Sababu 6 zinazoonyesha wazi Thomas Tuchel ndiye anamrithi Arsene Wenger

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
965
1,691
kwanza nimeeleza kwamba sasa ni wazi Wenger anaondoka msimu huu. Kwenye post ntaonyesha dalili zinaonyesha Thomas Tuchel ndiye anachukua nafasi yake.

1. Usajiri wa Obemeyang na Mkhitarian

Si kawaida kwa Wenger kusajiri mchezaji mwenye miaka 29. Na si kawaida kabisa kwake kusajiri wachezaji wawili wenye umri huo kwa dirisha moja. Auba anakaribia miaka 29 na Miki amefikisha umri huo. Mwanzoni ilisemekana ni usajiri wa Mislintant lkn ulikuwa ushauri wa Tuchel au ulifanyika kumshawishi ajiunge na Arsenal kwa sababu alifanya nao kazi Dortmund.

2. Uthibitisho wa Bayern Munich

Bayern wamethibitisha kwamba walikuwa wanamuhitaji lakini amesaini na klabu nyingine. Matthaus akaenda mbali na kuitaja Arsenal. Si Arsenal wala Tuchel aliyekanusha madai hayo.

3. Kauli ya Steve Bould

Labda kuna watu wana wasi wasi kwamba Arsene Wenger kwa roho yake ngumu hatakubali kuachia ngazi. Wiki hii Wenger alikuwa na matatizo ya koo hivyo mkutano na waandishi wa habari alifanya msaidizi wake Steve Bould. Alipoulizwa kama Wenger atakuwepo alisema "ningependa iwe hivyo". Mtu kama Bould wa pili toka kwa Wenger angekuwa anajua boss wake atakuwepo angejibu 'definitely'.

4. Thomas Tuchel kuikataa Bayern Munich

Bayern Munich wao wenyewe wamethibitisha hilo. Wengine wanashangaa 'eti' kuikataa Bayern akaenda Arsenal. Hivi kocha mwenye miaka 44 anaenda pale kuongeza nini? Kama ni Bundesilga wanachukua kila mwaka na Champions League si kombe geni. Watu mliwahi kujiuliza kwa nini Guadiola aliondoka Barcelona na na Bayern? Unashinda kila kitu lakini watu wanaona kawaida

5. Kauli ya Ikay Gundogan

Kiungo wa Man City Gundogan ambaye alicheza chini ya Tuchel Dortmund alisema anasikia boss wake huyo anakuja Uingereza. Sidhani kama Gundogan anasikia kama sisi, anaweza kuwa ashaongea naye.

6. Ataichagua Arsenal badala ya Chelsea

Kuna fununu kwamba hata Chelsea wanamuhitaji. Kwangu mimi zaidi ya fedha sijui kama Chelsea bado inawavutia makocha wenye malengo ya muda mrefu. Chelsea wamewafukuza Mourinho, Anceloth, De Matteo na sasa wanakaribia kufanya hivyo kwa Conte mwaka mmoja baada ya kuchukua ubingwa. Binafsi huwa nadhani waliua kabisa carrier ya De Matteo. Mtu aliyewapa Champions League ktk historia ya kilabu wakati makocha wakubwa kama Mourinho, Schorali na Anceroth wamepita pale na wameshindwa hakutakiwa kutendewa vile.
images%20(2)-01.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom