Saa moja ya 'mapambano' mimi na waliojitambulisha kuwa ni Polisi

Utoto wako ndio unaopelekea uogope visa au kudhani havitokei...ngoja ukue bwana mdogo.

Mkasa huo ni tone tu katika mengi niliyopitia...nashangaa ni vipi unapata ujasiri wa kujiita mtu asiye julikana kwa akili hiyo uliyonayo!
STORY YA UONGO. HALAFU UONGO WA KITOTO. UNAANGALIA SANA MOVIES ZA KIHINDI MPAKA UNATAMANI KUISHI MAISHA HAYO.
 
Kuna mpemba walimzuia na carry yake ya samaki pale Salenda alikuwa anatoka Kunduchi anawahisha mzigo feri..akawaomba sana waruhusu samaki wakashushwe feri yeye anabaki pale na gari inarudi wakamgomea.
Samaki wakaozea pale na baada ya masaa 3 wakamuachia bila ya kuwa na sababu ya msingi ya kumzuia.
Baada siku 21 alianza kufa mmoja mmoja wale walimzuia hadi mtu wa pili kutoka mkuu wa kituo.
Hadi leo zikipita gari za samaki wanazivuta kama msafara wa Rais ili wawahi feri
 
Huwa wanasahau kwamba tuko nao huku huku mtaani na wanafamilia zao huku huku mtaani.na wale walioko kwenye kota,nao pia muda wakistaafu wanarudi huku huku mtaani.

Kuna jamaa yangu alipigwagwa na polisi kiuonevu miaka ya 1998,jamaa mpaka leo anaendelea kumfuatilia yule polisi kujua anaishi wapi.sababu anamjua yeye na ndugu zake. kwa sasa anasema ana jambo nae.hawezi kukubali.tulijaribu kushauri kwamba aachane naye mbona mambo ya kitambo hayo jamaa anasema alishaapa kulipa kisasi so hawezi vunja kiapo
Mi ninamla mke wa trafiki alikuwa anaishi pale Oysterbay kisa ni kulipiza kisasi tu!!! Nilikuwa namvuruga kweli kweli yaani
 
Aache kujidanganya chochote atachofanya itakuwa kama amewafanyia polisi wote na hapo atakuwa amewachokoza maana watamchakaza sana pili wataongaika ni familia yake sababu nna uhakika lazima azame ngomeni nimeona mengi sana uhuru ni kitu muhimu sana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kwani watajua..
 
Utoto raha sana.
Umekubali ukweli sasa. Ni kweli utoto ni raha maana ungekuwa mtu mzima usingeandika huu upuuzi humu ndani ungeandika mambo ya maana ya ukweli. Unaangalia sana movies za kihindi. Ukichanganya na umri wako ndo maana unaona utoto raha...😂😂😂
 
Salaam

Natambua kuwa wapo askari wetu wa jeshi la Polisi waadilifu na wenye kujitoa kwa moyo wa dhati na kuweka roho rehani ili sisi wananchi tubaki salama, heshima kwao, leo naelezea mkasa ulionikuta kutoka kwa Askari wasio waadilifu ili kulitibu Taifa, fuatana nami.

Yalikuwa majira ya jioni kama saa kumi na moja hivi nikiwa naendesha gari katika moja ya barabara kubwa huku nikiwa nimefungulia muziki taratibu japokuwa buster ilikuwa ikifunda haswa.

Nikafika kwenye taa za barabarani na kukuta taa nyekundu, ile kusimama tu ghafla mlango ulifunguliwa na kuingia kipande cha mtu na akakaa kwenye seat kama hakujatokea kitu! (Tangu siku hii ndiyo nilijua umuhimu wa ku lock milango) awali nilihisi labda ni mtu ninaefahamiana nae labda nimemsahau hivyo anataka lift lakini haikuwa hivyo, nilimuuliza kwa ukali kuwa yeye ni nani na akanijibu ni afisa wa Polisi wa kituo kimoja kikubwa na kwamba gari hii inafuatiliwa muda mrefu na taarifa zake wanazo kuwa inabeba mirungi.

Nilichukia kauli hii kutokana hii gari haiendeshwi na mwengine yeyote zaidi yangu na ninakoishi mpaka nifike kwenye shughuli zangu ni lazima nikaguliwe na Askari zaidi ya sehemu tatu, sasa kwanini nisikamatwe siku zote hizo

Nikamwambia mliwahi kunisimamisha sikusimama? Akasema hapana! Nikamwambia nani kakupa ruhusa ya kuingia ghafla kama mvamizi, unajua nina kiasi gani hapa na vipi ningekudhuru kwa kujihami ningekosea? Akatoa kitambulisho chake na ghafla taa zikaruhusu nikaondoa gari akiwemo.

Akanipa ishara nisimame sehemu kama mbili hili lakini sikusimama kwa sababu sipendi dharau na isitoshe nilikuwa na silaha kweli ya kujihami kama ni mvamizi.

Nikafika sehemu nzuri nikasimama na ghafla ikapaki Altezza kumbe ndiyo aliyotoka yule Afande na ana wenzake kama wanne wakaja.

Wakataka nishuke wakague gari, nikamtaka yule jamaa nae pia ashuke na wote wakapinga vikali kuwa yule abaki kwenye gari na hapa wakanifungua akili juu ya mkasa uliowahi kumkuta dogo flani dereva wa Fusso, alimruhusu askari apande juu ya mzigo akague na akampandikizia mirungi, ilitoka laki saba ndiyo gari ikaachiwa.

Ndugu msomaji, mimi ni mkimya sana ila nina hasira sana mtu akiingia kwenye njia zangu, hivyo sikushuka na iliibuka vita ya maneno kwa muda mpaka raia wakasogea, nikamwambia yule afande utashuka hii siyo gari ya baba yako! Na yote hii ni kwa sababu nilishaona nikizubaa linaweza kunikuta tukio baya katika maisha yangu.

Askari wakashangaa sana huyu mtu anajiamini nini kiasi hiki na haonyeshi hofu hata chembe hivyo jamaa akashuka wakafungua buti na kukagua kisha kusema hawajaridhika hivyo twende kituoni.

Safari ya kituoni ikaanza na yule kipande akapanda kwangu tena na huku akionyesha kuhangaika nikajua anataka kunitegea mzigo hivyo nikawa namkazia macho sana, alinihoji kama nimeshapitia Uaskari au jeshi lolote nikamjibu hii ni dunia na lolote linawezekana, akaniuliza nafanya shughuli gani nikamjibu ni mganga wa kienyeji na hapo nilikuwa naelekea baharini kuwapokea majini niliowatuma kuangamiza mahali.

Nilijibu hivi kwa maana mbili, kwanza hayakuwa mahojiano bali mazungumzo na pili ni kwamba mji huo lipo tukio maarufu lililo tokea la Askari kupewa pesa na mtu wa magendo na baadae kumchoma kwa wenzake, kilichomtokea ni kupata maradhi ya ajabu na nyumba yake kuungua moto kila jumapili ingawa inawahiwa kuzimwa, na gari yake ilikuwa inawaka moto pia pamoja na kuitoa battery, na sasa hivi amekatwa miguu huyo askari hivyo hali hiyo ilipelekea jamaa kuogopa ulozi

Kufika kituoni na jamaa aliposhuka nilii lock gari na kuwafuata wazee wenye magwanda marefu na vyeo mabegani lakini ghafla yule askari alinivuta pembeni na kuniambia matangazo ya nini! Tukarudi kwenye gari na wale wa Altezza wakawa wamefika na wakaanza kukagua gari na baadae wakaganda sana chini ya dashboard kama wamepoteza kitu lakini hakuna walichoona, hivyo wakamchukua chemba mwenzao ni kama walikuwa wakimuuliza mzigo umeweka wapi maana walimzunguka.

Kwangu hawakuja tena waliniruhusu kwa ishara kinyonge kabisa nikaondoka huku wale wakuu wa magwanda wakifuatilia kwa mbali kasumba yetu.

Hii ni wazi ni michezo ambayo usipoijua inakula kwako.

Wassalaam.
Macho tizama,sikio sikia akili chambua🙌
 
stupid police
Pole sana aseee sikukuu imewadia hela inatafutwa kwa udi na uvumba, kuna siku natokea Home magomeni nikapigwa mkono na Traffic wa kike nae akapanda mbele kisha akaniambia twende, nilikua naenda Posta lkn nlivyoona kapanda yupo kimya basi nkaelekea uelekeo wa Magomeni mikumi nikakata mitaa mpaka chang'ombe wala hakuna anaemsemesha mwenzake, na mie ndo kwanza nabadili chaneli za Redio mpk nkafika Tazara namuona anahangaika kutuma msg tu mda wote katoa macho balaa.

Baada ya kuvuka Tazara naona difenda kama tatu zimenizunguka wanasema kuna askari umemteka nkawaambia muulizeni awape scenario.

Ndo yule mdada maskini akaelezea ingawa kama ilivyokua wala hakueka chumvi. Maaskari wakaniuliza sasa ulikua unampeleka wapi nkawaambia nlijua labda anataka kwenda ninapoenda ambapo ni Pugu. Basi mdada akashuka hapo anatweta balaa nkageuza zangu gari na kurudi ofisini posta
 
Yaani katika kazi ambayo mtoto wangu akiniambia nitamvunja miguu yote na mikono ni kuhusu kazi ya upolisi.... Sijawahi kuwapenda, siwapendi ba sitokuja kuwapenda daima Wajinga sana hawa
 
Umekubali ukweli sasa. Ni kweli utoto ni raha maana ungekuwa mtu mzima usingeandika huu upuuzi humu ndani ungeandika mambo ya maana ya ukweli. Unaangalia sana movies za kihindi. Ukichanganya na umri wako ndo maana unaona utoto raha...
Itoshe kusema wewe ni mpumbavu, sasa hapo unaloona ni la hatari kiasi kwamba haliwezekani ni lipi? Watu Zanzibar waliwahi kuchinja Askari mwenye bunduki wewe unashangaa haya kwa uoga wako binafsi!?
 
STORY YA UONGO. HALAFU UONGO WENYEWE WA KITOTO. UNAANGALIA SANA MOVIES ZA KIHINDI MPAKA UNATAMANI KUISHI MAISHA HAYO.NA UNATAKA SISI WATU WAZIMA TUKUKUBALIE.😁
 
STORY YA UONGO. HALAFU UONGO WENYEWE WA KITOTO. UNAANGALIA SANA MOVIES ZA KIHINDI MPAKA UNATAMANI KUISHI MAISHA HAYO.NA UNATAKA SISI WATU WAZIMA TUKUKUBALIE.
Sehemu gani katika huu mkasa unapohisi ni uongo na haiwezekani kutokea katika hii dunia ili nikufungue akili?
Sisi watu wazima mara nyingi si waumini upumbavu hivyo twende kwa hoja iwapo hujifurahishi kwa akili mbovu bali unamaanisha.
 
Salaam

Natambua kuwa wapo askari wetu wa jeshi la Polisi waadilifu na wenye kujitoa kwa moyo wa dhati na kuweka roho rehani ili sisi wananchi tubaki salama, heshima kwao, leo naelezea mkasa ulionikuta kutoka kwa Askari wasio waadilifu ili kulitibu Taifa, fuatana nami.

Yalikuwa majira ya jioni kama saa kumi na moja hivi nikiwa naendesha gari katika moja ya barabara kubwa huku nikiwa nimefungulia muziki taratibu japokuwa buster ilikuwa ikifunda haswa.

Nikafika kwenye taa za barabarani na kukuta taa nyekundu, ile kusimama tu ghafla mlango ulifunguliwa na kuingia kipande cha mtu na akakaa kwenye seat kama hakujatokea kitu! (Tangu siku hii ndiyo nilijua umuhimu wa ku lock milango) awali nilihisi labda ni mtu ninaefahamiana nae labda nimemsahau hivyo anataka lift lakini haikuwa hivyo, nilimuuliza kwa ukali kuwa yeye ni nani na akanijibu ni afisa wa Polisi wa kituo kimoja kikubwa na kwamba gari hii inafuatiliwa muda mrefu na taarifa zake wanazo kuwa inabeba mirungi.

Nilichukia kauli hii kutokana hii gari haiendeshwi na mwengine yeyote zaidi yangu na ninakoishi mpaka nifike kwenye shughuli zangu ni lazima nikaguliwe na Askari zaidi ya sehemu tatu, sasa kwanini nisikamatwe siku zote hizo

Nikamwambia mliwahi kunisimamisha sikusimama? Akasema hapana! Nikamwambia nani kakupa ruhusa ya kuingia ghafla kama mvamizi, unajua nina kiasi gani hapa na vipi ningekudhuru kwa kujihami ningekosea? Akatoa kitambulisho chake na ghafla taa zikaruhusu nikaondoa gari akiwemo.

Akanipa ishara nisimame sehemu kama mbili hili lakini sikusimama kwa sababu sipendi dharau na isitoshe nilikuwa na silaha kweli ya kujihami kama ni mvamizi.

Nikafika sehemu nzuri nikasimama na ghafla ikapaki Altezza kumbe ndiyo aliyotoka yule Afande na ana wenzake kama wanne wakaja.

Wakataka nishuke wakague gari, nikamtaka yule jamaa nae pia ashuke na wote wakapinga vikali kuwa yule abaki kwenye gari na hapa wakanifungua akili juu ya mkasa uliowahi kumkuta dogo flani dereva wa Fusso, alimruhusu askari apande juu ya mzigo akague na akampandikizia mirungi, ilitoka laki saba ndiyo gari ikaachiwa.

Ndugu msomaji, mimi ni mkimya sana ila nina hasira sana mtu akiingia kwenye njia zangu, hivyo sikushuka na iliibuka vita ya maneno kwa muda mpaka raia wakasogea, nikamwambia yule afande utashuka hii siyo gari ya baba yako! Na yote hii ni kwa sababu nilishaona nikizubaa linaweza kunikuta tukio baya katika maisha yangu.

Askari wakashangaa sana huyu mtu anajiamini nini kiasi hiki na haonyeshi hofu hata chembe hivyo jamaa akashuka wakafungua buti na kukagua kisha kusema hawajaridhika hivyo twende kituoni.

Safari ya kituoni ikaanza na yule kipande akapanda kwangu tena na huku akionyesha kuhangaika nikajua anataka kunitegea mzigo hivyo nikawa namkazia macho sana, alinihoji kama nimeshapitia Uaskari au jeshi lolote nikamjibu hii ni dunia na lolote linawezekana, akaniuliza nafanya shughuli gani nikamjibu ni mganga wa kienyeji na hapo nilikuwa naelekea baharini kuwapokea majini niliowatuma kuangamiza mahali.

Nilijibu hivi kwa maana mbili, kwanza hayakuwa mahojiano bali mazungumzo na pili ni kwamba mji huo lipo tukio maarufu lililo tokea la Askari kupewa pesa na mtu wa magendo na baadae kumchoma kwa wenzake, kilichomtokea ni kupata maradhi ya ajabu na nyumba yake kuungua moto kila jumapili ingawa inawahiwa kuzimwa, na gari yake ilikuwa inawaka moto pia pamoja na kuitoa battery, na sasa hivi amekatwa miguu huyo askari hivyo hali hiyo ilipelekea jamaa kuogopa ulozi

Kufika kituoni na jamaa aliposhuka nilii lock gari na kuwafuata wazee wenye magwanda marefu na vyeo mabegani lakini ghafla yule askari alinivuta pembeni na kuniambia matangazo ya nini! Tukarudi kwenye gari na wale wa Altezza wakawa wamefika na wakaanza kukagua gari na baadae wakaganda sana chini ya dashboard kama wamepoteza kitu lakini hakuna walichoona, hivyo wakamchukua chemba mwenzao ni kama walikuwa wakimuuliza mzigo umeweka wapi maana walimzunguka.

Kwangu hawakuja tena waliniruhusu kwa ishara kinyonge kabisa nikaondoka huku wale wakuu wa magwanda wakifuatilia kwa mbali kasumba yetu.

Hii ni wazi ni michezo ambayo usipoijua inakula kwako.

Wassalaam.
Hii stori ya kimkakati haina uhalisia

Kimsingi huwezi kufika mpaka ngome ukanasuka, kwa kuogopewa nini?
 
Huwa wanasahau kwamba tuko nao huku huku mtaani na wanafamilia zao huku huku mtaani.na wale walioko kwenye kota,nao pia muda wakistaafu wanarudi huku huku mtaani.

Kuna jamaa yangu alipigwagwa na polisi kiuonevu miaka ya 1998,jamaa mpaka leo anaendelea kumfuatilia yule polisi kujua anaishi wapi.sababu anamjua yeye na ndugu zake. kwa sasa anasema ana jambo nae.hawezi kukubali.tulijaribu kushauri kwamba aachane naye mbona mambo ya kitambo hayo jamaa anasema alishaapa kulipa kisasi so hawezi vunja kiapo

Dah! nimesoma mpaka nimesisimka. Kwa huyo Askari Polisi na alimpizie tu kisasi. Nina tabia ya kulipiza kisasi pia.
Huyo jamaa ningekuwa namjua ningempa nauli ya Daladala ya kumfuatilia adui yake ya mwaka mzima.
 
Juzi Kati wamenikamata Misigiri pale chini nikipanda mlima wakasema kwann nime overtake kwenye mlima nikawaambia nawahi Dodoma wakawa wapole hapo nipo na Corolla 111 nafika pale juu WP 3 mkono nikaweka pembeni wanataka leseni nikawajibu sijatembea nayo na sijui ilipo maana Nina makazi mengi mara oohoo mbona unatetemeka nikamjibu nikiongea na askari tena WP huwa sina hofu mara gia huku wanaona ni corrupt Sana Hawa mbuzi
Kuna stori zingine tutaponzana humu

Unatia gia unaondoka kumbe mwenzako alitia gia akaondoka ni katibu wa wizara fulani au anajuana na waziri fulani
 
Back
Top Bottom