Rwanda yatuhumiwa 'kupika' takwimu za uchumi kwa manufaa ya kisiasa

Wanasahau kuwa pembe la ngo'mbe daima halifichiki
Jarida la Financial Times (FT) linaripoti kuwa baada ya uchunguzi wa muda mrefu limegundua kuwa nchi ya Rwanda imekuwa ikichakachua takwimu zake za umasikini nchini humo, ikumbukwe kuwa France24 ilisharipoti mwaka 2015 kuwa serikali ya Kagame inachakachua takwimu zake za uchumi.

Uchakachuaji mkubwa zaidi ulifanyika mwaka 2015 punde kabla ya kura ya maoni iliyomwongezea Kagame (ambaye alishakuwa madarakani kwa miaka 15) muda wa kukaa madarakani kwa miaka mingine karibu ishirini! katika mazingiza hayo Kagame alikataa katakata kukubali takwimu zilizo onesha kuwa umasikini unaongezeka nchini Rwanda.

FT pia lilichapisha kwa mara ya kwanza barua ya ndani ambayo wafanyakazi watano wa benki ya dunia waliwaandikia viongozi wa taasisi hiyo mwaka 2015, katika barua hiyo wafanyakazi hao walilalamikia kile walicho kiita "uchakachuaji wa takwimu na kushindwa kwa Rwanda kutoa data za uhakika kwa uwazi", pia waliendelea kuandika kuwa "kile kilichokua kinaendelea kilikua na hatari ya kuichafua heshima ya benki ya dunia ikiwa nchi ya Rwanda itaendelea na mchezo wake".

View attachment 1180958

My take: naona kila siku mambo yanazidi kujijidhihirisha kuwa ni wapi mheshimiwa wetu anachota 'idea' zake za ajabuajabu na zisizo za kitanzania.
 
Wakati ukikimbilia kuwashwawashwa na mambo ya ndani ya Rwanda tunaomba pia utuhakikishie kama hata nchi yako ya Tanzania nayo haipiki data zake katika mambo yake mbalimbali ya Kimaendeleo. Ukiachia mbali hao Wazungu ambao hawajaanza Chuki zao na Rais Kagame leo ila kwa wenye Akili tunatambua kuwa Rwanda ya sasa chini ya Kagame imepiga hatua nyingi ukilinganisha na ilivyokuwa japo nakiri kuwa bado kuna Changamoto kadhaa za Kidemokrasia na Kisiasa ila Rais Kagame amejitahidi na yapo Maendeleo kadhaa utayakuta nchini Rwanda ambayo ilichafuka Kimapigano ( Mauaji ya Halaiki ) zaidi ya mara mbili katika Historia ambayo huwezi kuyakuta nchini Tanzania ambako wanajinasibu kuwa ni Baba wa Amani Afrika kama siyo duniani. Halafu ni Upumbavu uliopitiliza kila mara Kuhusisha Mapungufu ya Rais JPM Kiuongozi na Kisiasa na Urafiki wake na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Kuna Watu mnajiita Wasomi lakini arguments zenu haziakisi hivyo na si ajabu ndiyo maana hata Elimu ya nchini mwenu ina Changamoto Kubwa kama siyo nyingi.
Naona ndugu yetu michombero wabongo wamekugusa
 
Na Rwanda kwa sasa ndiyo nchi pekee Inatumia misaada kutoka kwa wahisani na kuirudisha huko ulaya kuidhamini Arsenal
tuuwie radhi ndugu yetu kutoka Rwanda, huku Tanzania tumeshazoea uhuru wa kutoa maoni na kusema ukweli hata kama utamuumiza kiongozi mkuu, wewe kama mnyarwanda nadhani huwezi kulitambua hilo kwa namna Kagame anavyowajaza propaganda.
Argument kuu hapa ni serikali ya kagame kupika takwimu ili kujinufaisha kisiasa na pia ili kuwapotosha nchi wahisani, kumbuka kuwa Rwanda ni moja ya wapokea misaada wakubwa zaidi barani Africa, kutokea 1994 benki ya dunia pekee imetoa zaidi ya dola bilioni nne kwa Rwanda.
 
Mungu aepushie mbali kabisa
anaiga vitu vingi sana kutoka kwa huyo jamaa, sijui hata usalama wetu ukoje kwa sababu kipindi cha JK ambapo tulikua tunawabana kiasi lakini bado kuna majasusi wa kinyarwanda walikua wanapenya hadi sehemu nyeti kabisa za nchi tena kwa muda mrefu, sasa hivi leo inawezekana hata hawajifichi wanarandaranda tu kwenye korido za jumba jeupe.
 
Bado hujajibu Hoja yangu na huenda haya Majibu yako yanathibitisha kuwa Wewe ni ' Kichwa Maji ' na ndiyo maana umenijibu Kitoto mno. Nakuuliza tena je hayo unayodai kuwa yanafanyika nchini Rwanda hapa Kwenu Tanzania hayafanyiki au hayajazoeleka? Hivi kuna kinachoweza Kufanyika nchini Rwanda halafu kiwe ama hakifanyiki au hakijawahi Kufanyika nchini Tanzania au katika nchi nyinginezo za Afrika? Na ni kwanini Urafiki wa Rais JPM na PK Kwenu nyie ni tatizo? Hata kama mnawasema kutokana na Changamoto zao je unataka kusema hakuna Mambo mengine mazuri na ya Kimaendeleo ambayo Tanzania inaweza Kuiga kutoka Rwanda na Rwanda inaweza Kuiga kutoka Tanzania? Nasubiri Jibu lako ili nizidi Kukudharau.
Wauwaji ya kimbari yaliyo tokea Rwanda hayaja wahi kutokea Tanzania na kamwe hayatakuja kutokea pamoja na changamoto nyingi tulio nazo.

Hivyo wala usipende kuilinganisha nchi yetu pendwa na Rwanda
 
Naona ndugu yetu michombero wabongo wamekugusa

Ni lini nilikuthibitishia au UHAMIAJI walikuthibitishia pasi na shaka kuwa Mimi siyo Mtanzania mwenzako upande nikiwa ni Mzaramo na mwingine nikiwa ni Mluguru? Kumbe Siku hizi Wazaramo na Waluguru siyo Watanzania bali ni Wanyarwanda?

Cc: Frank Wanjiru
 
Wauwaji ya kimbari yaliyo tokea Rwanda hayaja wahi kutokea Tanzania na kamwe hayatakuja kutokea pamoja na changamoto nyingi tulio nazo.

Hivyo wala usipende kuilinganisha nchi yetu pendwa na Rwanda

Bado hujajibu vyema Swali na naona unatangatanga tu hovyo kama Inzi wa Maliwatoni. Nakuuliza tena je Siku hizi nchini Tanzania Watu wa Makabila yangu Mawili ya Kiasili ya Zaramo na Luguru siyo Watanzania na wamegeuka rasmi kuwa ni Wanyarwanda kutoka nchini Rwanda? Nasubiri jibu langu tafadhali.
 
Kuanzia kupiga watu marisasi kitu ambacho ni kigeni hapa kwetu Tz.
Na kuchakachua data.
Vyote anatoa kwa dikteta Kagame.

Na atabadilisha katiba ili aendelee kutawala milele.
Wapiga ranli wake wapo stand by.

Na alishasema pale eapoti kuwa watakaokuja wataweza?

Yani anajiona anajua wakati yeye ndio worse presidente kuliko wote.

Bodi ya mikopo tu anatunyonga then anajiona awatu wanafurahia?

Aisee.
 
Kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake huko

Ukiona Mwanaume kama Wewe anawashwawashwa hivi kwa Sisi tuliozaliwa na kukulia Mikoa hii ya Pwani tunajua kuwa ana tatizo au kuna ' Mmimino ' fulani Mlaini na Mtamu anauhitaji ila anashindwa tu kuweka wazi au kujieleza ili wale ' Wamiminaji ' wamtunuku nao.
 
Mnalazimisha siasa za kijamaa hapa Tanzania kwenye kizazi hiki, lakini ukweli ni kuwa ujamaa sio formation inayoendana na mahitaji ya kizazi hiki. Hiyo kulazimisha ndio maana unaona nguvu kubwa zinatumika kulazimisha hali hiyo ikiwemo kuchezea box la kura ili kujaza wanaccm kwenye uongozi, watakaoungana mkono chochote atakacho Magufuli ambaye bado anaamini kwenye siasa za ujamaa. Ukweli ni kuwa siasa za ujamaa zilifail toka enzi za Nyerere, na siku Magufuli anatoka madarakani kesho yake asubuhi mambo yake mengi yatafutiliwa mbali.
Ndugu yangu nakushauri uwe unasoma kwa makini. Nani kasema ujamaa? Tafadhari usiwe unaadika kama hujasoma tutakupuuza humu jukwaani.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom