Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Hii nchi imesha kuwa ya kisenge, amri ya ccm ndio sheria kwa taasisi zote za serikali, wajinga zaidi ni NEC na watalaam wetu lindeni sheria sio kupokea lolote kutoka juu kwa maslahi yao binafsi mnatuharibia nchi.
 
CCM bhana sijui akili walishazipeleka wapi? Mahera anadai majina ya covid 19 yaliletwa na chadema ndio hayo aliyoyapeleka kwa Ndugai.

1. Mahera anadai CHADEMA iliwasilisha hayo majina tarehe 19 November 2020. Tarehe 20 Nov 2020 huyohuyo Mahera akiwa Azam tv alidai tume haijapokea majina ya viti maalumu kutokea CHADEMA. (Angalieni hizi tarehe mtaona nani muongo). Wanasema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu maana hii ni aibu.

2. Nusrat Hanje: tufanye basi ni kweli Mahera anasema ukweli kuwa Chadema iliwasilisha majina ya viti maalumu. Swali la kujiuliza: Nusrat Hanje alikuwa mahabusu, Chadema wana mamlaka gani nchi hii ya kuweka jina la Nusrat kwenye orodha ya viti maalumu na kuhakikisha wanamtoa mahabusu ili akaapishwe? Hapa ndio ninapowaona ccm either walishatuona watanzania hatuna akili au wao ndio hawana akili. Chadema ina mamlaka gani ya kumtoa mwanachama wake mahabusu ili awahi kuapishwa?

Ushauri wangu kwa chadema. Fungueni kesi mahakamani. Hii kesi ni rahisi sana kushinda. CCM imepanga huu mchezo kiboya sana.

Tunashukuru Nusrat Hanje ametoka mahabusu. Sasa dada wa watu yupo huru.
CCM wanajua kila mtu hana akili kama wanachama wao
 
Chadema muende mahakamani haraka sana kwa kuchafuliwa na NEC. Kuna jinai hapo. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu. Chadema, shikilieni hapohapo msiachie. Hii ni fursa ya kufunga goli.
 
Nilikuwa nawaza hivi hivi. Hata akili ya kuiba hawana. Tena wangepata na viti maalum kiulaini kabisa.. maana hao 50 lazima wangeenda bungeni, plus na viti maalum, leo wasingehaha kutafuta wabunge wa upinzani kwa kulazimisha hivi (mpaka kuapa garage jamani )!.

Tatizo kubwa ni kuwa anayefikiri na kutoa maamuzi ni mtu mmoja. Pengine anawashirikisha watu wawili watatu, ambao wote wanamuogopa huyo mtu. Hawawezi kumchallenge. Maamuzi yake hayo yanafanyiwa kazi bila kuhoji, kupinga wala kushauri vinginevyo. Hapo ndio tujue uwezo wa kufikiri wa bwana huyo. Kijani ikashinda kwa asilimia 98, uliona wapi akili ya hivi jamani!
Pia reasoning capacity yake ni low Sana ajui michezo.Nguvu kwanza fikra baadae.
Huwezi pinga utakosa shibe
 
DPP anatishia kupeleka watu gerezani. lakini DPP hasemi kwanini amevunja CPA, kifungu cha 91, Sura ya 20. Shauri lipo mahakamani, hakimu/Jaji ndio wanaweza kumtoa mtuhumiwa gerezani kwa remove order sio DPP (mlalamikaji). Nolle Prosequi inakutaka ueleze mahakama. Hukufanya hivyo.

Sheria haikupi mamlaka ya kumpeleka na kumtoa mtuhumiwa gerezani bila kibali cha mahakama. Ulichofanya kwa Nusrat ni mwendelezo wa kukanyaga sheria kwa kiburi tu. Umeweka bila kosa la msingi na umewatoa gerezani bila kufuata utaratibu. Kifupi umewakomoa, Nusrat kahongwa ubunge

DPP, ukisoma chapter 20, Section 91, CPA, part IV "Power of the DPP to enter nolle prosequi" haikupi mamlaka ya kumtoa mahabusu gerezani bila amri ya mahakama. Sheria inakutaka uieleze mahakama au kujulisha mahakama kwa maandishi kwa niaba ya Jamhuri. Hujafanya hivyo kwa NUSRAT.

Kwa utaratibu wa magereza Tanzania, wafungwa wanahesabiwa saa nane mchana, wanajiandaa kuingia selo saa tisa hadi saa kumi. DPP hana mamlaka ya kwenda gerezani kumtoa mahabusu au mfungwa saa moja na nusu usiku bila kibali cha mahakama kwa amei ya hakimu au Jaji. DPP hana mamlaka hayo, kisheria.

Kuhusu hilo la Freeman Mbowe, kwamba pamoja na wenzake, Mlimani City aliongoza kwa kuimba "Mungu ibariki Chadema" sehemu ya "Mungu ibariki Tanzania", kwanini iwe kosa kwa Mbowe sasa (ukitishia kumkamata) na iwe sio kosa kwa Nusrat hadi kuachiwa huru na mashtaka yake kufutwa?

Kama ulimkamata Nusrat kwa kosa hilo na ukamuacha iwe vipi halali kudhani Freeman Mbowe alitenda kosa hilo ambalo umelifuta kwa Nusrat na wenzake? UHALALI huo unatoka wapi? Kama Nusrat aliachiwa na kufutiwa mashtaka maana yake sio kosa, kwanini ulete stori nyinginezo.

Sio wajibu wa DPP kukamata watuhumiwa. Sio wajibu au jukumu la DPP kuwatoa watuhumiwa gerezani. DPP ni mwendesha mashtaka. Kusema "au na yeye (Mbowe) nimkamate?) ni kutishia raia kwa mamlaka ya ofisi yako. Sheria hazifuatwi. Tumeamua kufuata watu sio sheria.

DPP ni mlalamikaji katika kesi za jinai akiwakilisha Jamhuri. Mfungwa/mahabusu akiwa gerezani ni mali ya Gereza. Hakimu/Jaji wanaweza kumtoa gerezani kwa amri ya mahakama sio DPP. Katika mashauri ya Jinai, Jamhuri ni mlalamikaji. Kesi inafutwa na mahakama. Baada ya DPP kujiondoa.

DPP anasimama mbele ya vyombo vya habari anatamba kwamba "mimi ndie nimemtoa gerezani kwa mamlaka yangu" hadhi na mamlaka ya mahakama inapokwa na DPP. Kuirejesha nchi yetu kwenye misingi, lazima tuwaeleze hawa watu ukweli, sio "semi god".

Mamlaka ya mahakama imeporwa.

#MMM, Martin Maranja Masese
 
DPP anatishia kupeleka watu gerezani. lakini DPP hasemi kwanini amevunja CPA, kifungu cha 91, Sura ya 20. Shauri lipo mahakamani, hakimu/Jaji ndio wanaweza kumtoa mtuhumiwa gerezani kwa remove order sio DPP (mlalamikaji). Nolle Prosequi inakutaka ueleze mahakama. Hukufanya hivyo...
Uzi ulioenda shule. Hongera sana aliyetoa hizi nondo
 
Rais ajaye ajiandae kulipa fidia ya mabilion ya shilingi kwa watu walioumizwa na serikali hii ya mabavu

Niwazi kuwa wako watu wengi wamewekwa kizuizini kinyume na sheria siku nchi ikirudishwa kwa utawala wa sheria watakimbilia mahakamani kudai fidia zao
 
Back
Top Bottom