Mapinduzi kitakuwa na wajumbe wasiopungua 297. Upinzani utakuwa na wajumbe 110.
Kwa kuangalia uwiano huo tu, ni kuwa CCM tayari itakuwa na wingi wa wajumbe kwa uwiano wa karibu 3:1. Sasa tunaambiwa pia kuwa kutakuwa na wajumbe wengine 116 kutoka taasisi mbalimbali kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya mswada huo.
Sasa cha kutufanya tufikirie ni kuwa ni rais ndiye atakayewateua watu hao 116. Je, itakuwa ni makosa sana kufikiria kuwa atachagua watu ambao wanakubaliana naye au wale wenye mrengo wa chama chake? Je, akiwateua watu wengi (kati ya hao 116) ambao wanaelekea kukubaliana naye kuna mtu anaweza kumuuliza?
Kimsingi kwa mfumo unaopendekezwa ni wazi kuwa Bunge la Katiba litakuwa na wajumbe wasiopungua 523. Hii ni idadi ndogo sana ya Baraza la Kutunga Katiba.
Binafsi naamini kwanza kabisa wabunge na mawaziri wasiwe sehemu hii kwa sababu moja kubwa, tayari wao wanawajibika na majukumu yao ya kikatiba na majimbo yao. Kuwaongezea hili ni kuwapa majukumu zaidi yasiyo na sababu.
Baraza la Kutunga Katiba lisiwe na watu wasiopungua 2,000 ambao watatoka miongoni mwa wananchi na wakiwakilisha sehemu kubwa ya wananchi wetu (cross section).
Kwa mtindo ambao unapendekezwa na mswada, kuna uwezekano mkubwa kwamba baraza hili litakuwa ni la wasomi watupu.
Fikiria kuwa hao wajumbe 116 watatoka kwenye makundi matano, yaani asasi zisizo za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na makundi yenye mahitaji maalumu.
Sasa nina uhakika kuna mtu amejiaminisha huko waliko kuwa katiba mpya inahitaji kuandikwa na wasomi peke yao. Ndugu zangu, tukikubali hili tutakuwa tumenyang’anya haki ya wananchi kujiandikia katiba yao.
Wananchi wengi wa Tanzania siyo wasomi sana na siyo wote wako kwenye hizo taasisi tano.
Binafsi ninaamini ni lazima chombo kitakachoandika katiba kiwe kinawakilisha jamii yetu nzima (must represent the cross-section of our society).
Je, wakulima na maskini wanawakilishwa vipi? Je, makundi madogo (minority groups) wanawakilishwa vipi?
Tusije kugeuza mchakato wa katiba kuwa mchakato wa watu ambao tayari wana kiu ya madaraka na wameonja madaraka wakatutengenezea kitu cha kuzidi kuwapa wao madaraka ya kuwatawala wengine.
Hivyo basi, hata kama nisingeingia ndani na kuvichambua vipengele vyote vya mswada huo, naweza kusema kwa uhakika wa dhamira yangu kuwa ni miongoni mwa miswada mingine mibovu ambayo inaandikwa na watu ambao tunaamini wana akili timamu, na wasomi.
Na kama hawa ndio ambao watakuja kutuandikia katiba mpya, basi tunajitumbukiza wenyewe kwenye shimo ambalo tunajua hatuwezi kutoka.
Lakini kubwa zaidi ni kwamba kwa vile CCM haijawahi kuwa na ajenda ya katiba mpya na sasa inaonekana wamekusudia kabisa kuliburuza taifa zima kama mtu huru, nakataa kuburuzwa hivyo na binafsi ninaukataa mchakato huu unaoongozwa na chama hicho kwa misingi ya geresha ya kisiasa.
Nakataa mara moja na daima mchakato mzima ambao unapendekezwa na mswada huu, na ni matumaini yangu wengine nao wataukataa hivyo hivyo.
Kama CCM haiwezi kubuni mfumo bora wa kusimamia mchakato wa katiba mpya na badala yake kuturudishia kitu kile kile ambacho tumekikataa miezi michache iliyopita, ni jukumu letu kukataa siyo tu kuunga mkono mchakato huu bali pia kushiriki endapo utapitishwa - na uwezekano wa kupita ni mkubwa kwani wao ni wengi, rais wao na vyombo vyote vyao.
Ninachoweza kusema ni kwamba kama CCM na serikali yake watalazimisha kutulisha katiba mpya kwa nguvu, ni wajibu wetu kukataa kushiriki kwenye mijadala yao na kwa hakika kwenye kura ya maoni watakayoitisha.
Kama tumeweza kusubiri miaka 20, nina uhakika tunaweza kusubiri miaka mingine mitano kwani tunajua ni kina nani kweli walipigania katiba mpya. Wanaotaka katiba mpya ya CCM waendelee na mchakato wao, wanaotaka katiba mpya kwa ajili ya Watanzania wote wasubiri wakati wao. Kwani miaka minne iliyobakia si mingi.

Hili ni bango la tangazo au ni kitu gani manake anayelileta amekuwa bubu na halionyeshi kama yeye ndiye kaliandika; wala hasemi bango ni la mwaka gani maanake linaongelea miaka minne bado ipo hadi uchaguzi mkuu jambo linaloitengua kiuno hoja nzima, mambo ya kukopi na kupest at leat kuwepo na executive summary.
 
Naunga mkono hoja sisi katika ccm hatuna dhamira ya dhati ya kuleta katiba mpya! Ndo maana hata mabaraza ya katiba ya wilaya tumejaza wanachama wetu tu! Kama kweli watanzania wanataka katiba mpya, basi watasubiri sana!
 
Bahati mbaya watu wengi nchini mwetu hawapendi kuifikirisha akili yao kwa kiwango ambacho Mwenyezi Mungu aliwajaalia ufikiri..Siku zote wao ni 'Ndiyo Mzee' . Wao wanaona katika akiandika Rais na CCM yake ni Demokrasia! CCM imedidimisha uchumi wa nchi Je katiba ndo itakuwa Bora?
 
unafiki mtupu,mwanzoni mlipiga kelelekatiba mpya! katiba mpya!inaelekea kupatikana mnaanza viojana huo ndo msimamo wa chama chenu.Mwanzoni mligoma,baada ya juice za ikulu mkashiriki,naona mnatafuta kwenda ikulu kunywa tena juice.Angalizo wasikusahau wakienda ikulu
 
unafiki mtupu,mwanzoni mlipiga kelelekatiba mpya! katiba mpya!inaelekea kupatikana mnaanza viojana huo ndo msimamo wa chama chenu.Mwanzoni mligoma,baada ya juice za ikulu mkashiriki,naona mnatafuta kwenda
ikulu kunywa tena juice.Angalizo wasikusahau wakienda ikulu
Mbowe kaanza kunywa juisi m
K.were yupo msoga anawinda ndezi
 
Back
Top Bottom