Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Kuna matatizo sehemu nyingi hapa.

Hata wazazi tuna matatizo pia.
  • Inakuaje mzazi unakaa 12 km kutoka shuleni kwa mtoto tena umepanga? kwa nini usipange karibu na shule ya watoto wako unaamua kupanga karibu na kazini kwako?
  • Kwa nini mzazi usimtafutie mtoto shule karibu na nyumbani. Kama kwa radius ya 5km na hapo unapokaa hakuna shule nzuri, basi umekosea mahali pa kupanga/kujenga.
  • Si lazima masomo yaanze saa 1 asubuhi kila shule. Ni kukariri tu. Shule zinaweza kuwa na masaa tofauti ya kuanza masomo.
  • Shule zibanwe ziwe na mabasi mengi ili route zisiwe za kuzunguka sana. Hii itasaidia kupunguza muda wa watoto kuwa njiani. Wenye shule wasipobanwa kwenye eneo hili hawawezi kujali maana ni mahali wanapobana matumizi.
  • kama kwenye eneo moja kuna watoto wa shule moja wengi wazazi wanaweza ku opt kutolipia basi la shule wakatafuta usafiri wao wenyewe. Kuna mahali wazazi wamekodi noah inachukua watoto asubuhi na kuwarudisha jioni, badala ya basi la shule. Wanatumia pesa nyingi zaidi lakini kwa manufaa ya watoto wao
Kama hamna namna basi walau mtoto alale mapema ili apate masaa mengi ya kupumzika. Usimwache akaangalia tamthilia mpaka saa 4 usiku.
 
Imekaaje hii

Saa 11:20 alfajiri Unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni.

Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,

-Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
-Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
-Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?

Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote Ni wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA
Hii maadaa nimeitupia kwenye group langu la WhatsApp la Wazazi na Walimu shuleni kwa wanangu,na mchezo huo nao wanao maana shule yao inaanzia hizo age za 4 na 6! Bado nasikilizia majibu kutoka huko!!
 
Wengine wanaona ujanja mtoto miaka miwili anaanza kupelekwa day care..principle yangu ni mtoto akae home awajue siblings, ajue viumbe vya dunia, atembee ahave fun, ajue milima mito na bahari, ajue abc -z akiwa home, 1 to 100 akiwa home.. alale, acheze, ale.

Nursery nataka asome mwaka mmoja tu..sitaki kuskia ya baby class, kg 1, kg 2, pre grade 1 ..Halaf baada ya hapo ndo agraduate aende class 1 lol..watu wanafanywa mtaji
 
Huu wa kusuka Watoto na kuwakaza vichwa Ni unyanyasaji mwingine was watoto?

Kiukweli hawatendewi haki.

Tunakuja kutengeneza taifa la akili fyatu kwa mikono yetu wenyewe.

Inasikitisha Sana mkuu
Ndio mkuu, zile nywele za uzi zinauma sana wanawake wanajua, usipopaka dicloper ya tube kichwani siku ukisuka hulali na hua inaleta vipele na vidonda.

Sasa mtoto wa miaka minne anajazwa minywele ya uzi ya nini? anatafuta nini?

Watoto ni warembo na wazuri bila hata huo upuuzi wa minywele, kuzutwa zutwa kichwa na wasusi kunaleta mtoto anakomaa liuso kama mtu mzima, mtoto mpige kipara daily aoge had kichwani, ni dawa na inaleta kurelax, sasa na hili joto mtoto haogi kichwa mwezi.

Ningekua waziri wa elimu au rais ningepiga marufuku wanafunzi kusuka, wanasuka ili iweje kwamfano?
 
wengine wanaona ujanja mtoto miaka miwili anaanza kupelekwa day care..principle yangu ni mtoto akae home awajue siblings, ajue viumbe vya dunia, atembee ahave fun, ajue milima mito na bahari, ajue abc -z akiwa home, 1 to 100 akiwa home.. alale, acheze, ale. nursery nataka asome mwaka mmoja tu..sitaki kuskia ya baby class, kg 1, kg 2, pre grade 1 ..alaf baada ya hapo ndo agraduate aende class 1 lol..watu wanafanywa mtaji
Sasa mtoto mwa miaka 2 anapelekwa shuleni kufanya Nini kama sio upigaji huu

Uyu mtoto SI bado anajinyea?
 
Ndio mkuu, zile nywele za uzi zinauma sana wanawake wanajua, usipopaka dicloper ya tube kichwani siku ukisuka hulali na hua inaleta vipele na vidonda. Sasa mtoto wa miaka minne anajazwa minywele ya uzi ya nini? anatafuta nini? Watoto ni warembo na wazuri bila hata huo upuuzi wa minywele, kuzutwa zutwa kichwa na wasusi kunaleta mtoto anakomaa liuso kama mtu mzima, mtoto mpige kipara daily aoge had kichwani, ni dawa na inaleta kurelax, sasa na hili joto mtoto haogi kichwa mwezi.
Ningekua waziri wa elimu au rais ningepiga marufuku wanafunzi kusuka, wanasuka ili iweje kwamfano?
Kina mama (wake zetu) Nadhan ndo mashabiki wa huu upuuzi,

ifike mahala tutumie akili badala ya kuwaza ujinga.

Tukiendelea hivi usishangae Watoto hao wameanza kupakwa mikorogo na kuvalishwa mawigi
 
Au vinafikia kwenye tv vinakutana na vikatuni vya Tom and Jerry! Mbona ndiyo vitakodoa macho hadi saa 12 jioni ndiyo kanaanza kusinzia huku homework ikimsubiria!!!
Badala ya kumjenga mtoto Unakua unamharibu
 
Wazazi ndiyo tuna shida zaidi maana watoto kwa umri huu wa miaka 4 hufuata kile Wazazi tunawaamulia.
KABISA,
Hapa Inabidi wazazi waingilie Kati.

This is not fair, tunaharibu Watoto wetu kwa kuendekeza upuuzi wa watanionaje Mimi.
 
Imekaaje hii

Saa 11:20 alfajiri Unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni.

Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,

-Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
-Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
-Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?

Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote Ni wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA
Imekaaje hii

Saa 11:20 alfajiri Unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni.

Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,

-Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
-Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
-Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?

Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote Ni wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA
Imekaaje hii

Saa 11:20 alfajiri Unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni.

Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,

-Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
-Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
-Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?

Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote Ni wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA
Mkuu pole sana kwa taarifa yako hao watoto sio miaka 4 kama unavyosema hao ni watoto wa miaka miwili na nusu hadi mitatu na minne na walipaswa kupelekwa kwenye day care lakini wanapelekwa mashuleni wakafundishwe.

Wazazi wa siku hizi hawana akili hawajali tena usalama wala lishe bora kwa mtoto wanachotaka ni mtoto afundishwe tu yaani mtoto akijua tu kuongea basi anakimbizwa kwa mwalimu.

Huko mwanzo watoto wa miaka 2 hadi 4 walikuwa wanashinda kwenye day care yaani vituo vya kulelea watoto mchana ili wapate uji na chakula na pia wapate muda wa kucheza kidogo au malezi changamshi mwisho wapate muda wa kulala .

Cha ajabu wazazi hawajui hilo tena wanawatesa watoto kuwapeleka kwenye mashule ya mbali huku wengine wakishinda njaa mashuleni na kubebeshwa mabegi ya madaftari huu ni ukatili kwa mtoto.

Siku hizi si ajabu tena unakutana na watoto wa miaka miwili eti wametoka shule za vichochoroni wengine wanajiita tuition wakati ni darasa kabisa lenye ubao.kibaya zaidi mtoto wa kike bado anajipupulia sasa mwalimu ni wa kiume anamtawazaje huyo mtoto?

Je siku mwalimu akiamua kumbaka? Ukweli hali ya sasa inatisha shule zimekuwa nyingi mno chekechea vituo ni vingi kuliko hata hizo day care na hizo chekechea au nursery nyingi hazina usajili na zipo katika mazingira hatarishi.

Kuna haja ya wizara ya elimu na wizara ya Ustawi wa jamii kukaa pamoja na kutenganisha hawa watoto kwa umri wajulikane wa shule ni kuanzia umri gani tusipokuwa makini baadaye watoto wetu watadumaa akili na mwili au kupata madhara Mkubwa ya kiafya huko mbeleni kwakuwa watoto wadogo hawapati lishe bora tena kwakuwa wanaamshwa asubuhi na mapema kuwahishwa shuleni.

Hivi mtoto wa miaka miwili kwenye school bus ya SAA 12 asubuhi anaenda kusoma nini shuleni? Huyu sialipaswa ashinde nyumbani na msichana wa kazi au kwenye day care?

Serikali ifuatilie hili jambo huu ndio mwanzo wa msingi mbovu wa elimu.

Asante
 
Back
Top Bottom