Rwanda yatuhumiwa 'kupika' takwimu za uchumi kwa manufaa ya kisiasa

Kuanzia kupiga watu marisasi kitu ambacho ni kigeni hapa kwetu Tz.
Na kuchakachua data.
Vyote anatoa kwa dikteta Kagame.

Na atabadilisha katiba ili aendelee kutawala milele.
Wapiga ranli wake wapo stand by.

Na alishasema pale eapoti kuwa watakaokuja wataweza?

Yani anajiona anajua wakati yeye ndio worse presidente kuliko wote.

Bodi ya mikopo tu anatunyonga then anajiona awatu wanafurahia?

Aisee.
Kwenye tawala zote duniani hata ukiwa wewe ni Rais leo unayolalamikia hapa yanafanyika nchi zote. Tofauti tu ni approach ya jinsi yanavyofanyika na inteligencia yake.

Sipingi hoja yako na pia uko sahihi kulalamika ila usiwaze kwa JPM tu waza hata tawala zingine na zingine utakuwa huru kuishi Maisha yako.
 
Kumbe Gisenyi ipo pwani?
Ukiona Mwanaume kama Wewe anawashwawashwa hivi kwa Sisi tuliozaliwa na kukulia Mikoa hii ya Pwani tunajua kuwa ana tatizo au kuna ' Mmimino ' fulani Mlaini na Mtamu anauhitaji ila anashindwa tu kuweka wazi au kujieleza ili wale ' Wamiminaji ' wamtunuku nao.
 
Jarida la Financial Times (FT) linaripoti kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu limegundua kuwa nchi ya Rwanda imekuwa ikichakachua takwimu zake za umasikini nchini humo, ikumbukwe kuwa France24 ilisharipoti mwaka 2015 kuwa serikali ya Kagame inachakachua takwimu zake za uchumi.

Uchakachuaji mkubwa zaidi ulifanyika mwaka 2015 punde kabla ya kura ya maoni iliyomwongezea Kagame (ambaye alishakuwa madarakani kwa miaka 15) muda wa kukaa madarakani kwa miaka mingine karibu ishirini! katika mazingiza hayo Kagame alikataa katakata kukubali takwimu zilizo onesha kuwa umasikini unaongezeka nchini Rwanda.

FT pia lilichapisha kwa mara ya kwanza barua ya ndani ambayo wafanyakazi watano wa benki ya dunia waliwaandikia viongozi wa taasisi hiyo mwaka 2015, katika barua hiyo wafanyakazi hao walilalamikia kile walicho kiita "uchakachuaji wa takwimu na kushindwa kwa Rwanda kutoa data za uhakika kwa uwazi", pia waliendelea kuandika kuwa "kile kilichokua kinaendelea kilikua na hatari ya kuichafua heshima ya benki ya dunia ikiwa nchi ya Rwanda itaendelea na mchezo wake".

View attachment 1180958

My take: naona kila siku mambo yanazidi kujijidhihirisha kuwa ni wapi mheshimiwa wetu anachota 'idea' zake za ajabuajabu na zisizo za kitanzania.
Yaani Tanzania imekongoroka kiasi cha kuanza kuiga uchafu wa nchi duni ya Rwanda !
 
Wakati ukikimbilia kuwashwawashwa na mambo ya ndani ya Rwanda tunaomba pia utuhakikishie kama hata nchi yako ya Tanzania nayo haipiki data zake katika mambo yake mbalimbali ya Kimaendeleo. Ukiachia mbali hao Wazungu ambao hawajaanza Chuki zao na Rais Kagame leo ila kwa wenye Akili tunatambua kuwa Rwanda ya sasa chini ya Kagame imepiga hatua nyingi ukilinganisha na ilivyokuwa japo nakiri kuwa bado kuna Changamoto kadhaa za Kidemokrasia na Kisiasa ila Rais Kagame amejitahidi na yapo Maendeleo kadhaa utayakuta nchini Rwanda ambayo ilichafuka Kimapigano ( Mauaji ya Halaiki ) zaidi ya mara mbili katika Historia ambayo huwezi kuyakuta nchini Tanzania ambako wanajinasibu kuwa ni Baba wa Amani Afrika kama siyo duniani. Halafu ni Upumbavu uliopitiliza kila mara Kuhusisha Mapungufu ya Rais JPM Kiuongozi na Kisiasa na Urafiki wake na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Kuna Watu mnajiita Wasomi lakini arguments zenu haziakisi hivyo na si ajabu ndiyo maana hata Elimu ya nchini mwenu ina Changamoto Kubwa kama siyo nyingi.
Nimefurahia tu kiswahili safi sana toka Rwanda, inaelekea "Shem" hakuna shida ya mawasiliano . Dada zako wazuri wanatupagaisha sana..
 
Bado hujajibu Hoja yangu na huenda haya Majibu yako yanathibitisha kuwa Wewe ni ' Kichwa Maji ' na ndiyo maana umenijibu Kitoto mno. Nakuuliza tena je hayo unayodai kuwa yanafanyika nchini Rwanda hapa Kwenu Tanzania hayafanyiki au hayajazoeleka? Hivi kuna kinachoweza Kufanyika nchini Rwanda halafu kiwe ama hakifanyiki au hakijawahi Kufanyika nchini Tanzania au katika nchi nyinginezo za Afrika? Na ni kwanini Urafiki wa Rais JPM na PK Kwenu nyie ni tatizo? Hata kama mnawasema kutokana na Changamoto zao je unataka kusema hakuna Mambo mengine mazuri na ya Kimaendeleo ambayo Tanzania inaweza Kuiga kutoka Rwanda na Rwanda inaweza Kuiga kutoka Tanzania? Nasubiri Jibu lako ili nizidi Kukudharau.
Kuiga chochote kutoka Rwanda, kumeleta matatizo makubwa ambayo hatujayazoea na hayazoeleki.
 
Ndugu yangu umewahi kufika Rwanda? Au unaongea kwa kunukuu hao wapuuzi wa FT na France24? Rais Kagame ameijenga nchi ile kwa muda mfupi sana. Ni nchi iliyopiga hatua kubwa sana baada ya Genocide against the Tutsi. RPF wamechukua nchi ikiwa haina uchumi kabisa. Sasa uchumi unakuwa kwa asilimia kati ya 7 na 8. Halafu mnasema kapika data?? Chanzo chenu ni FT, France24 ambao wao wanasikiliza detractors like Dr Himbara and others ambao wanasema lolote ili mradi kuwafurahisha mabwana zao walikokimbia uhamishoni. France24 hawa hawa waliokuwa wanaitwa "french Hutu" na interahamwe murderers?? Leo mnawapa credibility ya kuongelea progress ya Rwanda?? Exiles always slant what they say to suit their hosts' narrative. Usiamini upuuzi huu. Tembea Rwanda ujionee halafu uje uongee hapa.
 
Ndugu yangu umewahi kufika Rwanda? Au unaongea kwa kunukuu hao wapuuzi wa FT na France24? Rais Kagame ameijenga nchi ile kwa muda mfupi sana. Ni nchi iliyopiga hatua kubwa sana baada ya Genocide against the Tutsi. RPF wamechukua nchi ikiwa haina uchumi kabisa. Sasa uchumi unakuwa kwa asilimia kati ya 7 na 8. Halafu mnasema kapika data?? Chanzo chenu ni FT, France24 ambao wao wanasikiliza detractors like Dr Himbara and others ambao wanasema lolote ili mradi kuwafurahisha mabwana zao walikokimbia uhamishoni. France24 hawa hawa waliokuwa wanaitwa "french Hutu" na interahamwe murderers?? Leo mnawapa credibility ya kuongelea progress ya Rwanda?? Exiles always slant what they say to suit their hosts' narrative. Usiamini upuuzi huu. Tembea Rwanda ujionee halafu uje uongee hapa.

Kagame ameijenga nchi hiyo, je hali halisi za wananchi wake kiuchumi zikoje? Kuna uwiano wa kimaisha baina ya wananchi na hiyo miundo mbinu?
 
Kagame ameijenga nchi hiyo, je hali halisi za wananchi wake kiuchumi zikoje? Kuna uwiano wa kimaisha baina ya wananchi na hiyo miundo mbinu?
Rais Kagame ameweza kuimarisha maisha ya wanyarwanda wa kawaida kwa kiasi kikubwa sana. The living standard has doubled under PK.
 
Wazungu hawezi kusifia hata siku moja. Wazungu na Developing Countries wako kama CCM na CDM. Chochote unafanya lazima watupie jicho.
Walihangaika sana na China lakini China haikuangalia Nyuma na leo ndio namba 2.
Hao wazungu ni wa kuwapuuza ndipo tutasonga la sivyo watatutoa kwenye msitari.

China did, we can too.

Mstari gani uliopo?
 
Wakati ukikimbilia kuwashwawashwa na mambo ya ndani ya Rwanda tunaomba pia utuhakikishie kama hata nchi yako ya Tanzania nayo haipiki data zake katika mambo yake mbalimbali ya Kimaendeleo. Ukiachia mbali hao Wazungu ambao hawajaanza Chuki zao na Rais Kagame leo ila kwa wenye Akili tunatambua kuwa Rwanda ya sasa chini ya Kagame imepiga hatua nyingi ukilinganisha na ilivyokuwa japo nakiri kuwa bado kuna Changamoto kadhaa za Kidemokrasia na Kisiasa ila Rais Kagame amejitahidi na yapo Maendeleo kadhaa utayakuta nchini Rwanda ambayo ilichafuka Kimapigano ( Mauaji ya Halaiki ) zaidi ya mara mbili katika Historia ambayo huwezi kuyakuta nchini Tanzania ambako wanajinasibu kuwa ni Baba wa Amani Afrika kama siyo duniani. Halafu ni Upumbavu uliopitiliza kila mara Kuhusisha Mapungufu ya Rais JPM Kiuongozi na Kisiasa na Urafiki wake na Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Kuna Watu mnajiita Wasomi lakini arguments zenu haziakisi hivyo na si ajabu ndiyo maana hata Elimu ya nchini mwenu ina Changamoto Kubwa kama siyo nyingi.

Huyu mnyarwanda anayeishi tanzania. We jamaa we ni mkimbizi
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom