Rwandair kuongeza ndege mbili (2) brand new CRJ 900 kutoka kiwandani

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Sipendi kupepesa macho wala kumumunya maneno pale panapotakiwa kupongeza
nimesoma gazeti moja la rwanda habari hii ikanifurahisha kwa kweli sipendi kujua nini kinaendelea bali nichukue fursa hii kumpongeza hon rais kagame na wanyarwanda wote wanaompa sapoti wakati huu akiwa madarakani ....

0ct 18 .2012 kampuni ya ndege ya rwanda inaratajia kuleta ndege zake mbili crj900 brandnew kutoka kiwandani moja itawasili 18oct na nyingine 21 nov ..napenda kuwapongeza wote wanaoshiriki kusapoti nchi hii na bila kusahaau wale watoto watarajiwa

naomba tujifunze na tujiulize hivi hawa ndege zao zote wanaleta kutokakiwandani sie tuna madini tuna makaa ya chuma mawe makaa ya mchanga na mengineyo tunashindwa nini kununua viwandani na kukimbilia kwenye ma used na kuishia kulipa madeni ya miakataba kwa kukodisha ndege mbofu mbofu?/

eeh yesu tusaidie
 

Attachments

  • pic 1.JPG
    pic 1.JPG
    149.2 KB · Views: 130
  • pic 3.JPG
    pic 3.JPG
    172.1 KB · Views: 131
  • pic 4.JPG
    pic 4.JPG
    198.4 KB · Views: 105
kama mnavyoiona picha mbili za mwisho ndege moja iko tayari krushwa na nyingine pembeni wakimalizia ili kuja kukukamua ewe mwananchi uweze kusapoti kwa kuruka na Rwandair
 
mkuuu hapo ndipo unapoona tunahitaji raisi na viongozi makini kama kagame, mbali ya madhaifu yake kama binadamu, bvita nakadhalika, lakini hawa jamaa sasa wameamua kupiga kazi sawa ni nchi ndogo sana lakini wanaonekana kweli wamedhamiria kuondoka katiak umaskini, sisi tuna kila kitu anzia, milima mabonde, mbuga za wanyama adimu duniani, madini ya kila aina, dhahabu, almasi, chuma, gesi, makaa ya mawe, ulanga, copper, mafuta na kadhalika lakini hatuna hata ndege ya maana katika ATCL.. na viongozi wapo wao wanapiga kelele inchi inaendelea.. kwakweli lazima sisi kama wananchi lazima tufanye kitu, watu wanaiba mabilioni leo ni mawaziri, sheria, na mahakama zipo, polisi wapo wana kenua meno.. wao wasikie wapinzani wanaaandama tu basi wamefika kulipua mabomu... kwakweli tz tuansikitishajambo la ajabu zaidoi, babu zetu amabao hawakuwa na masters wala phd, walituachia uchumi imara sana, viwanda visivyopungua 150 vikiongeza thamani ya mazao yenu ya pamba, katani, korosho, katani, chai na kadhalika, leo miaka 50 tangu tumepata uhuru tumeua kila kitu na ma phd, na mamasters runayo.... labda tz tumelongwa siyo bure...unawezaje kuendelea bila viwanda?? hongera zao Rwanda
 
haahaaaa facilitator
oRIGIN YAKE HIYO MKUU BAGAMMOYO KAZI YENYE MSHAHAR AMKUBWA KUPIGA NGOMA
 
haahaaaa facilitator
origin yake hiyo mkuu bagammoyo kazi yenye mshahar amkubwa kupiga ngoma

mbona sisi tunamabasi yaendayo kasi, tunatren kama daladala, tuna meli kama daladala
 
Precisionair wana ndege 11, si ni Watanzania???
nasema hivi kwa kuweka ukweli sawa kuwa deterioration ya nchi hii imechukua karibia miaka 20 na endapo tukiwa serious enough, 'healing' process inaweza kutuchukua miaka sio chini ya saba.
Hivyo badala ya kutegemea serikali imiliki ndege ni bora hilo tukalisahau. Mijizi na mizembe iliyojaa huko inabidi ife kwanza maana ungesema ione huruma na kubadilika sidhani kama hilo linawezekana.
Ndio maana nasema tuiangalie Precisionair japo nayo umiliki wake una utata lakini inapeperusha bendera yatu.
Hongera rais Kagame
 
mbona sisi tunamabasi yaendayo kasi, tunatren kama daladala, tuna meli kama daladala
ongeza na daraja la Kigamboni ambalo linajengwa na WAFANYAKAZI wa Tanzania ambao wengi wao hata nyumba za kuishi hawana lakini nasikia wengine wanasema ni jk!!
 
TUNAHITAJI RAIS DIKTETA ASIEKUWA NA MZAHA WA RASILIMALI ZETU NA ASIEKUWA NA HURUMA KWA YEYOTE ANAEFISADI UCHUMI WETU.nimeangalia CCM, CUF, TLP,sijaona nadhani dr Slaa anaweza
 
ongeza na daraja la kigamboni ambalo linajengwa na wafanyakazi wa tanzania ambao wengi wao hata nyumba za kuishi hawana lakini nasikia wengine wanasema ni jk!!

mkuu siasa za bongo ngumu kweli ukiwa raisi bongo wewe ni kuku kwa mlija tuu!
 
Safi sana if zitakuwa na tija kwetu mfano punguzo la nauli maana wale precision air kwa kweli nauli zao zipo juu huku ATC any time cancellation.
 
mkuu haya matusi sasa!
Tuoneshe mambo makubwa ambayo Rais wetu anafanya na haitokuwa matusi kwenye ngoma kama hizi.Tupe mradi ambao JK katoa hela serikalini na si kwa mkopo kutoka sehemu yoyote wala pesa za mifuko ya jamii.
 
Back
Top Bottom