Uchaguzi 2020 Sababu 27 za kwanini Magufuli hafai kupewa miaka mingine 5 ya kuwa Rais

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Magufuli kauliza katenda dhambi gani asipewe tena miaka 5. kwanza dhambi kubwa sana ni RAMBIRAMBI za tetemeko, kivuko kwa wahusika ziligeuzwa kuwa mali ya serikali na ikafanya kazi ya serikali huku mfuko wa maafa upo na bajeti yake ilipitishwa.

Sasa majibu yake haya hapa:

1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5
3. Ameongeza makato HESLB toka 8% to 15%
4. Amefukuza wafanyakazi na hajawapa hata senti tano kisa vyeti feki
5. Kaondoa fao la kujitoa NSSF
6. Kaondoa wanunuzi binafsi wa kahawa waliokuwa wanatoa bei nzuri
7. Karudisha gharama za matibabu kwa watoto na wajawazito
8 .Anatoza maiti kodi kuzitoa mochwari
9. Kavunja katiba ya nchi kuzuia wapinzani kufanya mikutano halali ya siasa
10. Katunga sheria kandamizi kukomoa watu
11. Kabambikia kesi watu kwa visasi na chuki
12. Kafilisi wafanyabiashara kwa chuki binafsi
13. Kathibiti mashirika ya kutetea haki za binadamu
14. Kadhibiti na kutisha vyombo vya habari na kuviamrisha vimtangaze yeye tu na chama chake
15. Kavuruga sana mahusiano ya kimataifa
16. Kavuruga demokrasia na anataka wananchi waishi kama mifugo yake kufuata analotaka
17. Kazima bunge live na kulitumia bunge kama muhuri kufanya mambo yake
18. Mahakama imebinywa na imekuwa siyo huru tena
19. Kawadhibiti viongozi wa dini wanaomkosoa na kumwambia ukweli
20. Kanunua ndege bila kufuata sheria ya PPRA
21. Watu wengi wameuwawa na kupotea na kutekwa
22.Amelea na kulinda kikosi kazi cha "watu wasiojulikana"
23. Amepandikiza hofu,ukatili na dhuluma kama nyenzoza siasa mpya za Tanzania na utu umetoweka
24. Kakivuruga chama chake na kukimega vipande vipande
25. Kajenga uwanja wa ndege kwao bila ya approval ya bunge wala cabinet
26. Alisema tutaishi kama MASHETANI.. kwa madai kuwa tulikuwa tunaishi kama Malaika. Hakika amelitimiza hilo.🤔
27. Kuwa na kundi la watu wasiojulikana awamu hii ya tano na polisi hawajawai kuwajua
 
Magufuli kauliza katenda dhambi gani asipewe tena miaka 5.. kwanza dhambi kubwa sana ni RAMBIRAMBI za tetemeko, kivuko kwa wahusika ziligeuzwa kuwa mali ya serikali na ikafanya kazi ya serikali huku mfuko wa maafa upo na bajeti yake ilipitishwa.

Sasa majibu yake haya hapa:

1. Hajatoa ajira miaka 5
2. Hajaongeza mishahara kwa miaka 5....
Lissu for Presidency
 
Binadamu yeyote anapenda sana kuwa kwenye comfort zone, yaani hatakubaliana na Jambo lolote hata liwe jema namna gani litalomuondoa kwenye hali aliyokuwa awali.

Mabadiliko yaliyoletwa na awamu ya tano yametufanya tuwajibike kwa asilimia kubwa katika kulipa Kodi, na kuwajibika katika nyanja nyingine pia za kijamii,

Sasa kwa kuwa kuna watu waliokuwa wakifaidi mfumo uliopita na sasa wamebanwa lazima walalamike,

Ndio hawa mleta mada akiwemo.
 
Amepoteza 5 yrs kupambana na Mbowe kuliko kupambana na shida zetu, katumia vibaya Kodi zetu kurudia chaguzi, kununua wapinzani ambao kawatelekeza baada ya kuunga juhudi kawaharibia potepote.

Fanyeni hima tumkatae October hatari yake atatushughulikia kweli kweli ameshatuonyesha atalipiza kisasi atanii.

Sasa kwann tuchague hatari . Hakuna chema chochote atafanya kwani atotuhitaji Tena tumpe kura.

Nafasi pekee ni October tukicheza tumekwiishaa.
 
Binadamu yeyote anapenda sana kuwa kwenye comfort zone, yaani hatakubaliana na Jambo lolote hata liwe jema namna gani litalomuondoa kwenye hali aliyokuwa awali.

Mabadiliko yaliyoletwa na awamu ya tano yametufanya tuwajibike kwa asilimia kubwa katika kulipa Kodi, na kuwajibika katika nyanja nyingine pia za kijamii,

sasa kwa kuwa kuna watu waliokuwa wakifaidi mfumo uliopita na sasa wamebanwa lazima walalamike,

Ndio hawa mleta mada akiwemo.
Aaah wapiga dili wa awamu hii jua lishawaka tafuteni ajira zingine October
 
Back
Top Bottom