Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

Wewe utakuwa na watoto vilaza na wasiopenda shule ndio maana unawachongea watoto wanaopenda shule ili wawe vilaza kama wanao. Mimi mwanangu yupo shule binafsi na wanasoma hadi saa tatu usiku, wewe unalalamikia saa 12 jioni? PUMBAVU!!!!
Wacha uzushi, hakuna shule inayofundisha kuanzia saa 12 asbh mpk saa 3usiku hakuna iyo shule hata Ulaya hakuna.
 
Hili swali ndilo nalojiuliza...

Ila nishaelewa...hii ni kwa sababu WALIMU HAWA NI WALE WALIOPATA DIV 3 MPAKA 4...Kwahiyo tuseme hawana mbinu za ufaulu wenye tija...
Tatizo sio ufaulu wa div 3 au 4, mbona sisi tulifundishwa na Walimu pasipo Elimu( UPE) na tulifanya vema. Shida kubwa ipo kwenye mitaala na muda wa ub adilishwaji wa mitaala hiyo . Kila baada ya waziri kubadilishwa basi akiipata nafasi hiyo atabadili kulingana na anavyotaka yeye. Mwisho wa yote walimu wanakuwa incompetent na hayo mazauzau ya mamitaala ya kila leo,hivyo huzisha wanafunzi wahivyohivyo wanao faulu Dr's la 7 wanafeli kdt cha 2, wana faulu vema kdt cha 4 wanaenda feli kdt cha cha 6
 
Acha ubishi. Mwanangu anasoma mikocheni anatoka saa 2 usiku
Ss hapo ndio umerudi kule kule, kama anarudi saa 2ucku manaake anatoka saa 12 jioni na co eti anasoma kuanzia saa 12 asbh mpk saa 3ucku, haipo shule hyo.
 
Wewe pambana na hali yako sio ufuatilie maisha ya wenzako.Huu uzi sambaza mwenyewe kwa wenye mamlaka ,sisi hatuna muda mchafu.
 
Hapo kuna hoja kubwa na zenye nguvu umejitahid kuziainisha. Matarajio ni serikali ione namna ipi sahh ya kuideal hii issue,of course imegeuka kero.
Na bora km ni ada irejeshwe tu ili km wazaz tunalipa,heri tulipe na serikal ikae na jukumu la kuupangilia vzr mfumo wa elimu yetu.

Kuna shule moja hapa Ilemela-Mwz kata ya Buswelu,kila wiki mtoto anatakiwa kulipa tshs 4,000/=. Ukipiga hesab hiyo kwa mwaka utaona ni afadhali ada irejeshwe tu! Mbya zaid,matokeo hayajawah kubadilika saana zaidi ya watoto kupata ufaulu wa wastani wa B,C,D.

Ikiwa tatizo ni wingi wa watoto,tujenge madarasa na muajiri walimu wa kutosha km permanent solution.

Idara ya ukaguz wa elimu nayo najiuliza ipo kusaidia nin hasa? Au ni kugawana keki ya taifa tu?
 
Inaskitisha kwa kweli.. mwanafunzi wa darasa la 4 anarudi nyumbani saa 12 mpaka saa 1 usiku..
Mwanafunzi wa darasa la 7 anarudi nyumbani saa 3 hadi saa 4 usiku..

Hii ni elimu au upumbavu? Mtoto akirudi kachoka hapo pia atatakiwa ajiandae kwenda kesho yake shule.. saa 12:30 alfajiri anatakiwa awe ameshaingia darasani..
 
Huwa nikitoka jogging jioni nakutana na vitoto vya shule za serikali ndo vinatoka shule mida hio saa moja na robo hv. Huwa nahuzunika sana rohoni coz wanawekwa kwenye hatr ya kubakwa na kujifunza tabia mbaya.

Young students may be 10% of our population but they're 100% of our future. Serikali inbidi waangalie hili kwakweli
Nashindwa kuelewa hawa walimu wa sasa wana tatizo gani jamani????
Sijui ni uwezo mduchuu wa kufikiri???
 
ONGEZENI SAUTI wapate kusikia huko 'batani' walipo.
Nakumbusha tu, wajasiriamali kupitia Elimu waliopo bungeni walimdhihaki Ndalichako zama hizo, na sasa nasikia WAMEGOMEA KALENDA za masomo.
 
Back
Top Bottom