SABABU 7 ZA KWA NINI HUTAKIWI KUTAFUTA MPENZI KWENYE MTANDAO WA INTANET

Chrix_Tz

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
880
1,098
1. Watu wanaigiza uhalisia
Katika eneo ambalo watu wanaigiza uhalisia wa maisha kwa kiasi kikubwa ni kwenye mitandao ya kutafuta wapenzi pamoja na mitandao ya kijamii.

Watu huweka picha ambazo siyo zao, majina ya uongo, maelezo binafsi ya uongo, hali za mahusiano za uongo, eneo la makazi la uongo, n.k.

2. Ni biashara
Mitandao mingi ya kutafuta wapenzi imeanzishwa kwa lengo la kibiashara. Hivyo uhalisia wa kupata mpenzi sahihi ni mdogo kwani suala la kutafuta wapenzi hutumiwa kama njia ya kupata pesa.

Kwa mfano unaweza kuanza mahusiano na mtu kumbe analipwa pesa afanye hivyo ili mfumo uzidi kupata wanachama au watembeleaji zaidi na hatimae kuzalisha pesa zaidi.

3. Umbali
Lengo mojawapo la mahusiano ni watu wawili kukaa pamoja kwa karibu zaidi ili washirikishane hisia zao. Hivyo kwa kiasi kikubwa umbali unaweza kuathiri mahusiano.

4. Hakuna mapenzi ya kweli
Mara nyingi watu wengi wanaojiunga na mitandao ya kutafuta wapenzi ni watu wanaojaribu mifumo hiyo au watoto.

Hivyo ni vigumu sana kupata mtu mwenye nia ya dhati ya kujenga mahusiano bora ambayo hatimaye yanaweza kufikia ndoa.

Kumbuka pia kwa kuwa tovuti za kutafuta wapenzi ni nyingi, ni rahisi mtu kuvunja mahusiano kwani atapata mpenzi mwingine ndani ya muda mfupi.

5. Watu wengi wamejeruhiwa
Majeraha ya mahusiano huharibu mahusiano ya watu wengi. Tafiti mbalimbali zilibaini kuwa watu wengi wanapojeruhiwa au kukosana na wapenzi wao hukimbilia kwenye mitandao ya kutafuta wapenzi.

Hebu fikiri unaanza mahusiano na mtu mwenye majeraha na uchungu wa mahusiano yaliyopita; ni wazi hamtoweza kujenga mahusiano yatakayodumu.

6. Kudanganyana ni rahisi zaidi
Je umewahi kusikia mtu akipiga simu akiwa kwenye daladala Dar es Salaam lakini anasema yuko Mwanza? Haya ndiyo mambo yanayotawala mitandao ya kutafuta wapenzi.

Kwa kuwa humwoni mtu unayewasiliana naye, ni rahisi kukudanganya kwenye mambo mengi. Anaweza kuwa anawasiliana na wapenzi sita kwa wakati mmoja lakini hutoweza kubaini.

7. Unaweza kufanyiwa uhalifu
Unapoingia kwenye mahusiano na mtu kwa kupitia mitandao ya kutafuta wapenzi mnaweza kubadilishana taarifa kadhaa. Ikiwa utatoa taarifa zako muhimu kama vile pasi ya kusafiria, kadi za benki, n.k. taarifa hizo zinaweza kutumiwa na wahalifu kukufanyia uhalifu.

NENO LA MWISHO

Kwa hakika wahenga waliposema si kila king’aacho ni dhahabu hawakukosea kitu. Ni muhimu sana kuchunguza vitu vinavyoletwa na wimbi la teknolojia ili kuona ubora, usalama na uhalisia wake.

Unaweza kujitumbukiza kwenye matatizo makubwa yanayoweza hata kugharimu uhai wako kwa kuingia kwenye mahusiano na mtu usiyemfahamu vizuri kwenye mtandao. Hivyo kuwa makini na chukua tahadhari mapema.
NIWATAKIE IJUMAA NJEMA.
kud_online-768x509.jpeg
 
Kwani wakiwasiliana wanaoana hapo hapo au wanaanza kufahamiana Mdogo Mdogo
Au mkikutana mtaani ndo Kama ni mbaya hawezi kukudanganya?
Mana tabia ni za MTU wala sio mtandao..mtandaoni ni Kama kurahisisha tu..
 
Kama haturuhusiwi kutafta mwanamke kwenye mtandao wa internet, je tunaruhusiwa kutafta wanawake kwenye mtandao wa website?
 
Kwani wakiwasiliana wanaoana hapo hapo au wanaanza kufahamiana Mdogo Mdogo
Au mkikutana mtaani ndo Kama ni mbaya hawezi kukudanganya?
Mana tabia ni za MTU wala sio mtandao..mtandaoni ni Kama kurahisisha tu..
Lakini madhara niliyoyazungumzia hapo ukiyaelewa vema huwezi fananisha na yule mtu ambae ni mtu alisia weng kwenye mtandao wamekua waongo sana unakuta mtu unakutumia hata picha ambayo si yake au anafake life wakat ktk hali ya kawaida kwa mtu unaemjua hata akifake ni simple kumgundua mkuu..
 
1. Watu wanaigiza uhalisia
Katika eneo ambalo watu wanaigiza uhalisia wa maisha kwa kiasi kikubwa ni kwenye mitandao ya kutafuta wapenzi pamoja na mitandao ya kijamii.

Watu huweka picha ambazo siyo zao, majina ya uongo, maelezo binafsi ya uongo, hali za mahusiano za uongo, eneo la makazi la uongo, n.k.

2. Ni biashara
Mitandao mingi ya kutafuta wapenzi imeanzishwa kwa lengo la kibiashara. Hivyo uhalisia wa kupata mpenzi sahihi ni mdogo kwani suala la kutafuta wapenzi hutumiwa kama njia ya kupata pesa.

Kwa mfano unaweza kuanza mahusiano na mtu kumbe analipwa pesa afanye hivyo ili mfumo uzidi kupata wanachama au watembeleaji zaidi na hatimae kuzalisha pesa zaidi.

3. Umbali
Lengo mojawapo la mahusiano ni watu wawili kukaa pamoja kwa karibu zaidi ili washirikishane hisia zao. Hivyo kwa kiasi kikubwa umbali unaweza kuathiri mahusiano.

4. Hakuna mapenzi ya kweli
Mara nyingi watu wengi wanaojiunga na mitandao ya kutafuta wapenzi ni watu wanaojaribu mifumo hiyo au watoto.

Hivyo ni vigumu sana kupata mtu mwenye nia ya dhati ya kujenga mahusiano bora ambayo hatimaye yanaweza kufikia ndoa.

Kumbuka pia kwa kuwa tovuti za kutafuta wapenzi ni nyingi, ni rahisi mtu kuvunja mahusiano kwani atapata mpenzi mwingine ndani ya muda mfupi.

5. Watu wengi wamejeruhiwa
Majeraha ya mahusiano huharibu mahusiano ya watu wengi. Tafiti mbalimbali zilibaini kuwa watu wengi wanapojeruhiwa au kukosana na wapenzi wao hukimbilia kwenye mitandao ya kutafuta wapenzi.

Hebu fikiri unaanza mahusiano na mtu mwenye majeraha na uchungu wa mahusiano yaliyopita; ni wazi hamtoweza kujenga mahusiano yatakayodumu.

6. Kudanganyana ni rahisi zaidi
Je umewahi kusikia mtu akipiga simu akiwa kwenye daladala Dar es Salaam lakini anasema yuko Mwanza? Haya ndiyo mambo yanayotawala mitandao ya kutafuta wapenzi.

Kwa kuwa humwoni mtu unayewasiliana naye, ni rahisi kukudanganya kwenye mambo mengi. Anaweza kuwa anawasiliana na wapenzi sita kwa wakati mmoja lakini hutoweza kubaini.

7. Unaweza kufanyiwa uhalifu
Unapoingia kwenye mahusiano na mtu kwa kupitia mitandao ya kutafuta wapenzi mnaweza kubadilishana taarifa kadhaa. Ikiwa utatoa taarifa zako muhimu kama vile pasi ya kusafiria, kadi za benki, n.k. taarifa hizo zinaweza kutumiwa na wahalifu kukufanyia uhalifu.

NENO LA MWISHO

Kwa hakika wahenga waliposema si kila king’aacho ni dhahabu hawakukosea kitu. Ni muhimu sana kuchunguza vitu vinavyoletwa na wimbi la teknolojia ili kuona ubora, usalama na uhalisia wake.

Unaweza kujitumbukiza kwenye matatizo makubwa yanayoweza hata kugharimu uhai wako kwa kuingia kwenye mahusiano na mtu usiyemfahamu vizuri kwenye mtandao. Hivyo kuwa makini na chukua tahadhari mapema.
NIWATAKIE IJUMAA NJEMA. View attachment 973698
Mmh! Ni changamoto kwa kweli! Basi itabidi tusitafute kwenye mitandao! Ambao hatuna wenza! Maana kumjua mkweli ni changamoto kwa kweli!
 
Japo sio wote wenye tabia hizi ila wamefunikwa kwa % kubwa na hawa wenye tabia hizi so hii ni tahadhari tu mkuu..
 
Mkuu naomba niku challenge kidogo. Hapa issue ni njia yakuwasiliana na mtu au unamaanisha nini. Utakutana na mtu kanisani lakini pia yupo mtandaoni. Mambo mengine ni kumuomba Mungu tuu
 
Mkuu siku hizi mitandao upande wa kutafuta wachumba imekua kibiashara zaidi mpk dada zetu yaan haitumiwi kama ambavyo lengo sahihi lililopo ni wachache sana ambao utakutana nao wenye userous na wenye nia pendwa..... Hivyo tuwe makini sana
 
Na kweli mpendwa
 
Back
Top Bottom