demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,250
- 15,116
Kuelekea dirisha la ipo vita ya chini chini ya kuhusu Msuva kutamaniwa na Simba SC ili hali anahitajika Nyumbani “Jangwani”.
Ifahamike Simba SC walianza harakati zao mapema wakijua kumshawishi jamaa inahitaji jitihada ya ziada kwa kuwa hana vina saba nao.
Baada ya sakata lake la kesi baina ya muajiri wake Wydad Casablanca kuamuliwa, endapo kama hato pata timu nje ya Tanzania basi zifuatazo ni sababu 10 kwanini atachagua Yanga SC na kuwapotezea Simba SC.
1. Ushawishi wa Hersi.
Sote tunafahamu kuwa huyu jamaa ni mtanzania mwenye ushawishi nambari wani katika michezo hivi sasa. Ukiona mchezaji anafanya mazungumzo na hersi basi itakupasa ufanye zaidi ya kile ulichopanga ili umpiku.
2. Nyumbani.
Factor nyingine ni kutaka kujihisi kuwapo nyumbani. Msuva hawezi chagua Simba kwa sababu ya kujihisi Mkimbizi katika mazingira atakayo hitaji utulivu.
3. Bingwa mtetezi.
Yanga SC ni mabingwa watetezi. Nani hataki kuwa sehemu ya wachezaji bora 11 katika Ligi.? Nani ataki kucheza katika kikosi bora cha msimu uliopita.? Ni mjinga tu atachagua kucheza katika mazingira yatakayo mlazimu afanye cha ziada ili kupata ushindi.
4. Project Mpya ya Yanga SC
Yanga SC iko katika project mpya ambayo inalenga kuifanya klabu kuwa ya kwanza kushiriki fainali na kutwaa kombe la CAF. Aina ya wachezaji waliopo wana akisi malengo ya project ya klabu. Bila shaka Msuva atapendelea zaidi kuwa sehemu ya project hiyo.
5. Exposure na Kujitangaza.
Msuva ana malengo ya kucheza nje ya mipaka kwa mara nyingine tena. Yanga SC inatoa platform pekee ya kumtangaza mchezaji kimataifa kutokana na muendelezo mzuri wa matokea na ubora wa kikosi.
6. Support ya dhati.
Saimon anatambua wazi kuwa mashabiki wa Simba wanamfahamu kuwa ana mapenzi ya dhati na klabu ya Yanga. Hivyo ni vigumu kupata support ya mashabiki ndani na nje ya uwanja.
7. Mazingira mazuri ya kufanya kazi.
Yanga SC inaongoza kuwa na mazingira mazuri ya mchezaji. Hakuna mchezaji anaweza kuchagua Bunju badala ya AVIC TOWN. Kambi na nyumba za wachezaji ni bora zaidi hapa afrika mashariki na kati.
8. Old Friends.
Kuwapo kwa old friends kikosini ni magnet kubwa sana kumvutia Msuva. Msuva hana mahusiano ya urafiki na mchezaji yeyote kutoka Simba SC.
9. Maslahi.
Kimaslahi Yanga wanauwezo mkubwa sana wa kumlipa mchezaji kile anacho hitaji. Historia inaonyesha wakili msomi alishindwa kuongozewa mkataba wenye maslahi mapana na klabu yake. Sidhani kama Msuva yuko tayari kwa hilo.
10. Kikosi chenye njaa ya Mafanikio.
Sitaki kueleza mafanikio nadhani wengi wetu tunafahamu kuwa kuna mafanikio hewa na mafanikio kuntu. Kikosi cha Yanga kimejaa wachezaji vijana wenye kiu zaidi ya mafanikio. Na kiu yao inaonekana na kudhibitika uwanjani. Kwa Msuva hii ni destination mzuri zaidi.