Sababu 6 kwanini biashara ndogo nyingi zinakufa na nini cha kufanya

Benittotz

Member
May 24, 2018
68
122
SABABU SITA 6 KWANINI BIASHARA NDOGO NYINGI ZINAKUFA NA NINI CHA KUFANYA KUEPUKA SABABU HIZI.

Tafiti za usimamizi wa biashara zinazoonyesha kuwa nusu ya biashara zinazoanzishwa zinakufa labla ya miaka mitano, huku moja ya tatu 1/3 (theluthi) pekee zikifanikiwa kufikisha miaka kumi.
Kwa ufupi ni kwamba 50% pekee ya biashara mpya ndio hufanikiwa kuvuka miaka mitano, na kufa mwanzoni mwa miaka mitano ya pili.

Jarida la Forbes kwa msaada wa tafiti zilizofanywa na channel ya kibiashara ya Bloomberg wanasema kwamba biashara nane Kati ya kumi zinazoanzishwa hufa ndani ya miez 18 ya kwanza.

Nini chanzo Cha biashara nyingi kushindwa kutoboa ikizingatiwa ya kwamba nafasi za mafanikio ni 50/50 ikiwa Aina ya bidhaa au huduma inayotolewa inahitajika katika jamii?.

ZIFUATAZO NI BAADHI YA SABABU NA SOLUTIONS ZAKE.

1. UONGOZI MBOVU.

Ikiwa huna maarifa na ujuzi wakutosha katika kusimamia uzalishaji, utendaji kazi, na kuongoza kwa maono ya kibiashara ni wazi mafanikio ya biashara yako yapo katika mstari mwekundu.
Uongozi mbovu unaweza kukidhihirisha kwa mizozo ya Mara kwa Mara baina yako na viongozi wa team zako, ubishi baina yako na viongozi wako hadharani au viongozi kutoa maelezo yanayokinzana kwa watu mnaowaongoza.
Ni hatari Sana Kama kiongozi unapokosa uzoefu wa kufanya maamuzi. Wakati mwingine hi hupelekea kuchelewa hatua kuchukuliwa au tatizo kushughulikiwa pindi ambapo biashara inayumba. Na hivyo kuwa mwanzo wa kufa kwa biashara.

NINI KIFANYIKE.
Uongozi mbovu unayumbisha biashara, unaathiri mfumo mzima wa utendaji kuanzia kwenye usimamizi wa fedha mpka motisha ya wafanyakazi. Hivyo kuwa kikwazo katika uzalishaji na kuiweka biashara ukingoni.
Hatua stahiki hapa NI kukubali kujifunza, soma mbinu za uongozi kadri uwezavyo, hudhuria madarasa husika. Tafuta mwalimu binafsi wa biashara (mentor) , fanya tafiti binafsi na kila Aina ya mbinu katika kunyanyua uwezo wako wa kuongoza. Zichanganue mbinu zote za uongozi na Kisha chagua iliyo Bora kwa Aina yako ya biashara.

2.BIDHAA KUKOSA UTOFAUTI NA THAMANI YA PEKEE.

Wakati mwingine unaweza kuwa na bidhaa au huduma Bora inayohitajika Sana sokoni lakin bado unafanya vibaya sokoni. Huenda unakosa mbinu Bora ya kuonyesha thamani ya bidhaa yako sokoni au una washindani wengi na umeshindwa kuifanya bidhaa yako kusimama juu yao na kuonekana thamani yake hivyo kupelekea kufanya vibaya sokoni.

NINI CHA KUFANYA.

Swali la msingi la kujiuliza hapa NI kitu hapa ni kitu gani kutofautisha na wapinzani wako. Unatumia mbinu gani ambayo ni tofauti na wenzio? Washindani wako wanafanya kitu gani vizuri kushinda wewe? Baada ya kuyajua haya boresha biashara yako. Tengeneza mfumo na package (kifurushi) Cha huduma ambayo Hakuna mwingine anaitoa katika soko kiasi kwamba itachukua umakini wa wateja na kuwafanya waipende huduma au bidhaa yako.

Hivi ndivyo ukatengeneza chapa (brand) yako. Chapa yako ndio hutoa taswira ya huduma yako kwa mteja na mteja huitumia chapa hiyo kuohusianisha na biashara yako.
Utambulisho wa chapa yako ikiwa ni pamoja na logo, Rangi, kauli mbiu au tagline na vitu vingine vyote vinavyoonekana pamoja na Sera na philosophy ya biashara yako lazima viiwakilishe thamani ya bidhaa au huduma unayotoa na kukutenganisha wewe binafsi na bidhaa yako.

Ili kuifanya chapa yako ifahamike lazima utumie mbinu nyingi za masoko ikiwa ni pamoja na mbinu ngumu pia. Usiogope kusimama kwenye matukio ya kijasirimali kuongea au kuweka vipeperushi vyako, pigia watu simu, tuma email, ongea na watu bila kusahau nguvu ya mitandao ya kijamii.


3. KUTOKUA NA MAWASILIANO MAZURI NA WATEJA NA KUJUA MAHITAJI YAO.

Kama utapuuza wanachosema wateja au kutokua na ukaribu nao, ni dhahiri kuwa biashara yako itakufa. Inashauriwa kuwa karibu na wateja na kuyaelewa mahitaji na mrejesho wanaokupatia.
Wateja wanaweza kuwa wanaipenda bidhaa au huduma unayoitoa lakini wangeipenda zaidi Kama kitu fulani kingepunguzwa au kuongezwa.
Unakisikia wanachojaribu kusema? Bado wanapenda unachowauzia? soko lako linashuka? Haya ni maswali muhimu ya kujiuliza sababu huenda kweli unauza bidhaa iliyo nje ya soko kwa wakati husika.

NINI KIFANYIKE
Mfanyabiashara aliefanikiwa huweka mkazo katika bidhaa iliyoko sokoni kujua wateja wa muhimu na wanavutiwa vipi na bidhaa au huduma hiyo. Tengeneza njia Bora ya usimamizi wa mahusiano na wateja (CRM, CUSTOMER RELATIONSHIP MANAGEMENT).

4.MFUMO WA BIASHARA USIO NA FAIDA.
Moja Kati ya viashiria vikubwa vya kuanguka kwa biashara ni kuwa na mfumo ambao si thabiti, kuendesha biashara Bila mpango wa kazi, na kukomaa na biashara ambayo njia zake za mapato i si za uhakika.
Wazo la biashara linaweza kuwa zuri lakini kutokuwa na mikakati ya uongozi kukapelekea anguko la biashara hiyo.

NINI KIFANYIKE.
Fanya tafiti na rejea ni namna gani biashara zingine zinafanya kazi sokoni. Kisha tengeneza mfumo kamili wa mpango wa biashara ambao unahusisha makadirio ya mapato yanayotegemewa, mikakati ya masoko na ufumbuzi wa changamoto za usimamizi katika kuvivuka vikwazo muhimu vya masoko na wapinzani.
Andaa jedwali linaloonyesha kazi husika na malengo yaliyoambatanishwa na ukomo wa muda. Ili kuweza kuyapima mafanikio,kutatua changamoto zinapojitokeza na kubaki katika njia sahihi. Mpango kazi thabiti unahusisha mbinu sahihi na unaisadia biashara yako kutoanguka.

5. USIMAMIZI MBOVU WA FEDHA.

SmallBizTrend. com inasema kuwa 40% ya biashara ndogo pekee ndio hupata faida, 30% zinapata hasara na hiyo 30% nyingine haipati faida Wala hasara (even).
Ili ufanikiwe ni lazima ujue katika biashara yako fedha inapatikana vipi na inatumika vipi. NI vyema pia kuandaa fungu la dharura kukuokoa na majanga ya kifedha au la biashara yako inakufa pindi yanapojitokeza.
Mara nyingi watu huanzisha biashara wakiwa na ndoto za kutengeneza fedha lakini hawana ujuzi Wala matamaniko ya kujua usimamizi wa mzunguko wa fedha, Kodi , gharama au Mambo mengine ya kifedha. Usimamizi mbovu was fedha hutengeneza njia Bora ya kuuwa biashara yako.

NINI KIFANYIKE
Tumia mfumo sahihi au watu sahihi wa maswala ya kihasibu kuhifadhi kumbukumbu zako za fedha na miamala yote. Ikiwa ni pamoja na kujumuisha matumizi na mapato yote,Kisha tumia taarifa hizo kutengeneza jedwali lako la faida na hasara. Taarifa hizi zitakusaidia Kuonyesha mwendo wa biashara yako na si kufanya vitu gizani.

6.UKUAJI WA GHAFLA AU KUTANUKA BIASHARA KWA HARAKA .

Wakati mwingine biashara mpya inakuwa kuliko inavyoweza kustahimili. Unaingiza bidhaaa sokoni na ghafla unapokea maombi mengi kuliko unavyoweza kuhudumia. Au Mambo yanaluwa tofauti, unashawishika kuwa bidhaaa zako zitauza Sana na unaweka bidhaaa nyingi ghalani mwisho wa siku soko linakuwa tofauti na unabaki kutapatapa namna ya kujinasua na kutokufa kwa biashara yako.

NINI KIFANYIKE
Kukuwa na kupanuka kwa biashara kunahitaji umakini wa mipango na mikakati unaohusisha usimamizi wa uzalishaji wa siku baada ya siku. Hii inahusisha utafiti katika kupima mgawanyo was watu katika eneo husika,kiwango Cha kipato chao kinachotumika katika Aina ya bidhaaa na mipango endelevu ya eneo husika.
Tafiti hizi pia lazima zijiridhishe kuwa wakati NI sahihi na fedha kwa mpango huo zipo. Hakikisha biashara iliyopo iko imara kabla ya kuanza kujitanua lakini pia usiongezee bidhaaa ambazo huna uhakika wa kuziuza.

Kuanzisha biashara ni Jambo la kusisimua Sana ambalo linahitaji bidhaaa au huduma iliyojikamilisha na uwepo wa uhitsji thabiti wa huduma au bidhaaa hiyo sokoni. Kama una mpango wa kuanzisha biashara au tayari una biashara yafaa ujue kuwa mafanikio yako yanategemea umakini wa mipango na mikakati yako na umakini wa usimamizi wa fedha tangu mwanzo mpka mwisho wa biashara yako.

UNAKARIBISHWA KUJIUNGA NA DARASA LANGU LA BIASHARA KWA ADA YA TSH 2,000/= KWA WIKI KUPITIA WATSAP NUMBER ILIYOPO HAPO CHINI.


IMEANDALIWA NA
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA
Email bensonflexon@gmail.com
Facebook Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
watsap 0654859954
call/txt 0653384656
 
Napenda kujua unamiliki biashara gani, una mda gan kwenye biashara, mfanikio yako toka umemaliza
Mana wahitimu wengi hawawezi kutekeleza kulingana na taaluma yao ila hutaka wengine ndo wafanye.
Pita kwenye Makala zangu za nyuma nimeyainisha yote hayo.Inshort nmeanza kurun business nikiwa mwaka wa pili, na kwa Sasa Nina own Duka la nguo za ndani, ni mwandishi, na business consultant. Anything else?
 
Nisikilize vizuri. Achana na complex knowledge of business.

Biashara ndogo zinafeli kwa sababu kuu hizi mbili

1. Lack of passion kwa mwenye biashara, yaani ile drive ya muanzisha biashara

2. Lack of enough capital kumudu misukosuko ya biashara mpya.

Mengine yote mbwembwe tu
 
Nisikilize vizuri. Achana na complex knowledge of business.

Biashara ndogo zinafeli kwa sababu kuu hizi mbili

1. Lack of passion kwa mwenye biashara, yaani ile drive ya muanzisha biashara

2. Lack of enough capital kumudu misukosuko ya biashara mpya.

Mengine yote mbwembwe tu
Kuna watu wengi wana passion na mitaji na biashara zinakufa.
Kufanikiwa kwa biashara ni muunganiko wa vitu vingi sana sio hivyo viwili tu.
 
Biashara nyingi zinakufa kwa kua uwezo wa watu kununua bidha unapungua siku hadi siku na hio hupelekea wenye biashara kua na gharama kubwa za uendeshaji na faida kiduchu. Na mweshe huamua kufunga biashara zao.
 
Kama wewe ni msakatonge basi hizi nondo zinakuhusu m nipo kwenye field mwaka wa sita sasa..na yote nimeyapitia hasa namba 6
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom