RwandAir Haoooo!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
SHIRIKA la Ndege la Rwanda (RwandAir) linatarajia kuzindua rasmi safari zake za ndege za kutoka Dar es Salaam kupitia Bujumbura kuanzia kesho.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi yake iliyoko jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa huduma hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

“Asubuhi saa moja muda wa Rwanda ndege zitaondoka kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kigali kila siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili pia zitaondoka Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa tano asubuhi kwenda moja kwa moja Kigali,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa shirika hilo la ndege linakusudia kuongeza zaidi njia na safari zake mara itakapokamilisha ununuzi wa ndege aina ya Boeing 767 na 737-800 Machi.

“Muda si mrefu tutatoa ofa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia 2010 mara tutakapoanza safari za moja kwa moja kutoka Kigali kwenda J’Burg Afrika ya Kusini,” iliongeza taarifa hiyo.

Chanzo: Tanzania Daima

My Take:
I remember them day; Serengeti yetu ikitua Bujumbura!
 
Ni aibu sana kutokuwa na national flag carier aibuu ukienda airport za east and central africa...utakuta ndege za kila nchi tena nchi ndogo ndogo ila si tanzania sisi tunaitwa wapiga siasa!!!
 
Kwa utawala wa Kagame watafanikiwa sana! Naamini wana kiu ya maendeleo, sio njaa ya kujaza matumbo!!
 
Tanzania Daima

SHIRIKA la Ndege la Rwanda (RwandAir) linatarajia kuzindua rasmi safari zake za ndege za kutoka Dar es Salaam kupitia Bujumbura kuanzia kesho. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ofisi yake iliyoko jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa huduma hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
“Asubuhi saa moja muda wa Rwanda ndege zitaondoka kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kigali kila siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili pia zitaondoka Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa tano asubuhi kwenda moja kwa moja Kigali,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo, taarifa hiyo iliongeza kuwa shirika hilo la ndege linakusudia kuongeza zaidi njia na safari zake mara itakapokamilisha ununuzi wa ndege aina ya Boeing 767 na 737-800 Machi.
“Muda si mrefu tutatoa ofa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia 2010 mara tutakapoanza safari za moja kwa moja kutoka Kigali kwenda J’Burg Afrika ya Kusini,” iliongeza taarifa hiyo.

My Take:
I remember them day; Serengeti yetu ikitua Bujumbura!

Pale KIA nafikiri wanatua kila siku na walianza muda mrefu kidogo
 
Honorable Kagame is bringing real change in Rwanda. May God give him more strengths so he see his plans accomplished for the people of Rwanda. Yangu macho mie katka Jumuiya ya Afrika Mashariki. May Rwanda show Tanzania the way forward. :D
 
Kagame anajua kilichomleta Duniani na hana utani hata kidogo.
 
Sisi si tumekalia kuuza sura tu!! Safari nyingi sizizo na manufaa kwa nchi. sana sana zinakula fedha zetu tu. Hongera Kagame.
 
You know what.. screw Tanzanian politics for a minute.. I'm gonna learn what Rwanda is doing right.
 
Hii Safi. Taratibu dominance ya KQ itapungua na hivyo bei kupungua pia.

Shirika letu vipi jamani? tatizo pale ni management, vitendea kazi, fedha au kitu gani? siamini kama ni fedha za uendeshaji, maana tunaweza pia kukopwa na Bank kuu au Kagodas
 
Hongera watu wa Rwanda,hongera sana kagame,hayo ndio mambo yanayotakiwa hata kama maendeleo ya Rwanda yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na wizi wa rasilimali za CONGO ya Jose Kabila uliofanikishwa kwa kiasi kikubwa na Mkongoman mtutsi Laurent Nkunda,lakini mwisho wa siku ni kwa manufaa ya Rwanda kama nchi si viongozi wa Rwanda binafsi hapo ndipo wanapotofautiana na hawa watawala wetu ambao wanatuibia sisi kwa hayo marichmond na ma iptl yao,kagame anaiba kuijenga Rwanda kwa kuwa Rwanda Haina Rasilimali nyingi kama sisi.
 
Kuna Post nimetoa leo inaitwa "Time for Tanzania to wake up from Aviation Slumber" kwenye sehemu ya Biashara na Uchumi. Someni msikie Mawazo ya Mrs. Munyagi wa Tanzania Civil Aviation Authority.
 
Thanks God, Kenya Airways na Ethiopian walikuwa wanatuibia!!!!!!!! wezi wakubwa. Sasa ushndani utapunguza bei.
Lakini jamani mbona mnaimba sana eti Rwanda imeendelea? Nani kaenda kule?
Mjomba, nikipata nauli ntaenda Kigali na Rwanda air. Nione kama kweli hizo nyimbo ni kweli au mnaimba vibwagizo vya nyimbo msizojua. Sidhani kama Rwanda imeendela kama Tanzania, sidhani kama Kigali ni nzuri kama DSM.

Mwenye pesa anasaidie niende, ntawajuza nitakachokiona. Plese JM lazima mtu aende
 
Back
Top Bottom