Sababu 10 za kumng’oa mbunge kabla ya muhula; Ni pamoja na kutoishi jimboni, kutohudhuria vikao vya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Mwandishi Wetu Toleo la 297 5 Jun 2013


  • Ni pamoja na kutoishi jimboni, kutohudhuria vikao vya Bunge

KAMA rasimu ya Katiba iliyotangazwa wiki hii itaridhiwa, basi wapiga kura wanaweza kumng'oa mbunge wao kabla hata ya kukamilisha kipindi chake cha miaka mitano, wakirejea sababu mojawapo kati ya takriban 10 zinazotajwa kikatiba.


Ibara ya 124 (1) ya rasimu hiyo inaeleza; "......wananchi watakuwa na haki ya kumuondoa mbunge wao madarakani, endapo mbunge atafanya mojawapo ya mambo yafuatayo;


Mosi, kuunga mkono sera ambazo zinakwenda kinyume cha maslahi ya wapiga kura au kinyume cha maslahi ya Taifa. Pili, kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake. Tatu, kuacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi.


Nne, kutohudhuria vikao vya Bunge vitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika. Tano, kuajiriwa au kufanya kazi nyingine na kuacha kuzingatia kazi yake ya kuonana na wapiga kura wake. Sita; kufanya biashara, kumiliki kampuni au kuwa na hisa katika kampuni ambazo zina mikataba au uhusiano wa kibiashara na taasisi za umma kwa namna ambayo inaleta mgongano wa kimaslahi.


Saba; kutiwa hatiani kwa kosa linalohusiana na rushwa au kosa jingine la jinai. Nane, kutenda kitendo ambacho ni kinyume cha maadili au kukosa uaminifu. Tisa, kushindwa kuwasilisha au kutetea hoja zinazotokana na kero za wapiga kura wake au kumi: mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya Bunge.











 
Tutajuaje kama anaunga mkono tusivyovitaka au kumtuma wakati kura za wabunge ni siri?
 
Hiyo ya kutoishi kwa wapiga kura itaizika ccm. Maana kila mbunge anaishi Dar, kwa mfano Mkoa wa Kagera ni Mbunge wa Biharamulo tu ndo aishi Dar es salaam
 
sasa waganga njaa wote walioja bungeni wataogopa kuomba ubunge.
watakaoomba ni wale tu wenye nia ya kuwatumikia wananchu full stop. wale waliokuwa wanaona ni nafasi ya kupata tenda za serikali .... wasahau njia hii, kwao imefungwa. SAFI SANA HAPA!
 
Kwenye umiliki/uhusiano na kampuni hapo wengi watakwama maana wapo ujisafishia njia kwa ajili yaa kufanisha ukwepaaji kodi na kufanya biashara nyingine haramu!
 
Back
Top Bottom