Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake.

2. Mahakama kwa Tarehe hiyohiyo ilikimbizwa mchamchaka na dola ikabariki atolewe na baada ya kutoka akakabidhiwa kwa serikali ambayo ndiyo iliyomtuhumu.

3. Baada ya kupindua mhimili wa serikali na mahakama, Nusrat akisaidiwa na Tume ya uchaguzi (serikali) Tarehe 24/11/2020 akatinga kwenye viunga vya Bunge na kukutana na spika kisha spika akamwapisha kuwa Mbunge wa viti maalumu. Ikumbukwe Mbunge huyu anatakiwa apitishe fomu zake za Ubunge mahakamani hivyo yawezekana mahakama ilitumika pia kubariki kilichotokea bungeni. Bunge nalo likabeba mapungufu ya serikali na kuyapiga mhuri, Nusrat leo ni mbunge siyo mahabusu Tena.

Nusrat anatukumbusha kwamba unapodai haki yako na ukaamini katika kuwatetea wananchi movu huibuka na kuvunja misingi yote ya sheria na kukuinua.

Nusrat Mtuhumiwa amefanya miujiza mikubwa inayopaswa kuandikwa kwenye mbao mbalimbali, ndani ya saa ishirini na nne amekuwa na hadhi tatu muhimu ambazo ni binadamu wachache wamewahi kuzipata Duniani. Hadhi hizo Ni;
1. Hadi tarehe 23/11/2020 jioni alikuwa Mtuhumiwa wa makosa yasiyo na dhamana akiishi mahabusu.

2. Tarehe 23/11/2020 usiku akatoka gerezani akiwa Mwananchi huru asiye na hatia na kuelekea nyumbani kuoga na kuchagua nguo ya kuvaa siku iliyofuata. Natumai hakulala.

3. Tarehe 24/11/2020 asubuhi akaibuka kwenye viunga vya Bunge na kushika msahafu kisha kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania yaani Mheshimiwa huku akiwa na kinga ya kibunge.

Haya yanatokea ulimwenguni ambapo kila Jumapili tunashinda nyumba za ibada kumwabudu muumba, haya yanafanywa na binadamu walewale ambao wanaomba Mungu atuepushe na balaa. Haya yanafanywa na binadamu wakitumia vitabu vitakatifu kuapa mbele ya vyombo vya habari.

Nadhani Nusrat anatuonesha kwamba adui yetu siyo Beberu bali adui yetu ni mtu mweusi anayelipwa fedha na watanzania kufanya maigizo ndani ya Tanzania kwa kutumia ofisi za umma na kutumia vitabu na misaafu tunayoamini ni mitikatifu.

Tunajiombea adhabu kwa Mungu, nadhani adhabu ipo mbioni kuwapata wanaowatendea Hawa viumbe haya. Si utashi wa Nusrat kuapa bali ameapa kuinusuru familia yake na ya mahabusu wengine waliokua hawana hatia. Ipo siku Nusrat atakua huru, ipo siku atapata nguvu yakusimamia anachokiamini.

Pole Nusrat na hongera kwa kuteuliwa kuwa Mbunge ukitokea Mahabusu. Wameona unafaa, wameona una kitu cha ziada kwa Taifa, usilipize tenda kwa nafasi uliyopewa.

Hongera Mtuhumiwa, hongera mtu huru, hongera Mbunge, hongera mpiganaji. Umeandika historia.
 
Ushauri wa bure kwa mtoa mada

1. Achana na siasa za Tanzania. Kwa usalama wa afya yako, NEVER TAKE TANZANIAN POLITICS SERIOUSLY

2. Tumia muda wako kula vizuri, kunywa maji mengi, kula matunda na fanya mazoezi.

3. Hakikisha unatafuta future ya watoto wako na wewe mwenyewe kwa njia zingine zozote nje ya siasa.

4. Sio kila unaemuona kanisani kavaa koti kafunga mikono kifuani anasali kwa unyenyekevu anakuwa ana maanisha.
 
Ni wakati wananchi wa tanganyika waelewe kuwa hii nchi si ya kupiganiwa na chama fulani, bali watu wote. Hata kama huendi vitani, watie moyo waliopo vitani, sio unawaacha unaenda kula bata unategemea wafie huko kwa ajili yako. Wananchi mjifunze. Chama hakiwapiganii msipojipigania wenyewe

Acheni upumbavu bwana.
 
Ushauri wa bure kwa mtoa mada

1. Achana na siasa za Tanzania. Kwa usalama wa afya yako, NEVER TAKE TANZANIAN POLITICS SERIOUSLY...
Imekuaje raia wa TANZANIAA wanaishi kama wageni kwenye Taifa Lao? Maana hawajali lolote wala chochote kuhusu serikali na mambo yanayofanyika ndani ya serikali, ili mradi maisha Yao yanasonga mbele kwa kupata ubwabwa na mboga wanaona ni Sawa tu.

Ukimya wao unaweza Sema Wana Taifa lingine tofauti na hili, Kwamba hapa wamekuja kutafuta tu na hawana haja ya Kutengeneza mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho.

Tume fika pahala raia wa Tanzania bila aibu anasema yeye siasa haimuhusu kwasababu sio mwana siasa! Anyway hapo utasema labda walinyimwa elimu ndio maana wanatoa kauli kama hizo.

Tuzidi kuwaombea hawa raia.
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake....

Hiyo inaitwa.. Chukua Chako Mapema. Alie juu mpandie hukohuko.... Acha kazi iendelee
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake....

Hata mimi naweza kulaumu shetani kanipitia kumbe kuna wanadamu,majini,wanga,vibwengu na wote wapo kwenye utawala wa mwenyemungu ila kwa kuwa yesu alisema ya mungu mpe mungu na ya muhandishi mpe JF
 
Mnyika katumia nguvu kubwa kuhalalisha mamlaka yake halafu jioni Halima Mdee anasambaza audio ya kumkejeli.

Mbowe, Mnyika na viongozi wa juu wa CHADEMA umefika wakati wajiuzulu kwa kuambiwa na nafsi zao wenyewe na sio kusubiri fedheha za majukwaani na njiani.
 
Kuna mtu ana Mkono wa chuma ndio yuko nyuma ya haya yote., what is impossible is possible within a second.,

Kuna wakati watanzania wanajiuliza kuna haja gani kuwa na majengo na gharama kama hizi mahkama zetu., kuajiriwa majaji kulipwa mishahara na posho mbali mbali wakati kuna mahali unaweza aidha kupata zaidi ya haki zako au kuzikosa kabisa na kwa muda mduchu sana.,
 
Ushauri wa bure kwa mtoa mada

1. Achana na siasa za Tanzania. Kwa usalama wa afya yako, NEVER TAKE TANZANIAN POLITICS SERIOUSLY

2. Tumia muda wako kula vizuri, kunywa maji mengi, kula matunda na fanya mazoezi

3. Hakikisha unatafuta future ya watoto wako na wewe mwenyewe kwa njia zingine zozote nje ya siasa

4. Sio kila unaemuona kanisani kavaa koti kafunga mikono kifuani anasali kwa unyenyekevu anakuwa ana maanisha

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
Inasikitisha Sana, mwanamke akishakuwa mwanaharakati anapitia changamoto nyingi Sana, Ndio maana wengine mnawaona wakina Mdee kama wasariti lakini washakutana na madhira mengi ya kuwekwa rokapu, wakati mwingine umo rokapu wanaweza wakawa wanadharirishwa kijinsia Bado kutishiwa maisha inafikia kipindi anafanyaa maamuzi kama haya
 
Kwani angetolewa gerezani kwa utaratibu wa kisheria halafu mengine yakafuata kungekuwa na shida gani?
Ubabe wa kipumbavu ni tatizo kubwa sana. Wapumbavu hawatakiwi kupewa nafasi ya kuamua katika jamii.
Babu rokapu isikiee tuuu
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake.

2. Mahakama kwa Tarehe hiyohiyo ilikimbizwa mchamchaka na dola ikabariki atolewe na baada ya kutoka akakabidhiwa kwa serikali ambayo ndiyo iliyomtuhumu.

3. Baada ya kupindua mhimili wa serikali na mahakama, Nusrat akisaidiwa na Tume ya uchaguzi (serikali) Tarehe 24/11/2020 akatinga kwenye viunga vya Bunge na kukutana na spika kisha spika akamwapisha kuwa Mbunge wa viti maalumu. Ikumbukwe Mbunge huyu anatakiwa apitishe fomu zake za Ubunge mahakamani hivyo yawezekana mahakama ilitumika pia kubariki kilichotokea bungeni. Bunge nalo likabeba mapungufu ya serikali na kuyapiga mhuri, Nusrat leo ni mbunge siyo mahabusu Tena.

Nusrat anatukumbusha kwamba unapodai haki yako na ukaamini katika kuwatetea wananchi movu huibuka na kuvunja misingi yote ya sheria na kukuinua.

Nusrat Mtuhumiwa amefanya miujiza mikubwa inayopaswa kuandikwa kwenye mbao mbalimbali, ndani ya saa ishirini na nne amekuwa na hadhi tatu muhimu ambazo ni binadamu wachache wamewahi kuzipata Duniani. Hadhi hizo Ni;
1. Hadi tarehe 23/11/2020 jioni alikuwa Mtuhumiwa wa makosa yasiyo na dhamana akiishi mahabusu.
2. Tarehe 23/11/2020 usiku akatoka gerezani akiwa Mwananchi huru asiye na hatia na kuelekea nyumbani kuoga na kuchagua nguo ya kuvaa siku iliyofuata. Natumai hakulala
3.Tarehe 24/11/2020 asubuhi akaibuka kwenye viunga vya Bunge na kushika msahafu kisha kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania yaani Mheshimiwa huku akiwa na kinga ya kibunge.

Haya yanatokea ulimwenguni ambapo kila Jumapili tunashinda nyumba za ibada kumwabudu muumba, haya yanafanywa na binadamu walewale ambao wanaomba Mungu atuepushe na balaa. Haya yanafanywa na binadamu wakitumia vitabu vitakatifu kuapa mbele ya vyombo vya habari. Nadhani Nasrati anatuonyesha kwamba adui yetu siyo Beberu bali adui yetu ni mtu mweusi anayelipwa fedha na watanzania kufanya maigizo ndani ya Tanzania kwa kutumia ofisi za umma na kutumia vitabu na misaafu tunayoamini ni mitikatifu. Tunajiombea adhabu kwa Mungu, nadhani adhabu ipo mbioni kuwapata wanaowatendea Hawa viumbe haya. Si utashi wa Nasrati kuapa bali ameapa kuinusuru familia yake na ya mahabusu wengine waliokua hawana hatia. Ipo siku Nasrati atakua huru, ipo siku atapata nguvu yakusimamia anachokiamini. Pole Nasrati na hongera kwa kuteuliwa kuwa Mbunge ukitokea Mahabusu. Wameona unafaa, wameona unakitu Cha ziada kwa Taifa, usilipize tenda kwa nafasi uliyopewa.

Hongera Mtuhumiwa, hongera mtu huru, hongera Mbunge, hongera mpiganaji. Umeandika historia.
Labda ni Afisa Kipenyo! Who knows!!
 
60 Reactions
Reply
Back
Top Bottom