Sababu 10 kwanini Tanzania inamuhitaji Job Yustino Ndugai kuwa Spika kwa miaka 5 tena

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,884
22,601
Wanajukwaa bunge la 11 linakwenda kumaliza muda wake ,kiongozi shupavu wa bunge hili ameonesha ubora wake wa hali ya juu hii inamaana Tanzania inamuhitaji kuliko yeye anavyoihitaji Tanzania hapa naweka madokezo kumi kwa nini anafaa kurejea tena kama kiongozi wa muhimili huu muhimu wa taifa letu :

1.Kusimamia Serikali katika miradi ya kimkakati .Job amekuwa makini na bunge lake kuhakikisha serkali ya awamu hii inafanikisha miradi kwa kutoa haki kwa wabunge wote kujadili pasina kungalia chama ,bunge limepitisha pesa za miradi na kamati za kibunge kufanya kazi ya kupitia kila uchao kuhakikisha ile dhana ya kuisimamia serkali,ukiona hii miradi jua speka wetu alikuwa kuwa nyuma yake.

2. Kutoruhusu Bunge kudhalilishwa
Kila aliyethubutu kulidhalilisha bunge letu tukufu amekipata cha mtemakuni kuanzia Makonda,Asadi na wabunge wa upinzania kulidhalilisha bunge amehakikisha chombo hiki cha wananchi hakidhalilishwi maana kukidharau ni kuwadharau wananchi walikiweka pale.

3.Kushirikiana na Serikali na Mahakama.
Hapa ameonesha kuwa ili bunge liisimamie serkali ni lazima lifanye kazi kwa ukaribu,urafiki na uwazi na sio uadui ,amewafunza watanzania kuwa kuisimamia serkali sio kuishambulia na kuidharau bali kuwa nayo karibu katika kutatua kero za wananchi huu ndio udugu wa watanzania

4. Kusimamia haki za wabunge bila kujali vyama vyao.
Mh spika ameonesha upekee ndio mara ya kwanza kuwatetea wabunge hadharani pale walipopitia mateso kutoka vyama vyao wabunge kama lijualikali,silinde,mwambe na lwakatale hawa ni mifano ya wazi kuwa spika alionesha kuwa na busara kwa kuwa wananchi wangekosa wawakilisha kwa kuonewa wabunge wako ,
Hakuna aliyetegemea kumuona spika akienda hospital kumtembelea KUB pamoja na matamshi ya dharau,dhihaka ya wabunge wa upinzania dhidi ya afya yake akiwemo mwenyewe K.U.B

5. Kilichangamsha bunge ukisikiliza jinsi anavyoendesha vikao vya bunge kwa uchangamfu analifanya hata kama umeboreka upende kulitazama matani ya hapa na pale na kuwafanya wabunge wajisikie huru kuzungumza

6. Kuwatumikia wananchi wa Kongwa .
Hapa job mtoto wa Yustino ameonesha kufanya kazi bora jimboni maana kwa miaka ya hivi karibuni kongwa inapaa sambamba na dodoma yake wananchi wa kongwa walilamba dume haswahaswa kwa huyu spika

7. Mabadiriko ya mfumo wa Bunge.
Bunge letu sasa linaenda sambamba na mabunge ya duania ya kwanza bunge limekuwa kidijitali sasa sio mambo ya makaratasi wabunge wanapata information hata wakiwa nje ya nchi na pia wanaweza kushiriki mijadala kama kawaida

8. Gawio la Serikali
Haijawahi kutokea kwa sasa pesa zinazobakia katika hurejeshwa serkalini ilizipangiwe matumizi mengine sio kuliwa kama zamani hii imeonesha kuwa bunge liko imara na spika anajielewa

9. Kuondoa matumizi mabaya ya pesa za wananchi.
Kama mbunge hayupo bungeni na amekula posho nairejesha na hakuna janjajanja ya kulipa pesa za matibabu kama mbunge hakufuata taratibu za kimatibabu za kibunge ,hii imemjengea heshima ndio maana Tanzania imekuwa mfano kwa mabunge ya commonwealth,SADC na EAC kwa kupewa heshima na hata bunge letu kila mwaka tangu2015-2020 linakula hati safi

10. Kuanzisha shule ya kimkakati ya wasichana (Bunge girls special school) yenye mchepuoa wa masomo ya sayansi ,hapa kweli aliona mbali sana na kuonesha kuwa vision yake inaweza kuleta matokeoa chanya siku zijazo,watoto wa maskini wanasoma katika shule ya kisasa kabisa

USSR
 
Wewe ni miongoni mwa wanaccm wachache sana wanaolipwa posho zao kwa kutumikishwa kwenye mambo magumu yenye kudhalilisha mno ! Wanyakyusa wanasema hivi , nanukuu , "KULILA MUUNTO " kwa tafsiri ni kwamba pamoja na kwamba unakula lakini unakula kwa jasho mno lililojaa tabu na masimango mazito mno !
 
Wewe ni miongoni mwa wanaccm wachache sana wanaolipwa posho zao kwa kutumikishwa kwenye mambo magumu yenye kudhalilisha mno ! Wanyakyusa wanasema hivi , nanukuu , "KULILA MUUNTO " kwa tafsiri ni kwamba pamoja na kwamba unakula lakini unakula kwa jasho mno lililojaa tabu na masimango mazito mno !
Kitendo cha spika kwenda kumwona mbowe hospital kimeonesha wanaccm tuivyokuwa na hila na visasi kama chadema wenye roho ya mauti muda wote
 
Ubunge alitolewa kwa kuonekana akiwa kwenye makongamano U.S. na U.K. huku anazuga unaumwa .
Ni utoro kama wa j .nasari
Sifa nyingine:
Baada ya risasi kushindwa kutoa uhai wa Lissu,alifanikisha kumvua ubunge kwa utoro angali akiwa kwenye matibabu.
 
Yaani katika mtu hafai kuwa kiongozi ni aaaaaaaaandugai. Huyu mtu ovyooo kabisa. Nawashangaa sana wanao msifu. Tena tusisahau kuwa aliwahi kumpiga mpinzani wake na akafa.
 
Kitendo cha spika kwenda kumwona mbowe hospital kimeonesha wanaccm tuivyokuwa na hila na visasi kama chadema wenye roho ya mauti muda wote

Hakwenda hospitali kumuona Mbowe kama mgonjwa, bali alienda kumnusa pombe ili aje kupotosha bungeni. Kama kweli anajua wajibu wake, angeitisha footage za CCTV Camera ili awe kwenye mstari sahihi wa maelezo ya spika.

Ubora wa hilo bunge tunaujua sisi wananchi, si kosa ww kuweka sababu zako maana hiyo ni haki yako. Ila ukweli ni kuwa huyo ni spika wa bunge kibogoyo, na sababu hasa ya hilo bunge kuwa kibogoyo, ni yeye kujipendekeza kwa rais fullstop.
 
Kweli kuna kundi la watu wasiojitambua hata kidogo, Ndugai ameonyesha udhaifu mkubwa, hawezi kulisimamia Bunge hata kidogo. Bora hata yule mama Makinda, sio huyu jamaa mtu anahama chama A kwenda B anamwambia toka leo wewe ni chama B na hama huko njoo huku.

Viongozi wetu wanashibisha matumbo, hilo wanaliweza, kushibisha matumbo yao hata kwa kuongea na kufanya utumbo.
 
Wana CCM, Hatumhitaji Ndugai wala Naibu wake, tunahitaji spika na naibu wawe watu wanaojua haki, wasiwe YES MAN N WOMEN, wawe na uwezo wa kuliendesha bunge bila upendeleo.

Viongozi wa kigogo wa awamu hii , mnaliaibisha jimbo la dodoma, ndugai, kabudi na lusinde,
 
IMG_2233.JPG
 
Haka kazee sikapendi!!!! kaongo!! kaongo!! kanafiki sana eti kamekulia tabu! wakati kamesoma chuo cha kimataifa? kiukweli maskini hasomi mpaka huko!

hotuba yake ya kuaga bunge kalidanganya eti wakt wa likizo Kanajificha kwa aibu, kanabaki chuo wenzake wakiondoka na madege?, hata hamu ya kumuona mama yake hakuwa nayo? roho mbaya tu!

wanafunzi bongo wana roho nzuri wangekuchangia Nauri! mkuu wa chuo angekupa nauri uondoke? kuliko kukaa ule bure! kalijitungia historia ya uongo!

na huyu ni wewe mwenyewe spika Ndugai! nielezee ukweli ulikuwa maskini? kulalia ngozi siyo umaskini! ni tamaduni zetu Africa! Sokoine, Kikwete, Wahasibu, Madaktari Wanatumia vijijini, Lowasa anatumia mpaka leo! wewe unaona ni umaskini???? Spika kweli?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom