Sababu Kubwa 2 za Kuukataa Mchakato huu wa Katiba Mpya

mi naona wacha ninoe panga langu maana vita hapa tanzania imenukia HATA MCHAKATO WA KATIBA NAO ATAAMUA MWKT WA CCM! sasa si wanasema atakayemkwaza mjumbe wa tume atachukuliwa hatua wengine hatukwazi tutafanya kweli nchi inayumba sisi tunauma uma maneno
 
Kama CCM haiwezi kubuni mfumo bora wa kusimamia mchakato wa Katiba Mpya na badala yake kuturudishia kitu kile kile ambacho tumekikataa miezi michache iliyopita ni jukumu letu kukataa siyo tu kuunga mkono mchakato huu bali pia kushiriki endapo utapitishwa - na uwezekano wa kupita ni mkubwa kwani wao ni wengi, rais wao na vyombo vyote vyao.

Ninachoweza kusema ni kwamba kama CCM na serikali yake watalazimisha kutulisha katiba mpya kama kwa nguvu. Ni wajibu wetu kukataa kushiriki kwenye mijadala yao na kwa hakika kwenye kura ya maoni watakayoitisha. Kama tumeweza kusubiri miaka 20 nina uhakika tunaweza kusubiri miaka mingine mitano kwani tunajua ni kina nani kweli walipigania Katiba Mpya. Wanaotaka Katiba Mpya ya CCM waendelee na mchakato wao, wanaotaka Katiba Mpya kwa ajili ya Watanzania wote wasubiri wakati wao. Kwani miaka minne iliyobakia si mingi.

Facebook: "Mimi Mwanakijiji"

Sijui kama watawala wetu wa sasa, waliishahsauriwa, na kama walishauriwa au wakishauriwa watakubali ushauri huu.

kwamba wakubali mapendekezo ya kuanzisha kwa katiba mpya tena bila papara na ikiwezekana kwa kuzingatia maoni yanayojenga yanayotolewa kila kona, ikiwa ni pamoja na kupunguza madaraka ya rais na kufumua na kuboresha namna ya upatikanaji wa tume ya huru uchaguzi na mengine kama hayo, maana wao kama chama tawala, ni chama cha upinzani tarajiwa

na kama uzoefu utajirudia, ni vyema wakajifunza kwa jirani zetu Kenya, waliokuwa wanapigania katiba mpya na kwamba ingekuwepo ndani ya siku 100, walipopanda madarakani walitaka wapewe muda na kutupilia mbali baadhi ya mapendekezo ambayo yangewaathili wale waliokuwa na nafasi ya kuyapitisha kabla ya kufanywa wapinzani..

nani ajuaye, leo unamrundikia na hutaki kuzungumzia madaraka maradufu ya serikali, kesho akitoka chama kingine na kwa bahati mbaya akagoma kubadili katiba (maana ndiyo walivyo wanasiasa) utajuta kuzaliwa! maana jera sasa itakuwa jirani bora wanaojitakia

Chonde chonde CCM tupe katiba maana nyine ndo mnaweza kufaidika na katiba mpya mkianguswa uchaguzi ujao, vinginevyo mkiendelea kuchelewesha kwa kutaka kutiliana ngumu na wanaharakati, kinaweza kuingia chama kikachelewa kutupa katiba maana kinaweza kudai kuwa na shughuli nyingi za kujenga utawala mpya
 
Hivi hawa watu wanafikiria hatujui ni kitu gani tunakikataa? Tunakataa mchakato wao wa CCM wa kuandika Katiba ya TAifa letu. Hili siyo jambo gumu sana kulifikiria.
 
""""Ninachoweza kusema ni kwamba kama CCM na serikali yake watalazimisha kutulisha katiba mpya kama kwa nguvu. Ni wajibu wetu kukataa kushiriki kwenye mijadala yao na kwa hakika kwenye kura ya maoni watakayoitisha. Kama tumeweza kusubiri miaka 20 nina uhakika tunaweza kusubiri miaka mingine mitano kwani tunajua ni kina nani kweli walipigania Katiba Mpya. Wanaotaka Katiba Mpya ya CCM waendelee na mchakato wao, wanaotaka Katiba Mpya kwa ajili ya Watanzania wote wasubiri wakati wao. Kwani miaka minne iliyobakia si mingi""""".

subira yavuta heri. kwa ninyi mlio utumwani na mnaoijua tanzania kupitia magazeti(biased tabloids) na blogs!! sio ajabu mkisema hivyo kwani mnachokiona kila cku ni habari za ARUSHA,MWANZA,MBEYA na miji mingine na mwisho mnadhani hiyo ndio hali halisi hadi vijijini. kaka Tanzania ni kubwa kupita kiasi na kama hujapata nafasi ya kuitembea huna haki ya kuongea kuhusu nini chaguo la watu. karibu tz uje utembee na upate hali halisi ya nchi ilivyo kisiasa.
hizo propaganda zenu ili mje mseme watu wamechakachua hazina maana.nashukuru analysis yako juu ya mapungufu yaliyomo katika uwasilishaji wa hoja ya katiba mpya na ninakuunga mkono100% lakini tukisema tususie eti kwa vile 2015 chama chako kitashinda!!!! tutakuwa tunacheza na muda na mustakabali wetu.kama ni kukomaa tunatakiwa tukomae sasa na kama kueleweka kinatakiwa kieleweke sasa,, sasa hivi..........
2015 tuingie tukiwa na kitu kinachotuongoza ili hata porojo za kura kuchakachuliwa zisiwepo.
ama umeshasoma alama kuwa chama chako hakina nafasi 2015 na uwepo wa katiba mpya kutainyima nafasi chama chako kupiga kelele za kuibiwa???????
msicheze na akili za waTZ kwa kujenga mazingira ya future conflicts

Sasa, kwa mtu yeyote ambaye amewahi kupita kwenye majengo ya shule anaweza kukiona kitu kimoja kilicho wazi sana - mchakato wa Katiba Mpya unamhitaji Rais ili kufanikiwa na kuwa halali. Lakini siyo kumhitaji Rais tu bali kumfanya Rais kuwa ndiye kiini cha mchakato mzima. Naweza kusema kwa ujasiri wa ukweli mchakato unaopendekezwa ukikubaliwa utamfanya Rais kuwa ndiye mwanzo na mwisho wa mchakato wa kuandika Katiba mpya na siyo wananchi.
MIMI PIA nafikiri sawa nawe
 
Katiba ni mali ya Watanzania na si kikundi cha wachache wanaojidai kuwakilisha Watanzania. Lakini, katiba hii haiwezi kupatikana bila shinikizo la Watanzania.
 
Mchakato huu unamfanya rais awe Kingkwete yaani Mfalme Kikwete.

KWAKO MWANAKIJIJI,
Kwanza Hongera kwa mawazo mazuri pili unaonaje endapo tukimpatia Rais power ya kuunda tume ya katiba lakini wajumbe wote ambao watateuliwa na Rais wapigiwe kura kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge la katiba lenye uwiano sawa wa wabunge kutoka CCM na Upinzani.
wajumbe hao mara baada ya kupitishwa let say na asilimia 60% ya bunge hilo basi wawe na mamlaka kamili bila ya kuingiliwa na Rais tena
katika kuitisha mkutano mkubwa wa katiba utakaokuwa na uwakilishi wa makundi mbali mbali ya kijamii kwa ajili ya kuandaa hadiju za rejea na kutokea hapo tume ishughulikie mchakato mzima wa katiba mpaka kusimamia kura ya maoni na kama ikipita basi wanachokifanya ni kuikabidhi tu kwa rais kama ni katiba mpya. ningependa sana kusikia kutoka kwako kuhusiana na wazo hili.
 
Kinachonishangaza mimi ni kwamba CCM hawakuwa na maono ya kuandika katiba mpya wala haikuwemo kwenye ilani yao, kuna watu tulipigwa mabomu katika maandamano ya kudai katiba mpya.Sasa najiuliza, ni kwanini wanakuwa kimbelembele kutaka mchakato uende haraka bila kujali sauti za watu?
 
Jaman nawashaur muingie msituni mkashike bunduki kama libya ili muweke katiba itakayo wafurahsha nyie asilimia miamoja , kwan nijuavyo mimi katiba haiwez furahsha watu wote ni asilimia 66 tu kwa hiyo nyie mpo kwenye hao 34, wengine tupo kwenye 66., hata misri katiba yao imepingwa , kwa hiyo achen kuamin kujiona eti mna fikra kubwa , na mnajua kuandika kwan hiyo ni kaz yenu ya uandish maneno mengi !
 
Hongera Mzee Mwnakijiji kwa uchambuzi mzuri. You are spot on. Mchakato wa kuandika katiba mpya unaosimamiwa na chama cha siasa na ambao unakipa chama kimoja cha siasa wawakilishi wengi kupindukia ni batili. CDM walikosea walipokubali huu mchakato, ila ni vizuri kwamba sasa wamegundua walivyohadaiwa na wanataka kujitoa.

Inastaajabisha kuona kwamba msomi kama Prof Baregu anadhani ni utaifa kuendelea kuweko kwenye mchakato huu. Ni muhimu afukuzwe CDM kabla hajaharibu zaidi.

Lazima tuanze upya. Haiwezekani kwa misingi ya sasa kupata katiba ya kidemokrasia.
 
Bora hata huo mswaada ungetoa madaraka makubwa kwa RAISI tu! Kuliko balaa hii tuliyonayo ya kutoa madaraka hayo makubwa kwa M/kiti wa chama cha siasa.Tukumbuke Mh.Raisi baada ya kukutana IKULU na wadau wazalendo na kushauriana nae walikubaliana kufanya marekebisho makubwa na muhimu ktk vipengele hv vyote tunavyolalamikia leo tena ktk awamu tatu(watafute wadau wazalendo waliokakutana nae watakuambia kiundani),Hii inaonyesha haya mapungufu mh.Raisi anayajua na ndio maana aliahidi kuyafanyia kazi(rejea hotuba yake iliyoitoa baada ya kukutana na kukubaliana na wadau wazalendo).Hivyo kwa uwezo wangu mimi wa kufikiri unanionyesha kuwa tatizo hapa si mh.RAISI bali chanzo cha matatizo haya ni M/kiti wa chama cha siasa Taifa.CCM kupitia mwenyekiti wao taifa wameamua kwa makusudi kupuuza makubaliano na muhafaka uliokafikiwa kwenye vikao halali tena vilivyofanyikia sehemu takatifu kati ya mh.RAISI na WADAU WAZALENDO,Siamini kama makubaliano yale mara baada ya kumfikia m/kiti wa ccm taifa na kuyatafakari hakuona tija yake kwa taifa ila ninachoamini ni wajumbe wa chama chake ndo wamemuangusha.Sitaki kuamini kuwa aliogopa kunyang'anywa kadi ya chama endapo asingekubaliana na matakwa ya wajumbe wa kamati kuu ya chama chake kwani kikatiba tungelazimika kufanya uchaguzi mkuu tena na si mara ya kwanza ikumbukwe hata ile sheria yenyewe alilazimika kusaini mswaada wake pamoja na mapungufu yaliyomo kuhofia endapo angekataa tena bunge lingevunjwa na kulazimika kuitishwa uchaguzi wa wabunge.Wakuu mie ndg yenu leo naomba niseme kitu kimoja cha msingi sana ktk taifa letu kwa hapa tulipofikia hv sasa tutake tusitake na tuamini tusiamini lkn ukweli ni kwamba Kikao kibaya na chenye maamuzi yasiyo na tija kwa taifa ni kile kinachoongozwa na M/kiti wa wabunge wa CCM kule dodoma mara zinapohairishwa shughuli za bunge.Mi namuomba mh.Raisi asimamie anachokiamini kwani na kama anavyotuhasa mara kwa mara AKILI ZA KUMBIWA CHANGANYA NA ZAKO,Hivyo basi tafsiri isiyo rasmi ni akili za kwako ni zile zilizokapitisha makubaliano kule IKULU na zakuambiwa ni hizi zinazotoka kwenye kikao cha wabunge wa chama chako kule Dodoma.
 
Baada ya katiba kupatikana maccm yatapitia ujumbe wako huu na kuangalia wapi walijikwaa.
 
""""Ninachoweza kusema ni kwamba kama CCM na serikali yake watalazimisha kutulisha katiba mpya kama kwa nguvu. Ni wajibu wetu kukataa kushiriki kwenye mijadala yao na kwa hakika kwenye kura ya maoni watakayoitisha. Kama tumeweza kusubiri miaka 20 nina uhakika tunaweza kusubiri miaka mingine mitano kwani tunajua ni kina nani kweli walipigania Katiba Mpya. Wanaotaka Katiba Mpya ya CCM waendelee na mchakato wao, wanaotaka Katiba Mpya kwa ajili ya Watanzania wote wasubiri wakati wao. Kwani miaka minne iliyobakia si mingi""""".

subira yavuta heri. kwa ninyi mlio utumwani na mnaoijua tanzania kupitia magazeti(biased tabloids) na blogs!! sio ajabu mkisema hivyo kwani mnachokiona kila cku ni habari za ARUSHA,MWANZA,MBEYA na miji mingine na mwisho mnadhani hiyo ndio hali halisi hadi vijijini. kaka Tanzania ni kubwa kupita kiasi na kama hujapata nafasi ya kuitembea huna haki ya kuongea kuhusu nini chaguo la watu. karibu tz uje utembee na upate hali halisi ya nchi ilivyo kisiasa.
hizo propaganda zenu ili mje mseme watu wamechakachua hazina maana.nashukuru analysis yako juu ya mapungufu yaliyomo katika uwasilishaji wa hoja ya katiba mpya na ninakuunga mkono100% lakini tukisema tususie eti kwa vile 2015 chama chako kitashinda!!!! tutakuwa tunacheza na muda na mustakabali wetu.kama ni kukomaa tunatakiwa tukomae sasa na kama kueleweka kinatakiwa kieleweke sasa,, sasa hivi..........
2015 tuingie tukiwa na kitu kinachotuongoza ili hata porojo za kura kuchakachuliwa zisiwepo.
ama umeshasoma alama kuwa chama chako hakina nafasi 2015 na uwepo wa katiba mpya kutainyima nafasi chama chako kupiga kelele za kuibiwa???????
msicheze na akili za waTZ kwa kujenga mazingira ya future conflicts

Hivi ww unaona kwa kuandika haya ndo una uchungu na watanzania? Ww ni mpuuzi na ccm yako nyie ndo mnataka kucheza na akili za watanzania tena siwapendi siwapendi
 
Hivi ww unaona kwa kuandika haya ndo una uchungu na watanzania? Ww ni mpuuzi na ccm yako nyie ndo mnataka kucheza na akili za watanzania tena siwapendi siwapendi
ndugu kumbe unaongozwa na chuki... humu tunatanguliza taifa kwanza.. anaefikiria tofauti na wewe huna haja ya kumchukia, jaribu kumshawishi kwa hoja. tupo katika mti mmoja ila matawi tofauti. tujaribu kuutunza mti wetu kwani siku shina la huu mti likianguka hakuna tawi litakalosalimika. BY THAT TIME!!! MWANAKIJIJI NA mamluki wengine hawatakuwepo
 
Back
Top Bottom