Sababu iliyonifanya nihamishe chaneli ya TV

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,462
154,333
Juzi kwenye hivi vipindi vya TV ambavyo wadada wameshika hatamu kutangaza, na huwa wanawauliza watu mambo mengi tu nilisikia kali. Mdada alikuwa kamkaribisha daktari wa hospitali wa wagonjwa wa akili, ambaye alielezea kuwa mtu anaweza akaonekana mzima kabisa , lakini ukimuuliza maswali fulani rahisi ukaweza kujua kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili;
MDADA: Daktari unaweza kutufahamisha ni maswali aina gani?
DAKTARI: Kwa mfano naweza kumuuliza mgonjwa swali la kihistoria kwa mfano nikasema,'Dr Livingstone alifanya safari tatu kwenda Ujiji na ndipo kifo kikamkuta, sasa je nika katika safari ya ngapi alipofariki?'
MDADA: (kwanza alicheka kidogo) Watazamaji hayo ndio aina ya maswali ya dokta, mi kwakweli sikuwa mzuri sana kwa historia wakati niko shule, sina jibu ila nategemea watazamaji kuna wengi mmekwishapata jibu....sasa dokta huwa hamna maswali rahisi yanayohusu jamii tuliyonayo leo? (....nikahamisha chaneli)
 
Mambo ya kuwekana makazini kimjombamjomba ndio hayo matatizo yake ka uyo mtangazaj
 
Huyo Dokta ndo ana matatizo ya akili...hilo swali kweli ni swali la kupima kama mtu ni mzima au laaa!!!!
 
hilo swali halihitaji uwe umesoma historia ni swali linalohitaji ufahamu wako wa kuchambua mambo haraka. kama Dr livingston alifanya safari tatu kabla ya kifo chake, inamaana alifariki katika safari ya tatu. asinge weza kufanya safari ya tatu kama angekuwa amefariki katika safari ya kwanza au ya pili. Ndiomaana maswali kama haya wanaulizwa watu wanaohisiwa kuwa wanamatatizo ya akili, nimaswali yanayohitaji ufahamu na akili iliyo timamu na wala hayahitaji elimu kuweza kujibu.
 
umetoa jibu mapema sana ungetuliatulia tuwapate wagonjwa wa akil humu jf
 
haya ndiyo matatizo ya shule za kisasa,watoto wanachukiliwa na school bus saa 12 asubuhi,wanazunguka kupitia wengine mpaka saa 2,ni ngumu kuwa na ufahaumu.
 
Dah. Sijacheka tangu asubuh, ila jibu la mtangazaji limeniacha hoi. Wana jf huu si utani ndo ukweli wa mambo. Kizazi cha leo ni wavivu kufikiria.
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom