Sababu alizozitoa Rais Samia kuhusu kubadilisha Baraza la Mawaziri, hazikuwa za kweli?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Tulimsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan, wakati alipotuahidi kuwa atafanya mabadiliko ya Baraza la mawaziri na kusema wazi kuwa amegundua kuwa kuna baadhi ya mawaziri wameaanza kampeni kuwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025 na akaendelea kusisitiza kuwa hao mawaziri atawaweka pembeni, wakati atakapotangazali Baraza lake jipya la mawaziri Ili wakajitayarishe vivuri zaidi kwenye kampeni zao za Urais Ili wakutane kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.

Rais Samia alisisitiza kuwa anataka Baraza la mawaziri, ambao watakuwa tayari kufanya Kazi kuwa ajili ya kutumikia maendeleo ya wananchi na wala hatapenda kuwa na mawaziri ambao wameshaanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.

Hata hivyo baada ya kulitangaza Baraza lake jipya na kuwaacha baadhi ya vigogo, wananchi tukapata tafsiri kuwa walioachwa, ndiyo wale ambao Rais Samia, alituhakikishia kuwa atawaacha kwa kuwa wameaanza kampeni mapema.

Lakini wananchi tumeshikwa na butwaa, siku ya Jana baada ya Rais Samia kutwambia kuwa amewaacha akina Profesa Kabudi na William Lukuvi, kwa kuwa atawapa majukumu mengine makubwa hapo Ikulu na wala hajawaacha kwenye Baraza la mawaziri kwa kuwa wameaanza kampeni za Urais mapema kabla ya mwaka 2025!

Ndipo hapo ninapouliza, je Rais Samia alituongopea, wakati alitueleza kuwa atawaacha baadhi ya mawaziri ambao wameaanza kampeni mapema, kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa Urais wa mwaka 2025?
 
TUNA RAIS MUONGO NA ANAYE CHAFUA WATU BILA SABABU.. KMA UNATAKA KUWATOA WEWE TOA TU NA KUSEMA SABABU,, KWA HILI NAMPENDA BURE MAGUFURI KWANI ALISEMA WAZI SBB ZA KUMTUMBUA MTU KULIKO HUU UNAFIKI KUWA WANAWANIA URAIS
Hata Mimi nilishangaa Sana, kwa kuwa Rais alituaminisha kuwa atateua Baraza jipya la mawaziri, ambapo atawaweka kando wale mawaziri walioanza kampeni mapema za Urais, sasa Rais Samia baada ya kutuhakikishia kuwa kina Kabudi na Lukuvi hawamo kwenye mbio hizo za Urais na atawapa majukumu maalum pale Ikulu, anataka kutwambia kuwa Kitila Mkumbo na Waitara ndiyo ambao wameanza kampeni za Urais mapema?
 
Mara Wanataka URAIS Mara WAZEE ,Mara Nataka Wanisaidie

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Mama anatulazimisha hata sisi tunaomshabikia tuanze kumwona kigeugeu.

Hata spika angetulia... tatizo chawa walidandia mipasho ya mama bila kutafakari kwa kina.
 
Hata Mimi nilishangaa Sana, kwa kuwa Rais alituaminisha kuwa atateua Baraza jipya la mawaziri, ambapo atawaweka kando wale mawaziri walioanza kampeni mapema za Urais, sasa Rais Samia baada ya kutuhakikishia kuwa kina Kabudi na Lukuvi hawamo kwenye mbio hizo za Urais na atawapa majukumu maalum pale Ikulu, anataka kutwambia kuwa Kitila Mkumbo na Waitara ndiyo ambao wameanza kampeni za Urais mapema?
Awamu hii tumepigwa.
 
Back
Top Bottom