SABABU GANI ZINAWASHAWISHI WATU KUKWEPA KODI

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,465
Tatizo la ukwepaji kulipa kodi ni kubwa mno kuliko linavyosimuliwa na watendaji wa serikali pamoja na Raisi mwenyewe.

Je ni sababu gani zinawafanya raia, wafanyabiashra, wanasiasa, watawala na wageni wanataka kukwepa au wanakwepa kodi kwa hali yeyote ile ?

Je ni
Kodi nyingi
Kubwa kupita kiasi
mfumo usioeleweka
hazilindi maslahi mapana ya jamaa

au ni hali kupenda tu kukwepa kodi?
 
Tanzania ni nchi pekee katika ukanda wa afrika mashariki ambayo kodi yake ni kubwa mno na haiko formulated sababu unaweza kua na mzigo wa thamani 5000 usd basi ukalipa kodi mara tatu yake ya thamani ya mzigo
 
Ni mfumo unatowa mwanya wa rushwa. Kuna makampuni au watu wanataka kulipa kodi kutokana na mauzo lakini wafanyakazi wa TRA wanaongeza makadirio ya kodi ili muhusika atowe rushwa AU unaleta gari, unaonyesha receipts lakini wao wanakupa bei zao sijui wanazitowa wapi mnaanza negotiate thamani ya gari hii inasababisha watu kutoa rushwa.
 
PAMOJA NA MZIGO MKUBWA WA KODI TUNAZOLIPA LAKINI BADO HATUONI MANUFAA YA KULIPA HIYO....KWANI NYINGI ZINAISHIA KWENYE MATUMBO YA MABWANYENYE KWA KUPITIA MISHAHARA MIKUBWA ISIYOLINGANA NA UTENDAJI WAO.....POSHO KWENYE SEMINA ZISIZO NA TIJA.....NA BILA KUSAHAU MIRADI HEWA ISIYOKAMILIKA......

NITAPATAJE MZUKA WA KULIPA KODI WAKATI HUDUMA ZOTE KIJAMII AMBAZO ZINGETAKIWA NIZIPATE BURE KUPITIA KODI YANGU BADO NATOZWA HELA.......NCHI YETU INA MSURURU MKUBWA SANA WA KODI AMBAZO KAMA ZINGEKUWA NA USIMAMIZI MZURI BASI TUNGEKUWA MBALI SANA KAMA TAIFA....

KWA HALI ILIVYO SASA HAISHANGAZI KUONA MTANZANIA HATA ANADIRIKI KUMSAIDIA MGENI KUKWEPA KODI ,JAMBO AMBALO NI NADRA SANA KAMA SIO HAKUNA KABISA KWA MATAIFA MENGINE YENYE KUWAJALI WANANCHI WAO........
 
Back
Top Bottom