Uchaguzi 2020 Sababu 7 zinazomtofautisha mpiga kura wa keshokutwa na miaka ya nyuma

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,569
15,306
Pamoja na ukweli kuwa uchaguzi huu ni wa Rais, Wabunge na Madiwani ila ni ukweli usiokificho uchaguzi huu umehamia kwa Dr Magufuli Vs T. Lissu, umerudi kwa Maalim Sief VS Dr Mwinyi.

Kwa kuzingatia hayo na kwa muono wangu hizi ni tofauti saba zinazomtofautisha mpiga kura huyu wa keshokutwa na wengine waliopita.

1: Huyu ni Msiri. Bila kujali chama hujui atampigia ndani hadi aipige hiyo kura. Kwa hali iliyopita ambayo wengi waliogopa kujionyesha waziwazi wanapenda nini kutoka na matukio ya wasiojulikana yaliyolenga sana watu wenye milengo ya kisiasa.

2: Huyu anataarifa nyingi. Asipohudhuria mkutanoni kwenye makonga anafuatilia YouTube, shortclips za WhatsApp, JF ,Twitter na hata Telegram.

3: Huyu anaweza kubadili maamuzi hata dakika ya majeruhi bila kujali alipanga kumpigia kura Dr Magufuli au Mwanasheria Lissu. Kwa maporomoko ya taarifa motomoto za kusisimua mitandaoni zinazoonyesha udhaifu wa upande mmoja kama zikiendelea kushushwa zinanguvu ya kutikisa maamuzi ya mpiga kura Kabla ya asubuhi ya kupinga kura. Na huu ndio udhaifu wa kudhani eti kuwa mwanaCCM basi automatically utampigia mgombea wa CCM na Otherwise.

4: Utekelezwaji wa Maagizo ya Mgombea wa CCM wakati huu wa kampeni. Mfano jumbo flani aliagiza hadi kufikia siku flani jambo flani liwe limetendeka na Muda huu ninapoandika wako watu wanatekeleza tena kwa spidi. Tukio hili ni muujiza kwa wakazi wa maeneo haya na limekuwa game changer japo linaweza kutafsirika kama unfair greasing tip.

5: Walimu ambao wengi ni kama hawajafurahishwa kiuchumi na kimshahara awamu hii, ukizingatia walipewa ahadi ya kumiliki laptop ambao hawana ndio wengi wanasimamia pia uchaguzi. Ikiwa watafanya zoezi hili kwa manungunika na bila ukaribu wa tume wanaweza pia kushawishiana matokeo. Sio hawa tu na wengine ambao wengi ni Vijana wasio na ajira na hawajui watazipataje na hawaoni mpango mkakati wa wazi kuja kupata. Wanaweza kubadili upepo huko jikoni.

6: Watu wengi waliohamia CCM kwa Sababu ya Upinzani kunajisika na ingizo la Lowasa 2015 na baadaye kuwatelekeza na kurudi CCM. Hii inajumuisha na wengi waliorudi CCM hapo katikati kwa ubora wa mwenyekiti na wengine wamelalamikiwa kuwa sio Hiyari yao. Alichokifanya Lissu kwa Muda mfupi kimerudisha vuguvugu la upinzani wa ukweli. Wenda wakatamani kurudi upinzani kwa njia ya kura huku sura na viwiliwili vikiwa CCM.

7: Kete ya Janga la Corona. Kipindi kile Rais aligeuka kuwa Baba wa Kiroho wa taifa. Nakumbuka kanisa moja nilisali Mchungaji alikosolilewa vikali na kupuuzwa huku rais aigeuka kuwa role model wa kiroho wa kanisa. Kete hii inaweza kuathiliwa kwa historia kuwa wengi wetu ni wazito kuelewa na wepesi kusahau. Ingekuwa na nguvu zaidi kama Maombi yakiondoa korona wakati imefikia hatua aliyotabiri Melinda Gates kuwa "Nikaona maiti zikizagaa mabarabarani Afrika". Wengine waliamini tu sisi Afrika ni ngangari hatufi kirahisi hata sasa huyo mdudu yupo lkn anakibiliwa vilivyo na CD4 Nyeusi. ILa hili nalo litashawishi mpiga kura wa keshokutwa.
 
Back
Top Bottom