Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Mtu
Ni wakati wananchi wa tanganyika waelewe kuwa hii nchi si ya kupiganiwa na chama fulani, bali watu wote. Hata kama huendi vitani, watie moyo waliopo vitani, sio unawaacha unaenda kula bata unategemea wafie huko kwa ajili yako. Wananchi mjifunze. Chama hakiwapiganii msipojipigania wenyewe

Acheni upumbavu bwana.
Mtu amaekula ameshiba na pesa ya pombe tatua anayo akajipiganie nini?
Yaani asilewe ila aende kupmabania mtu?
Acha matani basi,
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake....
Kuna watu wamedhamiria kuinajisi TANZANIA
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake.

2. Mahakama kwa Tarehe hiyohiyo ilikimbizwa mchamchaka na dola ikabariki atolewe na baada ya kutoka akakabidhiwa kwa serikali ambayo ndiyo iliyomtuhumu.

3. Baada ya kupindua mhimili wa serikali na mahakama, Nusrat akisaidiwa na Tume ya uchaguzi (serikali) Tarehe 24/11/2020 akatinga kwenye viunga vya Bunge na kukutana na spika kisha spika akamwapisha kuwa Mbunge wa viti maalumu. Ikumbukwe Mbunge huyu anatakiwa apitishe fomu zake za Ubunge mahakamani hivyo yawezekana mahakama ilitumika pia kubariki kilichotokea bungeni. Bunge nalo likabeba mapungufu ya serikali na kuyapiga mhuri, Nusrat leo ni mbunge siyo mahabusu Tena.

Nusrat anatukumbusha kwamba unapodai haki yako na ukaamini katika kuwatetea wananchi movu huibuka na kuvunja misingi yote ya sheria na kukuinua.

Nusrat Mtuhumiwa amefanya miujiza mikubwa inayopaswa kuandikwa kwenye mbao mbalimbali, ndani ya saa ishirini na nne amekuwa na hadhi tatu muhimu ambazo ni binadamu wachache wamewahi kuzipata Duniani. Hadhi hizo Ni;
1. Hadi tarehe 23/11/2020 jioni alikuwa Mtuhumiwa wa makosa yasiyo na dhamana akiishi mahabusu.

2. Tarehe 23/11/2020 usiku akatoka gerezani akiwa Mwananchi huru asiye na hatia na kuelekea nyumbani kuoga na kuchagua nguo ya kuvaa siku iliyofuata. Natumai hakulala.

3. Tarehe 24/11/2020 asubuhi akaibuka kwenye viunga vya Bunge na kushika msahafu kisha kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania yaani Mheshimiwa huku akiwa na kinga ya kibunge.

Haya yanatokea ulimwenguni ambapo kila Jumapili tunashinda nyumba za ibada kumwabudu muumba, haya yanafanywa na binadamu walewale ambao wanaomba Mungu atuepushe na balaa. Haya yanafanywa na binadamu wakitumia vitabu vitakatifu kuapa mbele ya vyombo vya habari.

Nadhani Nusrat anatuonesha kwamba adui yetu siyo Beberu bali adui yetu ni mtu mweusi anayelipwa fedha na watanzania kufanya maigizo ndani ya Tanzania kwa kutumia ofisi za umma na kutumia vitabu na misaafu tunayoamini ni mitikatifu.

Tunajiombea adhabu kwa Mungu, nadhani adhabu ipo mbioni kuwapata wanaowatendea Hawa viumbe haya. Si utashi wa Nusrat kuapa bali ameapa kuinusuru familia yake na ya mahabusu wengine waliokua hawana hatia. Ipo siku Nusrat atakua huru, ipo siku atapata nguvu yakusimamia anachokiamini.

Pole Nusrat na hongera kwa kuteuliwa kuwa Mbunge ukitokea Mahabusu. Wameona unafaa, wameona una kitu cha ziada kwa Taifa, usilipize tenda kwa nafasi uliyopewa.

Hongera Mtuhumiwa, hongera mtu huru, hongera Mbunge, hongera mpiganaji. Umeandika historia.
99999o9
Hiyo inaitwa.. Chukua Chako Mapema. Alie juu mpandie hukohuko.... Acha kazi iendelee
 
kifupi kirefu hiyo namba moja umeikosea.Alitolewaje mahabusu wakati ili mtu ambae kesi yake haina dhamana atolewe mahabusu ni lazima DPP amwambie hakimu/jaji mbele ya mahakama kuwa hana tena maslahi na kesi husika?Haya yalifanyika?
 
Kuna mtu ana Mkono wa chuma ndio yuko nyuma ya haya yote., what is impossible is possible within a second.,

Kuna wakati watanzania wanajiuliza kuna haja gani kuwa na majengo na gharama kama hizi mahkama zetu., kuajiriwa majaji kulipwa mishahara na posho mbali mbali wakati kuna mahali unaweza aidha kupata zaidi ya haki zako au kuzikosa kabisa na kwa muda mduchu sana.,
Kuna Dpp,jaji, spika asiyeonekana aliwahi tamani awe IGP, huendo ndo CDF, DG wa tiss

Amewaahidi viti maalum atawalinda ikiwa watafukuzw,a amemwagiza spika ahakikishe viti maalumu wanapata maslahi stahiki

Yuko radhi atumie NEC, TISs, police ili mdee asiwe mbunge wa kawe lakini awe viti maalum + hongo ya mil. 100.
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake.

2. Mahakama kwa Tarehe hiyohiyo ilikimbizwa mchamchaka na dola ikabariki atolewe na baada ya kutoka akakabidhiwa kwa serikali ambayo ndiyo iliyomtuhumu.

3. Baada ya kupindua mhimili wa serikali na mahakama, Nusrat akisaidiwa na Tume ya uchaguzi (serikali) Tarehe 24/11/2020 akatinga kwenye viunga vya Bunge na kukutana na spika kisha spika akamwapisha kuwa Mbunge wa viti maalumu. Ikumbukwe Mbunge huyu anatakiwa apitishe fomu zake za Ubunge mahakamani hivyo yawezekana mahakama ilitumika pia kubariki kilichotokea bungeni. Bunge nalo likabeba mapungufu ya serikali na kuyapiga mhuri, Nusrat leo ni mbunge siyo mahabusu Tena.

Nusrat anatukumbusha kwamba unapodai haki yako na ukaamini katika kuwatetea wananchi movu huibuka na kuvunja misingi yote ya sheria na kukuinua.

Nusrat Mtuhumiwa amefanya miujiza mikubwa inayopaswa kuandikwa kwenye mbao mbalimbali, ndani ya saa ishirini na nne amekuwa na hadhi tatu muhimu ambazo ni binadamu wachache wamewahi kuzipata Duniani. Hadhi hizo Ni;
1. Hadi tarehe 23/11/2020 jioni alikuwa Mtuhumiwa wa makosa yasiyo na dhamana akiishi mahabusu.

2. Tarehe 23/11/2020 usiku akatoka gerezani akiwa Mwananchi huru asiye na hatia na kuelekea nyumbani kuoga na kuchagua nguo ya kuvaa siku iliyofuata. Natumai hakulala.

3. Tarehe 24/11/2020 asubuhi akaibuka kwenye viunga vya Bunge na kushika msahafu kisha kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania yaani Mheshimiwa huku akiwa na kinga ya kibunge.

Haya yanatokea ulimwenguni ambapo kila Jumapili tunashinda nyumba za ibada kumwabudu muumba, haya yanafanywa na binadamu walewale ambao wanaomba Mungu atuepushe na balaa. Haya yanafanywa na binadamu wakitumia vitabu vitakatifu kuapa mbele ya vyombo vya habari.

Nadhani Nusrat anatuonesha kwamba adui yetu siyo Beberu bali adui yetu ni mtu mweusi anayelipwa fedha na watanzania kufanya maigizo ndani ya Tanzania kwa kutumia ofisi za umma na kutumia vitabu na misaafu tunayoamini ni mitikatifu.

Tunajiombea adhabu kwa Mungu, nadhani adhabu ipo mbioni kuwapata wanaowatendea Hawa viumbe haya. Si utashi wa Nusrat kuapa bali ameapa kuinusuru familia yake na ya mahabusu wengine waliokua hawana hatia. Ipo siku Nusrat atakua huru, ipo siku atapata nguvu yakusimamia anachokiamini.

Pole Nusrat na hongera kwa kuteuliwa kuwa Mbunge ukitokea Mahabusu. Wameona unafaa, wameona una kitu cha ziada kwa Taifa, usilipize tenda kwa nafasi uliyopewa.

Hongera Mtuhumiwa, hongera mtu huru, hongera Mbunge, hongera mpiganaji. Umeandika historia.
Mbona unalilia!? Kwenye kampeni si mlikuwa mnapiga kelele watu magerezani waachiwe, bila dhamana??? Ndo kaachiwa sasa! Au ulitaka afie huko ili mzidi kujenga hoja za uzushi??? Umesema "mahakama imepelekeshwa mchakamchaka." Je unajua spidi ya utendaji wa mahakama kuwa ni "gani," kimfano!?? Ukijibu nitag, sawa? Usiponijibu nijulishe pia, sawa!?
 
Ushauri wa bure kwa mtoa mada

1. Achana na siasa za Tanzania. Kwa usalama wa afya yako, NEVER TAKE TANZANIAN POLITICS SERIOUSLY

2. Tumia muda wako kula vizuri, kunywa maji mengi, kula matunda na fanya mazoezi.

3. Hakikisha unatafuta future ya watoto wako na wewe mwenyewe kwa njia zingine zozote nje ya siasa.

4. Sio kila unaemuona kanisani kavaa koti kafunga mikono kifuani anasali kwa unyenyekevu anakuwa ana maanisha.

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
Wee fanya hivyo mwenyewe. Kuna watu bado wana Imani na dhana ya Tanzania na hawaishi hapa duniani kwa kujaza matumbo yao tu na kutotoa watoto kama wewe! Sifa ya kuwa 'selfish' ni mbaya sana!
 
Ili mtu ateuliwe kuwa Mbunge Viti Maalum anatakiwa kujaza fomu za NEC namba 8D ambazo sehemu C Inatakiwa kujazwa na Katibu Mkuu wa Chama, na kiapo mbele ya Hakimu. Kama NEC imepokea hizo fomu, Mnyika alizijaza?

Kama Mnyika anatuambia akuzijaza, Nani alizijaza?

Je, NEC wanamjua Katibu Mkuu wa Chadema? Ndiye huyo aliyejaza?

Nusrat alikuwa Mahabusu, je, Nani alimjazia hizo fomu na alimjazia akiwa wapi na kuzirejesha Chadema? Je, mahakamani Nani alikwenda kuapa au Nusrati alitolewa akapelekwa mahakamani kimyakimya?

Je, sheria inaruhusu mtu kumjazia fomu za Ubunge mteule ambaye hayupo?Hakimu gani alimuapisha mtu asiyekuwepo?

Kama huu mchakato haukufuatwa Kuna umuhimu wa kuwa na taratibu na sheria?

Nasrati na wenzake walifutiwa mashtaka wakati gani na mbele ya hakimu Nani?

Kama lengo ni kuiua CHADEMA je tunaamini tunaiua au tunaua imani ya wananchi kwa vyombo vilivyopewa dhamana ya kusimamia haki?

Endapo mahakama ilimnyima Nusrat na wenzake dhamana, then over suddenly Jamhuri inajitokeza na kuwatoa ndani kisha bila kusita anatinga bungeni hatuoni Kama mahakama inatumika kuwaweka Mahabusu watu wasio na hatia kinyume kabisa na misingi ya uwepo wa chombo hiki?

Kama moja ya kazi ya Mahakama nikutenda haki, ni wakati gani Mahakama inapaswa kutenda haki? Ni baada ya kumnyima mtu Uhuru kwa miezi au miaka wakimtia Mahabusu? Au ni pale tu Mtuhumiwa anapofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ndipo mahakama inapaswa kutenda haki?

Je, mahakama huru inaona ni haki kuendelea kupokea chaji zisizo na mashiko chini ya amri ya kiapo Cha DPP kuwatia watu ndani?

Kwanini tuendelee kuamini mahakama ni chombo Cha haki Kama binadamu wanaopaswa kusimia haki hawapo tayari kuisimamia?
Sijaona 'impunity' dhidi ya sheria kama katika kipindi hiki! Sheria inafuatwa ikimhusu mpinzani tu, ama wengine ni malaika!
Wasidhani haya yanajificha, wako wengi tu duniani wanaofuatia. Siku moja yooooote haya yatakuja hesabiwa!
 
Maandamano tarehe 2 lakini tarehe moja Polisiccm wakaanza vitisho ikiwemo kuwakamata viongozi wa chadema siku moja kabla ya maandamano ni kwa nini hawakusubiria ifike tarehe 2 ? Nani muoga hapo?
Kwa maana nyingine, unaweza kufungwa Tanzania kwa 'kufikiria' kutenda kosa. Jirani yangu aweza kuniadhibu kwa kuwa 'nina ala' ya kumnajisia mkewe! Nchi ya ajjjabbu kabisa!
 
Back
Top Bottom